Ayubu 13
NEN

Ayubu 13

13
1 # Ay 9:24 “Macho yangu yameona hili lote,
masikio yangu yamesikia na kulielewa.
2 # Ay 12:3 Hayo mnayoyajua mimi pia ninayajua;
mimi si mtu duni kuliko ninyi.
3 # Ay 5:8; 23:3-4; 5:17; 40:2 Lakini ninayo shauku ya kuzungumza na Mwenyezi
na kuhojiana shauri langu na Mungu.
4 # Isa 9:15; Yer 23:32; Za 119:69; Yer 8:22; Ay 6:15 Ninyi, hata hivyo, hunipakaza uongo;
ninyi ni matabibu wasiofaa kitu, ninyi nyote!
5 # Mit 17:28; Amo 5:13; Ay 13:13; Amu 18:19; Mhu 5:3; Yak 1:19 Laiti wote mngenyamaza kimya!
Kwa kuwa kwenu hilo lingekuwa hekima.
6 # Ay 33:1; 36:4 Sikieni sasa hoja yangu;
sikilizeni kusihi kwangu.
7 # Ay 16:17; 36:4; 17:5; Rum 3:5-8 Je, mtazungumza kwa uovu kwa niaba ya Mungu?
Je, mtazungumza kwa udanganyifu kwa niaba yake?
8 # Law 19:15; Mit 24:23 Mtamwonyesha upendeleo?
Mtamtetea Mungu kwenye mashtaka yake?
9 # Ay 12:16; 9:3; Gal 6:7 Je, ingekuwa vyema Mungu akiwahoji ninyi?
Je, mngeweza kumdanganya kama ambavyo mngeweza kuwadanganya wanadamu?
10 # Law 19:15; 2Nya 19:7 Hakika angewakemea
kama mkiwapendelea watu kwa siri.
11 # Ay 31:23; Kut 3:6 Je, huo ukuu wake haungewatisha ninyi?
Je, hofu yake isingewaangukia ninyi?
12 # Neh 4:2-3 Maneno yenu ni mithali za majivu;
utetezi wenu ni ngome za udongo wa mfinyanzi.
13 # Ay 13:5; 7:11; 9:21 “Nyamazeni kimya nipate kusema;
kisha na yanipate yatakayonipata.
14 # Amu 9:17; Za 119:109 Kwa nini nijiweke mwenyewe kwenye hatari
na kuyaweka maisha yangu mikononi mwangu?
15 # Za 27:1; Dan 3:28; Ay 5:8; 27:5; Mit 14:32; Rum 8:38-39 Ingawa ataniua, bado nitamtumaini;
hakika nitazitetea njia zangu mbele zake.
16 # Hos 14:4; Flp 1:19; Isa 12:1-2 Naam, hili litanigeukia kuwa wokovu wangu,
kwa maana hakuna mtu asiyemcha Mungu
atakayethubutu kuja mbele yake!
17 # Ay 21:2 Sikilizeni maneno yangu kwa makini;
nayo masikio yenu yaingize kile nisemacho.
18 # Ay 13:3; 23:4; 37:19; 2:3; 9:21 Sasa kwamba nimekwisha kutayarisha mambo yangu,
ninajua mimi nitahesabiwa kuwa na haki.
19 # Isa 50:8; Rum 8:33; Ay 3:13; 40:4; 9:15 Je, kuna yeyote anayeweza kuleta mashtaka dhidi yangu?
Kama ndivyo, nitanyamaza kimya na nife.
20“Ee Mungu, unijalie tu mimi haya mambo mawili,
nami sitajificha uso wako:
21 # Za 39:10; Ebr 10:31; Kut 9:3; Ay 6:4 Ondoa mkono wako uwe mbali nami,
nawe uache kuniogofya kwa hofu zako kuu.
22 # Ay 9:35; 14:15 Niite kwenye shauri nami nitajibu,
au niache niseme, nawe upate kujibu.
23 # 1Sam 26:18; Ay 7:21; 9:21; 14:17; 33:9 Ni makosa na dhambi ngapi nilizotenda?
Nionyeshe kosa langu na dhambi yangu.
24 # Isa 8:17; Za 88:14-15; Yer 30:14 Kwa nini kuuficha uso wako
na kunihesabu mimi kuwa adui yako?
25 # Law 26:36; Isa 43:17; Hos 13:3 Je, utaliadhibu jani lipeperushwalo na upepo?
Je, utayasaka makapi makavu?
26 # Ay 21:23; Za 25:7 Kwa kuwa unaandika mambo machungu dhidi yangu
na kunifanya nizirithi dhambi za ujana wangu.
27 # Mwa 40:15; Mdo 16:24 Umeifunga miguu yangu kwenye pingu.
Unazichunga kwa makini njia zangu zote
kwa kutia alama kwenye nyayo za miguu yangu.
28 # Hos 5:12; Yak 5:2 “Hivyo mwanadamu huangamia kama kitu kilichooza,
kama vazi lililoliwa na nondo.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014