37
1 #
Za 38:10; Isa 15:5; Yer 4:19; Hab 3:16 “Kwa hili moyo wangu unatetemeka,
nao unaruka kutoka mahali pake.
2 #
Za 18:13; 29:3-9 Sikiliza! Sikiliza ngurumo ya sauti yake,
sauti ya ngurumo itokayo kinywani mwake.
3 #
2Sam 22:13; Za 18:14; Ay 36:32; Mt 24:27; Lk 17:24 Huuachilia umeme wake wa radi chini ya mbingu yote
na kuupeleka hata miisho ya dunia.
4 #
1Sam 2:10; Kut 20:19 Baada ya hayo huja sauti ya ngurumo yake;
Mungu hunguruma kwa sauti yake ya fahari.
Wakati sauti yake ingurumapo tena,
huuachilia umeme wake wa radi.
5 #
Ay 11:7-9
Sauti ya Mungu hunguruma kwa namna za ajabu;
yeye hutenda mambo makuu kupita ufahamu wetu.
6 #
Kum 28:12; Ay 38:22; Mwa 7:4; Ay 36:27 Huiambia theluji, ‘Anguka juu ya dunia,’
nayo manyunyu ya mvua, ‘Uwe mvua ya nguvu.’
7 #
Ay 12:14; Za 111:2; 109:27; 104:19-23 Ili wanadamu wote aliowaumba wapate kujua kazi zake,
yeye humzuilia kila mtu shughuli zake.
8 #
Ay 28:26; 38:40; Za 104:22 Wanyama hujificha;
hubakia kwenye mapango yao.
9 #
Za 50:3; 147:17 Dhoruba hutoka katika chumba chake,
baridi hutoka katika upepo uendao kasi.
10 #
Ay 38:29-30; Za 147:17 Pumzi ya Mungu hutoa barafu,
eneo kubwa la maji huganda.
11 #
Ay 26:8; 36:30; 28:26 Huyasheheneza mawingu kwa maji,
naye husambaza umeme wake wa radi kupitia hayo.
12 #
Za 147:16; 148:8; Ay 37:3 Nayo mawingu huzungukazunguka pande zote kwa amri yake,
juu ya uso wa dunia yote,
kufanya lolote ayaamuruyo.
13 #
Kut 9:22-23; 1Sam 12:17; Kut 9:18; 1Fal 18:45 Huleta mawingu ili kuadhibu wanadamu,
au kuinyeshea dunia yake na kuonyesha upendo wake.
14 #
Ay 32:10; 5:9 “Ayubu, sikiliza hili;
nyamaza na uyafikiri maajabu ya Mungu.
15 #
Ay 36:30, 32 Je, unajua jinsi Mungu anavyoyaongoza mawingu,
na kufanya umeme wake wa radi utoe mwanga?
16 #
Ay 36:29; 5:9; 36:4 Je, wajua jinsi mawingu yanavyokaa yakiwa yametulia,
hayo maajabu yake yeye aliye mkamilifu katika maarifa?
17 #
Mdo 27:13
Wewe unayeshindwa na joto katika nguo zako
wakati nchi imenyamazishwa kimya bila upepo wa kusini,
18 #
Mwa 1:1, 8; Ay 22:14; Kum 28:23; Za 104:2 je, waweza kuungana naye katika kuzitandaza anga,
zilizo ngumu kama kioo cha shaba ya kuyeyushwa?
19 #
Rum 8:26; Ay 13:18; 9:3 “Tuambieni yatupasayo kumwambia;
hatuwezi kutayarisha shauri letu kwa sababu ya ujinga wetu.
20Je, aambiwe kwamba nataka kuongea?
Je, yuko mtu ambaye angeomba kumezwa?
21 #
Amu 5:31; Mdo 22:1; 26:13 Basi hakuna awezaye kulitazama jua,
jinsi linavyongʼaa angani,
upepo ukishafagia mawingu.
22 #
Za 19:5; Kut 24:17 Kutoka kaskazini yeye huja na fahari kuu;
Mungu huja katika utukufu wa kutisha.
23 #
Ay 5:9; Rum 11:33; Ay 8:3; Yer 25:5; Mao 3:33 Yeye Mwenyezi hatuwezi kumfikia, naye ametukuzwa katika uweza;
katika hukumu zake na haki yake kuu, hataonea.
24 #
Mik 6:8; Mt 10:28; 11:25; Efe 5:15 Kwa hiyo, wanadamu mheshimuni,
kwa kuwa yeye hamstahi yeyote anayejidhania kuwa ana hekima.”