Hosea 3
NEN

Hosea 3

3
Upatanisho Wa Hosea Na Mkewe
1 # Hos 1:2; 2Sam 6:19 Bwana akaniambia, “Nenda, ukaonyeshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kama Bwana apendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.”
2Basi nilimnunua huyo mwanamke kwa shekeli kumi na tano#3:2 Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 170. za fedha, pia kwa kiasi kama cha homeri moja na nusu#3:2 Homeri moja na nusu ni kama lita 330. ya shayiri. 3#Kum 21:23Kisha nilimwambia, “Utaishi nami kwa siku nyingi, hupaswi kuwa kahaba au kuwa na uhusiano wa karibu na mtu yeyote, nami nitaishi na wewe.”
4 # Hos 2:11; 13:11; Dan 11:31; Amu 18:14-17, 23-24; Mao 2:9; Kum 28:6; Zek 10:2; Kut 25:7 Kwa maana Waisraeli wataishi siku nyingi bila kuwa na mfalme wala mkuu, bila kuwa na dhabihu wala mawe matakatifu, bila kisibau wala sanamu. 5#1Sam 13:14; Eze 34:23-24; Kum 4:30; Yer 50:4-5; Isa 9:13; 10:20; Hos 5:15; Mik 4:1-2; Za 18:45Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa Bwana na kwa baraka zake katika siku za mwisho.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014