Amosi 6
NEN

Amosi 6

6
Ole Kwa Wanaoridhika
1 # Lk 6:24; Isa 32:9-11; Ay 24:23; Sef 1:12; Amo 3:9 Ole wenu ninyi mnaostarehe na kuridhika katika Sayuni,
na ninyi mnaojisikia salama juu ya Mlima Samaria,
ninyi watu mashuhuri wa taifa lililoendelea kuliko mataifa mengine,
ambao watu wa Israeli wanawategemea!
2 # 2Fal 17:24; Yer 49:23; Isa 10:9; 2Fal 14:25; Hes 34:8; Mwa 10:10; 2Nya 26:6; Yos 11:22 Nendeni Kalne mkaone kutoka huko;
mwende hadi Hamathi iliyo kuu,
kisha mshuke hadi Gathi ya Wafilisti.
Je, wao ni bora kuliko falme zenu mbili?
Je, nchi yao ni kubwa kuliko yenu?
3 # Isa 47:7; 56:12; Eze 12:22, 27; Mhu 8:11; Amo 5:18; 9:10 Mnaiweka mbali siku iliyo mbaya
na kuleta karibu utawala wa kuogofya.
4 # Isa 1:11; Eze 34:2-3; Amo 3:12; Mit 3:12; 7:17; Es 1:6 Ninyi mnalala juu ya vitanda vilivyofunikwa kwa pembe za ndovu,
na kujinyoosha juu ya viti vya fahari.
Mnajilisha kwa wana-kondoo wazuri
na ndama walionenepeshwa.
5 # Isa 5:12; 14:11; Za 137:2; Amo 5:23; 1Nya 15:16 Ninyi mnapiga vinubi kama Daudi,
huku mkitunga nyimbo za vinanda mbalimbali.
6 # Isa 28:1; Amo 2:8; Eze 9:4; 16:49 Mnakunywa mvinyo kwa bakuli zilizojazwa,
na mnajipaka mafuta mazuri,
lakini hamhuzuniki kwa maangamizi ya Yosefu.
7Kwa hiyo mtakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kwenda uhamishoni;
karamu zenu na kustarehe kutakoma.
Bwana Anachukia Kiburi Cha Israeli
8 # Mwa 22:16; Ebr 6:13; Law 26:19, 30; Za 47:4; Kum 32:19; Yer 12:8; Amo 4:2 Bwana Mwenyezi ameapa kwa nafsi yake mwenyewe: Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema:
“Nachukia kiburi cha Yakobo,
nachukia ngome zake;
nitautoa mji wao na kila kitu
kilichomo ndani mwake.”
9Kama watu kumi watabaki katika nyumba moja, wao pia watakufa. 10#1Sam 31:12; Amo 8:3Kama jamaa ambaye atachoma miili akija ili kuitoa nje ya nyumba, na kumuuliza yeyote ambaye bado anajificha humo, “Je, yuko mtu yeyote pamoja nawe?” Naye akisema, “Hapana,” ndipo atakaposema, “Nyamaza kimya! Haturuhusiwi kutaja jina la Bwana.”
11 # Amo 3:15; Isa 55:11; 34:5 Kwa kuwa Bwana ameamuru,
naye atabomoa jumba kubwa vipande vipande
na nyumba ndogo vipande vidogo vidogo.
12 # Hos 10:4; Isa 1:21; Amo 5:7; 3:10 Je, farasi waweza kukimbia kwenye miamba mikali?
Je, aweza mtu kulima huko kwa maksai?
Lakini mmegeuza haki kuwa sumu
na matunda ya uadilifu kuwa uchungu:
13 # Ay 13:8; 8:15; Isa 28:14-15 ninyi mnaoshangilia kushindwa kwa Lo-Debari
na kusema, “Je, hatukuteka Karnaimu kwa nguvu zetu wenyewe?”
14 # Yer 5:15; Hes 13:21; 1Fal 8:65; Amo 3:11 Maana Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote asema,
“Nitainua taifa dhidi yenu, ee nyumba ya Israeli,
nalo litawatesa kuanzia Lebo-Hamathi
hadi Bonde la Araba.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014