2 Wathesalonike 3
NEN

2 Wathesalonike 3

3
Hitaji La Maombi
1 # 1The 4:1; 5:25; 1:8 Hatimaye, ndugu, tuombeeni ili Neno la Bwana lipate kuenea kwa haraka na kuheshimiwa kila mahali, kama vile ilivyokuwa kwenu. 2#Rum 15:31Ombeni pia ili tupate kuokolewa kutokana na watu waovu na wabaya, kwa maana si wote wanaoamini. 3#1Kor 1:9; Mt 5:37Lakini Bwana ni mwaminifu, naye atawaimarisha ninyi na kuwalinda kutokana na yule mwovu. 4#2Kor 2:3Nasi tuna tumaini katika Bwana ya kuwa mnafanya na mtaendelea kufanya yale tuliyowaagiza. 5#1Nya 29:18Bwana aiongoze mioyo yenu katika upendo wa Mungu na katika saburi ya Kristo.
Onyo Dhidi Ya Uvivu
6 # 1Kor 5:4; Rum 16:17; 1Kor 11:2 Ndugu, tunawaagiza katika Jina la Bwana Yesu Kristo, jitengeni na kila ndugu ambaye ni mvivu na ambaye haishi kufuatana na maagizo tuliyowapa. 7#1Kor 4:16Maana ninyi wenyewe mnajua jinsi iwapasavyo kufuata mfano wetu. Sisi hatukuwa wavivu tulipokuwa pamoja nanyi, 8#Mdo 18:3; Efe 4:28wala hatukula chakula cha mtu yeyote pasipo kukilipia. Badala yake tulifanya kazi kwa bidii usiku na mchana, ili tusimlemee mtu yeyote miongoni mwenu. 9#1Kor 9:4-14; 4:16Tulifanya hivi, si kwa sababu hatukuwa na haki ya kupata msaada kama huo, bali ndio sisi wenyewe tuwe kielelezo. 10#1The 3:4; 4:11Kwa maana hata tulipokuwa pamoja nanyi, tuliwapa amri kwamba: “Mtu yeyote asiyetaka kufanya kazi, hata kula asile.”
11 # 1Tim 5:13 Kwa kuwa tunasikia kwamba baadhi ya watu miongoni mwenu ni wavivu. Hawafanyi kazi bali hujishughulisha na mambo ya wengine. 12#1The 4:1; 4:11; Efe 4:28Basi watu kama hao tunawaagiza na kuwahimiza katika Bwana Yesu Kristo, kwamba wafanye kazi kwa utulivu kwa ajili ya chakula chao wenyewe. 13#Gal 6:9Kwa upande wenu, ndugu, ninyi kamwe msichoke katika kutenda mema.
14 # Rum 16:17 Ikiwa mtu yeyote hayatii maagizo yetu yaliyoko katika barua hii, mwangalieni sana mtu huyo. Msishirikiane naye, ili apate kuona aibu. 15#Gal 6:1Lakini msimhesabu kuwa adui, bali mwonyeni kama ndugu.
Salamu Za Mwisho
16 # Rum 15:33; Rut 2:4 Basi, Bwana wa amani mwenyewe awapeni amani nyakati zote na kwa kila njia. Bwana awe nanyi nyote.
17 # 1Kor 16:21 Mimi, Paulo, ninaandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Hii ndio alama ya utambulisho katika barua zangu zote. Hivi ndivyo niandikavyo.
18 # Rum 16:20 Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo iwe nanyi nyote. Amen.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014