11
Upendo Wa Mungu Kwa Israeli
1 #
Kut 4:22; Mt 2:15; Yer 2:2; Eze 16:22; Hos 12:9; 13:4 “Wakati Israeli alipokuwa mtoto, nilimpenda,
nilimwita mwanangu kutoka Misri.
2 #
Hos 2:13; 4:13; 2Fal 17:15; Isa 65:7; Yer 18:15 Lakini kadiri nilivyomwita Israeli,
ndivyo walivyokwenda mbali nami.
Walitoa dhabihu kwa Mabaali
na kufukiza uvumba kwa vinyago.
3 #
Kum 1:31; 32:11; Kut 15:26; Yer 30:17 Mimi ndiye niliyemfundisha Efraimu kutembea,
nikiwashika mikono;
lakini hawakutambua
kuwa ni mimi niliyewaponya.
4 #
Yer 31:2-3, 20; Law 26:13; Kut 16:32; Za 78:25 Niliwaongoza kwa kamba za huruma ya kibinadamu,
kwa vifungo vya upendo;
niliondoa nira shingoni mwao
nami nikainama kuwalisha.
5 #
Yer 8:4-6; Hos 7:16; 10:6; Kut 13:17 “Je, hawatarudi Misri,
nayo Ashuru haitawatawala
kwa sababu wamekataa kutubu?
6 #
Hos 13:16; Mao 2:9 Panga zitametameta katika miji yao,
zitaharibu makomeo ya malango yao
na kukomesha mipango yao.
7 #
Yer 3:6-7; 8:5; Isa 26:10 Watu wangu wamedhamiria kuniacha.
Hata kama wakimwita Yeye Aliye Juu Sana,
kwa vyovyote hatawainua.
8 #
Mwa 14:8; 19:25; Hos 6:4; Mao 3:32; Yer 7:29; Za 25:6; 1Fal 3:26 “Efraimu, ninawezaje kukuacha?
Ee Israeli, ninawezaje kukutoa?
Nitawezaje kukutendea kama Adma?
Nitawezaje kukufanya kama Seboimu?
Moyo wangu umegeuka ndani yangu,
huruma zangu zote zimeamshwa.
9 #
Kum 13:17
Sitatimiza hasira yangu kali,
wala sitageuka na kumharibu Efraimu.
Kwa kuwa mimi ndimi Mungu,
wala si mwanadamu,
Aliye Mtakatifu miongoni mwenu.
Sitakuja kwa ghadhabu.
10 #
Hos 3:5; 6:1-3; Isa 31:4; 42:13; Za 18:45 Watamfuata Bwana;
atanguruma kama simba.
Wakati angurumapo,
watoto wake watakuja wakitetemeka
kutoka magharibi.
11 #
Isa 11:11; Mwa 8:8; Eze 28:26; 34:25-28 Watakuja wakitetemeka
kama ndege wakitoka Misri,
kama hua wakitoka Ashuru.
Nitawakalisha katika nyumba zao,”
asema Bwana.
Dhambi Ya Israeli
12 #
Hos 4:2; 10:13; Kum 7:9 Efraimu amenizunguka kwa uongo,
nyumba ya Israeli kwa udanganyifu.
Naye Yuda ni mkaidi dhidi ya Mungu,
hata kinyume cha yule mwaminifu Aliye Mtakatifu.