Ayubu 29
NEN

Ayubu 29

29
Ayubu Anamaliza Utetezi Wake
1 # Za 18:28; Ay 13:12 Ayubu akaendelea na hoja yake, akasema:
2 # Yer 1:12; 44:27 “Tazama jinsi ninavyoitamani miezi iliyopita,
zile siku ambazo Mungu alikuwa akinilinda,
3 # Ay 11:17; 12:25 wakati taa yake iliniangazia kichwani changu,
na kwa mwanga wake Mungu nikapita katikati ya giza!
4 # Za 25:14; Mit 3:32 Natamani siku zile nilizokuwa katika ustawi wangu,
wakati urafiki wa Mungu wa ndani ulipoibariki nyumba yangu,
5 # Za 127:3-5; 128:3; Rum 4:1 wakati Mwenyezi alikuwa pamoja nami,
nao watoto wangu walikuwa wamenizunguka,
6 # Ay 20:17; Za 81:16; Mwa 49:20; Kum 32:13 wakati njia yangu ilikuwa imenyweshewa siagi,
nao mwamba ukanimiminia vijito vya mafuta ya zeituni.
7 # Ay 5:4; 31:21; Yer 20:2; 38:7 “Wakati nilipokwenda kwenye lango la mji
na kuketi katika kiwanja,
8 # 1Tim 5:1; Law 19:32 vijana waliniona wakakaa kando,
nao wazee walioketi wakasimama;
9 # Amu 16:19; Mit 30:32 wakuu wakaacha kuzungumza
na kuziba vinywa vyao kwa mikono yao;
10 # Za 137:6 wenye vyeo wakanyamazishwa,
nazo ndimi zao zikagandamana na makaakaa ya vinywa vyao.
11 # Ay 4:4; Ebr 11:4 Yeyote aliyenisikia alinena mema juu yangu,
nao walioniona walinisifu,
12 # Kum 24:17; Ay 31:17-21; Za 72:12; Mit 21:13 kwa sababu nilimwokoa maskini aliyeomba msaada,
naye yatima aliyekuwa hana wa kumsaidia.
13 # Ay 31:20; 22:9; Kum 10:18 Mtu aliyekuwa karibu kufa alinibariki,
nami niliufanya moyo wa mjane kuimba.
14 # 2Sam 8:15; Rum 13:14; Efe 6:14 Niliivaa haki kama vazi langu;
uadilifu ulikuwa joho langu na kilemba changu.
15 # Hes 10:31 Nilikuwa macho ya kipofu
na miguu kwa kiwete.
16 # Ay 24:4; Mit 29:7 Nilikuwa baba kwa mhitaji;
nilimtetea mgeni.
17 # Ay 24:9; 4:10, 11; Za 3:7 Niliyavunja meno makali ya waovu,
na kuwapokonya wahanga kwenye meno yao.
18 # Za 62:2; Mit 3:1-2 “Nikafikiri, ‘Nitafia katika nyumba yangu mwenyewe,
nazo siku zangu zitakuwa nyingi kama chembechembe za mchanga.
19 # Hes 24:6; Yer 17:8 Mizizi yangu itafika mpaka kwenye maji,
nao umande utakaa juu ya matawi yangu usiku kucha.
20 # Za 18:34; Isa 38:12; Mwa 49:24 Utukufu wangu utabakia kuwa mpya ndani yangu,
upinde wangu daima utaendelea kuwa mpya mkononi mwangu.’
21 # Ay 29:21 “Watu walinisikiliza kwa tumaini,
wakingojea ushauri wangu kwa utulivu.
22 # Kum 32:2 Baada ya mimi kuzungumza, hawakusema zaidi;
maneno yangu yaliingia masikioni mwao kwa makini.
23Waliningojea kama manyunyu ya mvua
na kuyapokea maneno yangu
kama ardhi inyonyavyo mvua ya vuli.
24Walipokata tamaa niliwaonyesha uso wa furaha;
nuru ya uso wangu ilikuwa ya thamani kwao.
25 # Ay 31:31; 4:4 Niliwachagulia njia na kukaa kama mkuu wao;
niliishi kama mfalme katikati ya majeshi yake;
nikawa kama yeye anayewafariji waombolezaji.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014