4
Zijaribuni Hizo Roho
1 #
Mt 7:15; 1Kor 10:14; Yer 29:9; 1Kor 12:10; 2The 2:2; 1Yn 2:18 Wapendwa, msiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho mwone kama zimetoka kwa Mungu, kwa sababu manabii wengi wa uongo wametokea ulimwenguni. 2#Yn 1:4; 1Yn 2:23; 1Kor 12:3Hivi ndivyo mnavyoweza kutambua Roho wa Mungu: Kila roho inayokubali kwamba Yesu Kristo amekuja katika mwili yatoka kwa Mungu. 3#1Yn 2:22; 2Yn 7; 1Yn 2:18Lakini kila roho ambayo haimkubali Yesu haitoki kwa Mungu. Hii ndiyo roho ya mpinga Kristo, ambayo mmesikia kwamba inakuja na sasa tayari iko ulimwenguni.
4 #
Rum 8:31; 2Fal 6:16 Watoto wapendwa, ninyi mmetokana na Mungu, nanyi mmewashinda kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu. 5#Yn 17:14, 16Wao wanatokana na ulimwengu na kwa hiyo hunena yaliyo ya ulimwengu, hivyo ulimwengu huwasikiliza. 6#Yn 8:47; 14:17Sisi twatokana na Mungu na yeyote anayemjua Mungu hutusikiliza, lakini asiyetokana na Mungu hatusikilizi. Hivi ndivyo tunavyoweza kutambua Roho wa Kweli na roho ya upotovu.
Mungu Ni Pendo
7 #
1Yn 3:11; 2:4 Wapendwa, tupendane, kwa kuwa pendo latoka kwa Mungu. Kila apendaye amezaliwa na Mungu, naye anamjua Mungu. 8#1Yn 4:7, 16; 2:4; 3:6Yeye asiyependa hamjui Mungu, kwa sababu Mungu ni pendo. 9#Yn 3:16; 17; 1Yn 5:11Hivi ndivyo Mungu alivyoonyesha pendo lake kwetu: Mungu alimtuma Mwanawe wa pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kupitia kwake. 10#Rum 5:8, 10; 1Yn 2:2Hili ndilo pendo: si kwamba tulimpenda Mungu, bali yeye alitupenda, akamtuma Mwanawe, ili yeye awe dhabihu ya upatanisho kwa ajili ya dhambi zetu. 11#Yak 3:16; 1Yn 2:25; Yn 1:4; 1Yn 4:9Marafiki wapendwa, kama Mungu alivyotupenda sisi, imetupasa na sisi kupendana. 12#Yn 1:18; 1Tim 6:16Hakuna mtu yeyote aliyemwona Mungu wakati wowote. Lakini tukipendana, Mungu anakaa ndani yetu, na pendo lake limekamilika ndani yetu.
13 #
1Yn 3:24; 2:3 Tunajua kwamba twakaa ndani yake na yeye ndani yetu, kwa sababu ametupa sisi sehemu ya Roho wake. 14#Yn 15:27; Lk 2:10Nasi tumeona na kushuhudia kwamba Baba amemtuma Mwanawe ili awe Mwokozi wa ulimwengu. 15#1Yn 5:5; Rum 10:9Kila akiriye kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu, basi Mungu hukaa ndani yake, naye ndani ya Mungu. 16#1Yn 4:8, 12, 13; 3:24Hivyo nasi twajua na kulitumainia pendo la Mungu alilo nalo kwa ajili yetu.
Mungu ni Upendo. Kila akaaye katika upendo hukaa ndani ya Mungu na Mungu hukaa ndani yake. 17#1Yn 4:12; 2:5; Efe 3:12; Mt 10:15Kwa njia hii, pendo hukamilishwa miongoni mwetu ili tupate kuwa na ujasiri katika siku ya hukumu, kwa sababu kama alivyo ndivyo tulivyo sisi katika ulimwengu huu. 18#Rum 8:15; 1Yn 4:12Katika pendo hakuna hofu. Lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa sababu hofu inahusika na adhabu. Kila mwenye hofu hakukamilika katika pendo.
19 #
1Yn 4:10
Twampenda yeye kwa sababu yeye alitupenda kwanza. 20#1Yn 2:9; 3:17; Yn 1:18Ikiwa mtu atasema, “Nampenda Mungu,” lakini anamchukia ndugu yake, yeye ni mwongo. Kwa maana kila mtu asiyempenda ndugu yake ambaye anamwona, atampendaje Mungu asiyemuona? 21Naye ametupa amri hii: Yeyote anayempenda Mungu lazima pia ampende ndugu yake.