Amosi 7
NEN

Amosi 7

7
Maono Ya Kwanza: Nzige
1 # Amo 8:1; Za 78:46; Yer 51:14; Yoe 1:4 Hili ndilo alilonionyesha Bwana Mwenyezi katika maono: Alikuwa anaandaa makundi ya nzige baada ya kuvunwa fungu la mfalme na wakati ule tu mimea ya pili ilipokuwa ikichipua. 2#Kut 10:15; Eze 11:13; Isa 37:4; Amo 4:9Wakati nzige walikuwa wamekula mimea yote ya nchi, nililia kwa sauti kuu, “Bwana Mwenyezi, samehe! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”
3 # Kut 32:14; Yon 3:10; Kum 32:36; Za 106:45; 1Nya 21:15; Hos 11:8; Yoe 2:14; Yak 5:16; Yer 18:8; 26:19 Kwa hiyo Bwana akaghairi.
Kisha Bwana akasema, “Hili halitatokea.”
Maono Ya Pili: Moto
4 # Isa 66:16; Yoe 1:19; Kum 32:22 Hili ndilo Bwana Mwenyezi alilonionyesha katika maono: Bwana Mwenyezi alikuwa akiita hukumu ya moto; nao ulikausha vilindi vikuu, ukateketeza nchi. 5#Yoe 2:17Ndipo nikalia, “Bwana Mwenyezi, nakusihi, zuia! Je, Yakobo atawezaje kuendelea kuishi? Yeye ni mdogo sana!”
6 # Kut 32:14; Yer 18:8; 42:10; Za 102:17; Yon 3:10; Eze 9:8 Kwa hiyo Bwana akaghairi.
Bwana Mwenyezi akasema, “Hili nalo halitatokea.”
Maono Ya Tatu: Timazi
7Hili ndilo alilonionyesha katika maono: Bwana alikuwa amesimama karibu na ukuta ambao ulikuwa umejengwa kwa timazi, akiwa na uzi wa timazi mkononi mwake. 8#Isa 28:17; Mao 2:8; 2Fal 21:13; Eze 7:2-9; Yer 1:11-13; 15:6; Mik 7:18Naye Bwana akaniuliza, “Je, Amosi unaona nini?”
Nikamjibu, “Uzi wa timazi.”
Kisha Bwana akasema, “Tazama, ninaweka uzi wa timazi miongoni mwa watu wangu Israeli; sitawahurumia tena.
9 # Law 26:31; Mwa 26:23; 2Fal 14:23; 1Fal 13:34; 2Fal 15:9-10; Isa 63:18; Hos 10:8 “Mahali pa Isaki pa juu pa kuabudia miungu pataangamizwa,
na mahali patakatifu pa Israeli pa kuabudia pataharibiwa;
kwa upanga wangu nitainuka
dhidi ya nyumba ya Yeroboamu.”
Amosi Na Amazia
10 # 1Fal 12:32; Yos 7:2; 2Fal 14:23-24; Yer 38:4; 26:8-11 Kisha Amazia kuhani wa Betheli akatuma ujumbe kwa Yeroboamu mfalme wa Israeli, akisema: “Amosi analeta fitina juu yako katikati ya Israeli. Nchi haiwezi kuvumilia maneno yake yote. 11#Amo 5:27; Yer 36:16Kwa kuwa hili ndilo Amosi analosema:
“ ‘Yeroboamu atakufa kwa upanga,
na kwa hakika Israeli watakwenda uhamishoni,
mbali na nchi yao.’ ”
12 # Mt 8:34; 1Sam 9:9 Kisha Amazia akamwambia Amosi, “Nenda zako, ewe mwonaji! Urudi katika nchi ya Yuda. Ujipatie riziki yako huko na kutoa unabii wako. 13#Yer 20:2; 36:5; Amo 2:12; Mdo 4:18; Yos 7:2; 1Fal 12:29Usiendelee kutoa unabii katika Betheli, kwa sababu hapa ni mahali pa mfalme pa kuabudia na Hekalu la ufalme huu.”
14 # 1Sam 10:5; Zek 13:5; 2Fal 2:5; 4:38; Isa 9:10; 1Fal 10:27 Amosi akamjibu Amazia, “Mimi sikuwa nabii wala mwana wa nabii, lakini nilikuwa mchungaji wa kondoo na mtunza mikuyu. 15#Mwa 37:5; 2Sam 7:8; Yer 7:1-2; 26:12; Eze 2:3-4; Isa 6:9Lakini Bwana akanitoa kutoka kuchunga kondoo na kuniambia, ‘Nenda, ukawatabirie watu wangu Israeli.’ 16#Isa 30:10; Eze 20:46; Mik 2:6; Yer 22:2Sasa basi, sikieni neno la Bwana. Ninyi mnasema,
“ ‘Usitabiri dhidi ya Israeli,
na uache kuhubiri dhidi ya nyumba ya Isaki.’
17 # Hos 4:13; 9:3; Eze 4:13; Yer 28:12; 29:21; Mao 5:11; Amo 5:27; 2:12-13; 2Fal 17:6 “Kwa hiyo hili ndilo asemalo Bwana:
“ ‘Mke wako atakuwa kahaba mjini,
nao wana wako na binti zako watauawa kwa upanga.
Shamba lako litapimwa na kugawanywa,
na wewe mwenyewe utafia katika nchi ya kipagani.
Nayo Israeli kwa hakika itakwenda uhamishoni,
mbali na nchi yao.’ ”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014