3
# 3 Sura hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22. 1#Ay 19:21; Za 88:7; Yer 15:17-18Mimi ndiye mtu aliyeona mateso
kwa fimbo ya ghadhabu yake.
2 #
Ay 19:8; Za 82:5; Yer 4:23 Amenifukuzia mbali na kunifanya nitembee
gizani wala si katika nuru;
3 #
Isa 5:25; Za 38:2 hakika, amegeuza mkono wake dhidi yangu
tena na tena, mchana kutwa.
4 #
Za 51:8; Isa 38:13; Yer 50:17; Ay 30:30; Mao 4:8 Amefanya ngozi yangu na nyama yangu kuchakaa
na ameivunja mifupa yangu.
5 #
Yer 23:15
Amenizingira na kunizunguka
kwa uchungu na taabu.
6 #
Isa 59:10; Za 143:3; 88:5-6 Amenifanya niishi gizani
kama wale waliokufa.
7 #
Ay 3:23; Yer 40:4 Amenizungushia ukuta ili nisiweze kutoroka,
amenifunga kwa minyororo mizito.
8 #
Kum 1:45; Ay 30:20; Za 22:2; 5:2 Hata ninapoita au kulia ili kuomba msaada,
anakataa kupokea maombi yangu.
9 #
Ay 9:24; Hos 2:6; Isa 63:17 Ameizuia njia yangu kwa mapande ya mawe,
amepotosha njia zangu.
10 #
Ay 10:16; Hos 13:8; Amo 5:18-19 Kama dubu aviziaye,
kama simba mafichoni,
11ameniburuta kutoka njia,
akanirarua na kuniacha bila msaada.
12 #
Mao 2:4; Ay 16:12; Za 38:2; 34:2 Amevuta upinde wake
na kunifanya mimi niwe lengo
kwa ajili ya mishale yake.
13Alinichoma moyo wangu kwa mishale
iliyotoka kwenye podo lake.
14 #
Mwa 38:23; Za 22:6-7; Ay 30:9; Neh 4:2-4; Mt 27:29-31; Yer 20:7 Nimekuwa kichekesho kwa watu wangu wote,
wananidhihaki kwa wimbo mchana kutwa.
15 #
Yer 9:15
Amenijaza kwa majani machungu
na kunishibisha kwa nyongo.
16 #
Mit 20:17
Amevunja meno yangu kwa changarawe,
amenikanyagia mavumbini.
17Amani yangu imeondolewa,
nimesahau kufanikiwa ni nini.
18 #
Ay 17:15; Za 31:22 Kwa hiyo nasema, “Fahari yangu imeondoka
na yale yote niliyokuwa nimetarajia kutoka kwa Bwana.”
19Nayakumbuka mateso yangu na kutangatanga kwangu,
uchungu na nyongo.
20 #
Za 42:5; 43:5 Ninayakumbuka vyema,
nayo nafsi yangu imezimia ndani yangu.
21Hata hivyo najikumbusha neno hili
na kwa hiyo ninalo tumaini.
22 #
Za 130:7; Mt 3:6; Neh 9:31; Ay 34:15; Za 130:1; Hos 11:9; Za 78:38; 57:10; Mal 3:6 Kwa sababu ya upendo mkuu wa Bwana, hatuangamii,
kwa kuwa huruma zake hazikomi kamwe.
23 #
Kut 34:6; Isa 33:2; Ebr 10:23 Ni mpya kila asubuhi,
uaminifu wako ni mkuu.
24 #
Za 16:5
Nimeiambia nafsi yangu, “Bwana ni fungu langu,
kwa hiyo nitamngojea.”
25 #
Za 33:18; Isa 25:9; 30:18; Za 130:6 Bwana ni mwema kwa wale ambao tumaini lao ni kwake,
kwa yule ambaye humtafuta;
26 #
Za 37:7
ni vyema kungojea kwa utulivu
kwa ajili ya wokovu wa Bwana.
27 #
Za 90:12
Ni vyema mtu kuchukua nira
bado angali kijana.
28 #
Yer 15:17
Na akae peke yake awe kimya,
kwa maana Bwana ameiweka juu yake.
29 #
Yer 31:17; Ay 2:8; 42:6 Na azike uso wake mavumbini
bado panawezekana kuwa na matumaini.
30 #
Ay 16:10; Isa 50:6; Mik 5:1; Mt 5:39 Na atoe shavu lake kwa yule ampigaye,
na ajazwe na aibu.
31 #
Za 94:14; Isa 54:7 Kwa kuwa watu hawakatiliwi mbali
na Bwana milele.
32 #
Za 106:43-45; Nah 1:12; Hos 11:8 Ingawa huleta huzuni, ataonyesha huruma,
kwa kuwa upendo wake usiokoma ni mkuu.
33 #
Ay 37:23; Ebr 12:10; Yer 31:20; Eze 18:23 Kwa maana hapendi kuwaletea mateso
au huzuni watoto wa wanadamu.
