2 Samweli 22
NEN

2 Samweli 22

22
Wimbo Wa Daudi Wa Sifa
(Zaburi 18)
1 # Kut 15:1; Amu 5:1; Za 18:2-50 Daudi alimwimbia Bwana maneno ya wimbo huu wakati Bwana alipomwokoa mikononi mwa adui zake wote, na pia mkononi mwa Sauli. 2#1Sam 2:2; Za 31:3; 91:2; 71:3; 144:2; Kum 32:4; Za 18:2; Mit 18:10; Mt 18:10Akasema:
Bwana ni mwamba wangu,
ngome yangu na mwokozi wangu,
3 # Mit 10:29; Yoe 3:16; Kum 23:15; 32:37; Za 14:6; 31:2; 59:16; 71:7; 91:2; 94:22; Isa 25:4; Yer 16:19; Mwa 15:1; Kum 33:17; Lk 1:69; Za 9:9; 52:7 Mungu wangu ni mwamba wangu,
ambaye kwake ninakimbilia,
ngao yangu na pembe ya wokovu wangu.
Yeye ni ngome yangu, kimbilio langu
na mwokozi wangu,
huniokoa kutoka kwa watu wenye jeuri.
4 # Za 48:1; 96:4; 145:3 Ninamwita Bwana, anayestahili kusifiwa,
nami ninaokolewa kutoka kwa adui zangu.
5 # Za 69:14-15; Yon 2:3 “Mawimbi ya mauti yalinizunguka,
mafuriko ya maangamizi yalinilemea.
6 # Za 116:3; Mdo 2:24 Kamba za kuzimu#22:6 Kuzimu kwa Kiebrania ni Sheol, maana yake ni Shimo lisilo na mwisho. zilinizunguka,
mitego ya mauti ilinikabili.
7 # Mwa 35:3; Amu 2:15; 2Nya 15:4; Za 4:1; 77:2; 120:1; Isa 26:16; Za 34:15; 116:4; 116:4; Kut 3:7 Katika shida yangu nalimwita Bwana,
nilimlilia Mungu wangu.
Kutoka Hekaluni mwake alisikia sauti yangu,
kilio changu kikafika masikioni mwake.
8 # Amu 5:4; Za 97:4; Kut 19:18; Za 68:8; 77:18; Yer 10:10; Ay 9:6; 26:11; Za 75:3 “Dunia ilitetemeka na kutikisika,
misingi ya mbingu ikatikisika,
vilitetemeka kwa sababu
alikuwa amekasirika.
9 # Za 50:3; 97:3; Ebr 12:29; Ufu 11:5; Isa 6:6; Eze 1:13; 10:2; Hab 3:5 Moshi ukapanda kutoka puani mwake,
moto uteketezao ukatoka kinywani mwake,
makaa ya moto yawakayo
yakatoka ndani mwake.
10 # Kut 19:9; Law 16:2; Kum 33:26; 1Fal 8:12; Ay 26:9; Za 104:3; Isa 19:1; Yer 4:13; Nah 1:3; Isa 64:1 Akazipasua mbingu akashuka chini,
mawingu meusi yalikuwa chini ya miguu yake.
11 # Mwa 3:24; Kut 25:22; Za 104:3 Alipanda juu ya kerubi akaruka,
akapaa juu kwa mbawa za upepo.
12 # Kut 19:9 Alifanya giza hema lake la kujifunika:
mawingu meusi ya mvua ya angani.
13 # Ay 37:3; Za 77:18 Kutokana na mwanga wa uwepo wake
mawingu yalisogea,
ikanyesha mvua ya mawe
na umeme wa radi.
14 # 1Sam 2:10; Isa 30:30 Bwana alinguruma kutoka mbinguni,
sauti ya Aliye Juu Sana ilisikika.
15 # Kum 32:23; Za 7:13; 77:7; Hab 3:11 Aliipiga mishale na kutawanya adui,
umeme wa radi na kuwafukuza.
16 # Za 6:1; 50:8, 21; 106:9; Nah 1:4; Isa 30:33; 40:24; Kut 14:21 Mabonde ya bahari yalifunuliwa,
na misingi ya dunia ikawa wazi
kwa kukaripia kwake Bwana,
kwa uvumi wa pumzi kutoka puani mwake.
17 # Za 144:7; Kut 2; 10 “Alinyoosha mkono kutoka juu na kunishika;
alinitoa kutoka kilindi cha maji makuu.
18 # Lk 1:71 Aliniokoa kutoka adui wangu mwenye nguvu nyingi,
kutoka adui zangu waliokuwa na nguvu nyingi kuliko mimi.
19 # Za 23:4 Walinikabili siku ya msiba wangu,
lakini Bwana alikuwa msaada wangu.
20 # Ay 36:16; Za 31:8; 118:5; 22:8; Isa 42:1; Mt 12:18; 2Sam 15:26 Alinileta nje mahali penye nafasi tele,
akaniokoa kwa kuwa alipendezwa nami.
21 # 1Sam 26:23; Za 26:6; Ay 17:9; 22:30; 42:7-8; Za 24:4 Bwana alinitendea sawasawa na uadilifu wangu;
sawasawa na usafi wa mikono yangu amenilipa.
22 # Mwa 18:19; Za 128:1; Mit 8:32 Kwa maana nimezishika njia za Bwana;
sijatenda ubaya nikamwacha Mungu wangu.
23 # Kum 6:4-9; Za 119:30-32, 102; Kum 7:12 Sheria zake zote zi mbele yangu,
wala sijayaacha maagizo yake.
