2 Wakorintho 6
NEN

2 Wakorintho 6

6
1 # 1Kor 3:9; 2Kor 5:20; 1Kor 15; 2 Kama watendakazi pamoja na Mungu, tunawasihi msipokee neema ya Mungu bure. 2#Isa 49; 8; Za 69:13; Isa 55:6Kwa maana asema:
“Wakati wangu uliokubalika nilikusikia,
siku ya wokovu nilikusaidia.”
Tazama, wakati uliokubalika ndio huu, siku ya wokovu ndiyo sasa.
Taabu Za Paulo
3 # Mt 5:29; Rum 14:13-20; 1Kor 8:9-13; 9:13; 10:32 Hatuweki kitu cha kukwaza katika njia ya mtu yeyote, ili huduma yetu isionekane kuwa na lawama. 4#2Kor 4:2; 1Kor 4:1Bali kama watumishi wa Mungu tuonyeshe kwa kila njia: katika saburi nyingi; katika dhiki, katika misiba, na katika shida; 5#Mdo 16:23; 2Kor 11:23-25; 1Kor 4:11katika kupigwa, katika kufungwa gerezani na katika ghasia; katika kazi ngumu, katika kukesha na katika kufunga; 6#1Kor 2:4; Rum 12:5; 1Tim 1:5; 1The 1:5katika utakatifu, katika ufahamu, katika uvumilivu, na katika utu wema; katika Roho Mtakatifu na upendo wa kweli; 7#2Kor 4:2-7; Rum 13:12; 2Kor 10:4; Efe 6:10-18katika maneno ya kweli na katika nguvu za Mungu, kwa silaha za haki za mkono wa kuume na za mkono wa kushoto; 8#1Kor 4:10-13; Mt 27:63katika utukufu na katika kudharauliwa; katika sifa mbaya na katika sifa nzuri; tukiwa kama wadanganyaji, lakini tukiwa wakweli; 9#Rum 8:36; 2Kor 1:8-10; 4:10-11tukiwa maarufu, lakini tukihesabiwa kama tusiojulikana; tukiwa kama wanaokufa, lakini tunaishi; tukipigwa, lakini hatuuawi; 10#Mt 5:12; 2Kor 7; 4; Flp 2:17; 4:4; Kol 1:24; 1The 1:6; 2Kor 8:9; Mdo 3:6; Rum 8:32tukiwa kama wenye huzuni, lakini siku zote tukifurahi; tukionekana maskini, lakini tukitajirisha wengi; tukiwa kama wasio na kitu, lakini tuna vitu vyote.
11 # 2Kor 7:3; Za 119:32 Tumesema nanyi wazi, enyi Wakorintho na kuwafungulieni mioyo yetu wazi kabisa. 12#2Nya 12:15Sisi hatujizuii kuwapenda, bali ninyi mmeuzuia upendo wenu kwetu. 13#1The 2:11; 2Kor 7:2Sasa nasema, kama na watoto wangu: Ninyi pia ifungueni mioyo yenu kabisa.
Msifungiwe Nira Pamoja Na Wasioamini
14 # Mwa 24:3; Kum 22:10; 1Kor 5:9-10; Efe 5:7-11 Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza? 15#1Kor 10:21; Mdo 5:14; 1Kor 6; 6Kuna mapatano gani kati ya Kristo na Beliari?#6:15 Beliari hapa ina maana ya uovu, kutokumcha Mungu. Yeye aaminiye ana sehemu gani na yeye asiyeamini? 16#1Kor 10:21; 3:16; Mt 16:16; Law 26:12; Yer 32:38; Eze 37:27; Ufu 21; 3Kuna mapatano gani kati ya Hekalu la Mungu na sanamu? Kwa kuwa sisi tu Hekalu la Mungu aliye hai. Kama Mungu alivyosema: “Nitakaa pamoja nao na kutembea katikati yao, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu.”
17 # Ufu 18; 4; Isa 51:11; Eze 20:34-41 “Kwa hiyo tokeni miongoni mwao,
mkatengwe nao,
asema Bwana.
Msiguse kitu chochote kilicho najisi,
nami nitawakaribisha.”
18 # Kut 4:22; 2Sam 7:14; 1Nya 17:13; Isa 43:6; Rum 8:14; 2Sam 7:8 “Mimi nitakuwa Baba kwenu,
nanyi mtakuwa wanangu na binti zangu,
asema Bwana Mwenyezi.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014