5
Kulichunga Kundi La Mungu
1 #
Mdo 11:30; Lk 24:48; 1Pet 4:13; Ufu 1:9 Kwa wazee waliomo miongoni mwenu, nawasihi mimi nikiwa mzee mwenzenu, shahidi wa mateso ya Kristo, na mshiriki katika utukufu utakaofunuliwa: 2#Yn 21:6; 1Tim 3:3lichungeni kundi la Mungu mlilokabidhiwa, mkitumika kama waangalizi, si kwa kulazimishwa bali kwa hiari, kama Mungu anavyowataka mwe; si kwa tamaa ya fedha, bali mlio na bidii katika kutumika. 3#Eze 34:4; Mt 20:25-28; Flp 3:17; 1Tim 4:12Msijifanye mabwana juu ya wale walio chini ya uangalizi wenu, bali kuweni vielelezo kwa hilo kundi. 4#1Kor 9:25; Ebr 13:20; 1Kor 9:25; 2Tim 4:8; Yak 1:12; 1Pet 1:4Naye Mchungaji Mkuu atakapodhihirishwa, mtapokea taji ya utukufu isiyoharibika.
5 #
Efe 5:21; Mit 3:34; Yak 4:6 Vivyo hivyo, ninyi mlio vijana watiini wazee. Nanyi nyote imewapasa kujivika unyenyekevu kila mtu kwa mwenzake, kwa kuwa,
“Mungu huwapinga wenye kiburi,
lakini huwapa wanyenyekevu neema.”
6 #
Yak 4:10
Basi, nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake. 7#Mit 27:5; Mt 6:25; Ebr 13:5Mtwikeni yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana na mambo yenu.
8 #
Ay 1:7; Lk 21:34, 36; 1The 5:6; 1Pet 4:7; Ufu 12:12 Mwe na kiasi na kukesha, maana adui yenu ibilisi huzungukazunguka kama simba angurumaye akitafuta mtu ili apate kummeza. 9#Yak 4:7; Kol 2:5; Mdo 14:22Mpingeni, mkiwa thabiti katika imani, mkijua ya kwamba mateso kama hayo yanawapata ndugu zenu pote duniani.
10 #
2Kor 4:17; 2The 2:17 Nanyi mkiisha kuteswa kwa kitambo kidogo, Mungu wa neema yote, aliyewaita kuingia katika utukufu wake wa milele ndani ya Kristo, yeye mwenyewe atawarejesha na kuwatia nguvu, akiwaimarisha na kuwathibitisha. 11#Rum 11:36; 1Pet 4:11; Ufu 1:6Uweza una yeye milele na milele. Amen.
Salamu Za Mwisho
12 #
2Kor 1:19; Ebr 13:22 Kwa msaada wa Silvano,#5:12 Yaani Sila. ambaye ninamhesabu kuwa ndugu mwaminifu, nimewaandikia waraka huu mfupi ili kuwatia moyo, na kushuhudia kwamba hii ni neema halisi ya Mungu. Simameni imara katika neema hiyo.
13 #
Mdo 12:12
Kanisa lililoko Babeli, lililochaguliwa pamoja nanyi, wanawasalimu; vivyo hivyo mwanangu Marko anawasalimu. 14#Rum 16:16; Efe 6:23Salimianeni kwa busu la upendo.
Amani iwe nanyi nyote mlio katika Kristo.