Mhubiri 11
NEN

Mhubiri 11

11
Mkate Juu Ya Maji
1 # Kum 15:10; 24:19; Hos 10:12; Mt 10:42; Isa 32:20; Mit 19:17 Tupa mkate wako juu ya maji,
kwa maana baada ya siku nyingi
utaupata tena.
2 # Mik 5:5; Efe 5:16; Za 112:9 Wape sehemu watu saba, naam hata wanane,
kwa maana hujui ni baa gani
litakalokuwa juu ya nchi.
3Kama mawingu yamejaa maji,
hunyesha mvua juu ya nchi.
Kama mti ukianguka kuelekea kusini
au kuelekea kaskazini,
mahali ulipoangukia,
hapo ndipo utakapolala.
4Yeyote atazamaye upepo hatapanda,
yeyote aangaliaye mawingu hatavuna.
5 # Za 139:14-16; Yn 3:8-10 Kama vile usivyofahamu njia ya upepo,
au jinsi mwili uumbwavyo
ndani ya tumbo la mama,
vivyo hivyo huwezi kufahamu kazi ya Mungu,
Muumba wa vitu vyote.
6 # Mhu 9:10 Panda mbegu yako asubuhi,
nako jioni usiruhusu mikono yako ilegee,
kwa maana hujui ni ipi itakayofanikiwa,
kwamba ni hii au ni ile,
au kwamba zote zitafanikiwa sawasawa.
Mkumbuke Muumba Wako Ukiwa Bado Kijana
7 # Mhu 7:11 Nuru ni tamu,
tena inafurahisha macho kuona jua.
8Hata kama mtu ataishi miaka mingi kiasi gani,
na aifurahie yote.
Lakini na akumbuke siku za giza,
kwa maana zitakuwa nyingi.
Kila kitu kitakachokuja ni ubatili.
9 # Ay 19:29; Kum 29:19; Mdo 14:16; Rum 14:10; Mhu 2:24; 3:17 Furahi ewe kijana, wakati ungali kijana,
moyo wako na ukupe furaha
katika siku za ujana wako.
Fuata njia za moyo wako
na chochote macho yako yaonayo,
lakini ujue kwamba kwa ajili ya haya yote
Mungu atakuleta hukumuni.
10 # 2Kor 7:1; Za 94:19; Mhu 2:24 Kwa hiyo basi, ondoa wasiwasi moyoni mwako
na utupilie mbali masumbufu ya mwili wako,
kwa kuwa ujana na nguvu ni ubatili.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014