24 # Mwa 6:9; Efe 1:4; Yn 1:47 Nimekuwa sina hatia mbele zake,
nami nimejilinda nisitende dhambi.
25 # 1Sam 26:23 Bwana amenilipa sawasawa na uadilifu wangu,
sawasawa na usafi wangu machoni pake.
26 # Mt 5:7 “Kwa yeye aliye mwaminifu unajionyesha kuwa mwaminifu,
kwa asiye na hatia unajionyesha kutokuwa na hatia,
27 # Mt 5:8; Law 26:23-24 # 1Nya 27:9-10 kwa aliye mtakatifu unajionyesha kuwa mtakatifu,
lakini kwa aliyepotoka unajionyesha kuwa mkaidi.
28 # Kut 3:8; 1Sam 2:8-9; Za 72:12-13; Mit 30:13; Dan 4:31; Sef 3:11; Isa 2:12-17; 5:15; Za 12:5; Mt 5:3 Wewe huwaokoa wanyenyekevu,
lakini macho yako ni juu ya wenye kiburi
ili uwashushe.
29 # Za 27:1; Isa 2:5; Mik 7:8; Ufu 21:23; 22:5 Wewe ni taa yangu, Ee Bwana.
Bwana hulifanya giza langu
kuwa mwanga.
30Kwa msaada wako naweza kushinda jeshi,
nikiwa pamoja na Mungu wangu
nitaweza kuruka ukuta.
31 # Kum 32:4; Mt 5:48; Za 12:6; 119:140; Mit 30:5-6; Mwa 15:1; Dan 4:37; Ufu 15:3 “Kuhusu Mungu, njia yake ni kamilifu;
neno la Bwana halina dosari.
Yeye ni ngao kwa wote
wanaokimbilia kwake.
32 # Kut 32:31; 1Sam 2:2; Isa 45:5-6 Kwa maana ni nani aliye Mungu
zaidi ya Bwana?
Ni nani aliye Mwamba
isipokuwa Mungu wetu?
33 # 1Sam 2:2; 2Sam 7:22; Za 27:1; Kum 18:13 Mungu ndiye anivikaye nguvu
na kufanya njia yangu kuwa kamilifu.
34 # Isa 35:6; Hab 3:19; Kum 32:13 Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu,
huniwezesha kusimama mahali palipo juu.
35 # Za 144:1; 7:12; 11:2; Zek 9:13 Huifundisha mikono yangu kupigana vita;
mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.
36 # Efe 6:16 Hunipa ngao yako ya ushindi,
unajishusha chini ili kuniinua.
37 # Mit 4:11 Huyapanua mapito yangu,
ili miguu yangu isiteleze.
38“Niliwafuatia adui zangu na nikawaseta,
sikurudi nyuma mpaka walipoangamizwa.
39 # Za 44:5; 110:6; Mal 4:3 Niliwaseta kabisa, nao hawakuweza kuinuka tena;
walianguka chini ya miguu yangu.
40 # Yos 10:24; 1Fal 5:3; Za 44:5 Ulinivika nguvu kwa ajili ya kupigana vita;
uliwafanya adui zangu wasujudu miguuni pangu.
41 # Kut 23:27 Uliwafanya adui zangu wageuke na kukimbia,
nami nikawaangamiza adui zangu.
42 # Isa 1:15; Za 50:22; 1Sam 14:37; 28:6; Ay 27:6; Mit 1:28 Walipiga yowe, lakini hapakuwepo na yeyote wa kuwaokoa;
walimlilia Bwana, lakini hakuwajibu.
43 # 1Fal 20:10; 2Fal 13:7; Isa 41:2; Amo 1:3; Za 7:5; Isa 41:25; Mik 7:10; Zek 10:5; Isa 5:25; 10:6; 22:5 Niliwaponda kama mavumbi ya nchi;
niliwaponda na kuwakanyaga kama tope barabarani.
44 # Kut 11:3; 2Sam 3:1; 8:1-14; Isa 55:3-5; Kum 28:13 “Umeniokoa kutokana na mashambulizi ya watu wangu;
umenihifadhi mimi kama kiongozi wa mataifa.
Watu ambao sikuwajua wananitumikia,
45 # Za 66:3; 81:15; Kum 33:29 nao wageni huja wakininyenyekea,
mara wanisikiapo, hunitii.
46 # Mik 7:17 Wote wanalegea,
wanatoka katika ngome zao wakitetemeka.
47 # Kut 15:2; Kum 32:15; Za 18:31; 89:26; 95:1 Bwana yu hai! Sifa ni kwa Mwamba wangu!
Atukuzwe Mungu,
Mwamba, Mwokozi wangu!
48 # Hes 31:3; Za 144:2; 1Sam 25:39; Za 94:1 Yeye ndiye Mungu anilipiziaye kisasi,
ayawekaye mataifa chini yangu,
49 # Za 140:1; 27:6 aniwekaye huru toka kwa adui zangu.
Uliniinua juu ya adui zangu;
uliniokoa toka kwa watu wajeuri.
50 # Za 9:11; 47:6; 68:4; Rum 15:9 Kwa hiyo nitakusifu, Ee Bwana,
katikati ya mataifa;
nitaliimbia sifa jina lako.
51 # Za 21:1; 144:9-10; 1Sam 16; 13; Za 89:20; Mdo 13:23; 2Sam 7:13; Za 89:24, 29 Humpa mfalme wake ushindi mkuu;
huonyesha fadhili zake kwa mpakwa mafuta wake,
kwa Daudi na wazao wake milele.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014