12
1 #
Mwa 41:6; Eze 17:10; 2Fal 17:4; Za 78:67; Hos 4:19; 5:13 Efraimu anajilisha upepo;
hufukuzia upepo wa mashariki kutwa nzima
na kuzidisha uongo na jeuri.
Anafanya mkataba na Ashuru
na kutuma mafuta ya zeituni Misri.
2 #
Ay 10:2
#
Mik 6:2; Hos 4:9; 9:15; Kut 32:34; Amo 2:4 Bwana analo shtaka dhidi ya Yuda,
atamwadhibu Yakobo kwa kadiri ya njia zake
na kumlipa kwa kadiri ya matendo yake.
3 #
Mwa 25:26; 32:24-29 Yakobo akiwa tumboni alishika kisigino cha kaka yake;
kama mwanadamu, alishindana na Mungu.
4 #
Mwa 12:8; 28:12-15; 35:15 Alishindana na malaika na kumshinda;
alilia na kuomba upendeleo wake.
Alimkuta huko Betheli
na kuzungumza naye huko:
5 #
Kut 3:15
Bwana Mungu Mwenye Nguvu Zote,
Bwana ndilo jina lake!
6 #
Mik 6:8; 7:7; Za 106:13; Eze 18:30; Isa 19:22; Yoe 2:12; Yer 22:3 Lakini ni lazima urudi kwa Mungu wako;
dumisha upendo na haki,
nawe umngojee Mungu wako siku zote.
7 #
Law 19:26; Amo 8:5 Mfanyabiashara hutumia vipimo vya udanganyifu;
hupenda kupunja.
8 #
Za 62:10; Ufu 3:17; Eze 28:5 Efraimu hujisifu akisema,
“Mimi ni tajiri sana; nimetajirika.
Pamoja na utajiri wangu wote hawatakuta ndani yangu
uovu wowote au dhambi.”
9 #
Law 23:43; Hos 2:15; Neh 8:17 “Mimi ndimi Bwana Mungu wenu
niliyewaleta kutoka Misri;
nitawafanya mkae tena kwenye mahema,
kama vile katika siku
za sikukuu zenu zilizoamriwa.
10 #
Amu 14:12; Eze 20:49; 2Fal 17:13; Yer 7:25 Niliongea na manabii, nikawapa maono mengi
na kusema mifano kupitia wao.”
11 #
Amo 4:4; Hos 4:15; 6:8; 8:11 Je, Gileadi si mwovu?
Watu wake hawafai kitu!
Je, hawatoi dhabihu za mafahali huko Gilgali?
Madhabahu zao zitakuwa
kama malundo ya mawe
katika shamba lililolimwa.
12 #
Mwa 28:5; 29:18 Yakobo alikimbilia katika nchi ya Aramu;
Israeli alitumika ili apate mke,
ili aweze kulipa kwa ajili yake alichunga kondoo.
13 #
Kut 14:19-22; Isa 63:11-14; Kut 13:3; Hos 11:1 Bwana alimtumia nabii
kumpandisha Israeli kutoka Misri,
kwa njia ya nabii alimtunza.
14 #
Eze 18:13; Dan 11:18 Lakini Efraimu amemchochea sana hasira;
Bwana wake ataleta juu yake
hatia yake ya kumwaga damu naye atamlipiza
kwa ajili ya dharau yake.