34Kuwaponda chini ya nyayo
wafungwa wote katika nchi,
35 #
Mwa 14:18-22
Kumnyima mtu haki zake
mbele za Aliye Juu Sana,
36 #
Za 140:12; Mit 17:15; Hab 1:13; Yer 22:3 kumnyima mtu haki:
Je, Bwana asione mambo kama haya?
37 #
Mit 19:21; Za 33:9-11; Mit 21:30 Nani awezaye kusema nalo likatendeka
kama Bwana hajaamuru?
38 #
Ay 2:10; Isa 45:7; Yer 32:42 Je, si ni kwenye kinywa cha Aliye Juu Sana
ndiko yatokako maafa na mambo mema?
39 #
Yer 30:15; Mik 7:9 Mwanadamu yeyote aliye hai aweza kulalamika
wakati anapoadhibiwa kwa ajili ya dhambi zake?
40 #
2Kor 13:5; Za 119:59; 139:23-24 Tuzichunguze njia zetu na kuzijaribu,
na tumrudie Bwana Mungu.
41 #
Dan 9:5; Yer 14:20; 2Fal 24:4; Yer 5:7-9; Za 86:4 Tuinue mioyo yetu pamoja na mikono yetu
kwa Mungu mbinguni, na tuseme:
42 #
Dan 9:5
“Tumetenda dhambi na kuasi
nawe hujasamehe.
43 #
Mao 2:2, 17, 21; Za 35:6 “Umejifunika mwenyewe kwa hasira na kutufuatilia;
umetuchinja bila huruma.
44 #
Mao 2:1; Zek 7:13; Za 97:2; Isa 58:4 Unajifunika mwenyewe kwa wingu,
ili pasiwe na ombi
litakaloweza kupenya.
45 #
1Kor 4:13
Umetufanya takataka na uchafu
miongoni mwa mataifa.
46 #
Za 22:13; Mao 2:16 “Adui zetu wote wamefumbua vinywa vyao
wazi dhidi yetu.
47 #
Yer 48:43; Isa 24:17-18; 51:19 Tumeteseka kwa hofu kuu na shida ya ghafula,
uharibifu na maangamizi.”
48 #
Yer 9:1; Mao 2:18 Vijito vya machozi vinatiririka kutoka machoni mwangu,
kwa sababu watu wangu wameangamizwa.
49Macho yangu yatatiririka machozi bila kukoma,
bila kupata nafuu,
50 #
Za 14:2; 80:14; Isa 63:15 hadi Bwana atazame chini
kutoka mbinguni na kuona.
51Lile ninaloliona huniletea huzuni nafsini
kwa sababu ya wanawake wote wa mji wangu.
52 #
Za 35:7; 69:4 Wale waliokuwa adui zangu bila sababu
wameniwinda kama ndege.
53 #
Yer 38:6; 37:16; Dan 6:17 Walijaribu kukomesha maisha yangu ndani ya shimo
na kunitupia mawe;
54 #
Za 69:2; Yon 2:3-5; Eze 37:11; Za 88:5 maji yalifunika juu ya kichwa changu,
nami nikafikiri nilikuwa karibu
kukatiliwa mbali.
55 #
Za 130:1; 2Nya 33:12; Yon 2:2; Za 18:5, 6 Nililiitia jina lako, Ee Bwana,
kutoka vina vya shimo.
56 #
Rum 8:26; Za 116:1-2; 6:8 Ulisikia ombi langu: “Usikizibie masikio yako
kilio changu nikuombapo msaada.”
57 #
Isa 41:10; Yak 4:8; Za 46:1; 69:18; Isa 58:9 Ulikuja karibu nilipokuita,
nawe ukasema, “Usiogope.”
58 #
Yer 51:36; Za 34:22; Yer 50:34; 1Sam 25:39 Ee Bwana, ulichukua shauri langu,
ukaukomboa uhai wangu.
59 #
Yer 18:19; Za 35:23 Umeona, Ee Bwana, ubaya niliotendewa.
Tetea shauri langu!
60 #
Yer 11:20; 18:18 Umeona kina cha kisasi chao,
mashauri yao yote mabaya dhidi yangu.
61Ee Bwana, umesikia matukano yao,
mashauri yao yote mabaya dhidi yangu:
62 #
Eze 36:3
kile adui zangu wanachonongʼona na kunungʼunikia
dhidi yangu mchana kutwa.
63 #
Ay 30:9; Za 139:2 Watazame! Wakiwa wameketi au wamesimama,
wananidhihaki katika nyimbo zao.
64 #
Za 28:4; Yer 51:6; 2Tim 4:14; Yer 11:20; Ufu 6:10 Uwalipe kile wanachostahili, Ee Bwana,
kwa yale ambayo mikono yao imetenda.
65 #
Kut 14:8; Kum 2:30; Isa 6:10; Za 8:3 Weka pazia juu ya mioyo yao,
laana yako na iwe juu yao!
66Wafuatilie katika hasira na uwaangamize
kutoka chini ya mbingu za Bwana.