Wakolosai 4
NEN

Wakolosai 4

4
1 # Law 25:43, 53 Ninyi mabwana, watendeeni watumwa wenu yaliyo haki na yanayostahili, mkitambua ya kwamba ninyi pia mnaye Bwana mbinguni.
Maagizo Zaidi
2 # Lk 18:1; 1The 5:17; Efe 6:18; Flp 4:6 Dumuni sana katika maombi, mkikesha katika hayo pamoja na kushukuru. 3#Mdo 14:27; Efe 6:19-20; Rum 15:30; 1Kor 16:9Pia tuombeeni na sisi ili Mungu atufungulie mlango wa kunena, ili tupate kuitangaza siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake pia mimi nimefungwa. 4#Efe 6:20Ombeni ili nipate kuitangaza Injili kwa udhahiri kama ipasavyo kunena. 5#Efe 5:15; Mk 4:11; Efe 5:16Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati. 6#Efe 4:29; Mk 9:50; 1Pet 3:15Maneno yenu yawe yamejaa neema siku zote, yanayofaa, ili mjue jinsi iwapasavyo na inavyofaa kumjibu kila mtu.
Salamu Za Mwisho
7 # Mdo 20:4; Efe 6:21-22 Tikiko atawaambia habari zangu zote. Yeye ni ndugu mpendwa, mtendakazi mwaminifu na mtumishi mwenzangu katika Bwana. 8#Efe 6:22; 6:21Nimemtuma kwenu kwa madhumuni haya ili mpate kufahamu hali yetu, na pia awatie moyo. 9#Flp 1:10; Flm 10; Kol 4:12Anakuja pamoja na Onesimo, ndugu yetu mpendwa na mwaminifu, ambaye ni mmoja wenu. Watawaambia mambo yote yanayotendeka hapa kwetu.
10 # Mdo 19:21; 4:36 Aristarko aliye mfungwa pamoja nami anawasalimu, vivyo hivyo Marko, binamu yake Barnaba. (Mmeshapata maagizo yanayomhusu; akija kwenu, mpokeeni.) 11#Flp 2:25Yesu, yeye aitwaye Yusto, pia anawasalimu. Hawa peke yao ndio Wayahudi miongoni mwa watendakazi wenzangu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu, nao wamekuwa faraja kwangu. 12#Kol 1:7; Flp 1:23; Rum 15:30; 1Kor 2:6Epafra, ambaye ni mmoja wenu na mtumishi wa Kristo Yesu, anawasalimu. Yeye siku zote anawaombea kwa bidii kwamba msimame imara katika mapenzi yote ya Mungu, mkiwa wakamilifu na thabiti. 13#Kol 2:1Ninashuhudia kumhusu kwamba anafanya kazi kwa bidii kwa ajili yenu, na kwa ajili ya ndugu wa Laodikia na wale wa Hierapoli. 14#2Tim 4:11; Flp 1:24; 2Tim 4:10Rafiki yetu mpenzi Luka yule tabibu, pamoja na Dema, wanawasalimu. 15#Rum 16:5Wasalimuni ndugu wote wa Laodikia, na pia Nimfa, pamoja na kanisa linalokutana katika nyumba yake.
16 # 2The 3:14 Baada ya barua hii kusomwa kwenu, hakikisheni kwamba inasomwa pia katika kanisa la Walaodikia. Nanyi pia msome barua inayotoka Laodikia.
17 # Flp 1:2; 2Tim 4:5 Mwambieni Arkipo hivi: “Hakikisha kuwa unakamilisha ile huduma uliyopokea katika Bwana.”
18 # 1Kor 16:21; Ebr 13:3 Mimi, Paulo, naandika salamu hizi kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni minyororo yangu. Neema iwe nanyi. Amen.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014