Mika 1
NEN

Mika 1

1
1 # Yer 26:18; 2Pet 1:21; 1Nya 3:12-13; Hos 1:1; Isa 1:1 Neno la Bwana lilimjia Mika, Mmoreshethi, wakati wa utawala wa Yothamu, Ahazi na Hezekia, wafalme wa Yuda; ufunuo aliouona kuhusu Samaria na Yerusalemu.
2 # Kum 4:26; 32:1; Yer 6:19; Mwa 31:50; Za 11:4; Isa 1:2 Sikieni, enyi mataifa, enyi nyote,
sikilizeni, ee dunia na wote mliomo ndani yake,
ili Bwana Mwenyezi ashuhudie dhidi yenu,
Bwana kutoka Hekalu lake takatifu.
Hukumu Dhidi Ya Samaria Na Yerusalemu
3 # Isa 18:4; 64:1; 26:21; Eze 3:12; Ebr 12:18, 19; Amo 4:13 Tazama! Bwana anakuja kutoka mahali pake;
anashuka na kukanyaga
mahali palipoinuka juu pa dunia.
4 # Za 46:2-6; Hes 16:31; Nah 1:5 Milima inayeyuka chini yake
na mabonde yanagawanyika
kama nta mbele ya moto,
kama maji yatiririkayo kasi
kwenye mteremko.
5 # Amo 8:14; Hos 5:5; Yer 2:18-19 Yote haya ni kwa sababu ya kosa la Yakobo,
ni kwa sababu ya dhambi za nyumba ya Israeli.
Kosa la Yakobo ni lipi?
Je, sio Samaria?
Je, mahali pa juu pa Yuda pa kuabudia miungu ni nini?
Je, sio Yerusalemu?
6 # Kum 20:6; Amo 5:11 “Kwa hiyo nitaufanya Samaria kuwa lundo la kokoto,
mahali pa kuotesha mizabibu.
Nitayamwaga mawe yake katika bonde
na kuacha wazi misingi yake.
7 # Eze 6:6; Kut 32:20; Kum 9:21; 23:17-18 Sanamu zake zote
zitavunjwa vipande vipande;
zawadi zake zote za Hekalu
zitachomwa kwa moto;
nitaharibu vinyago vyake vyote.
Kwa kuwa alikusanya zawadi zake
kutokana na ujira wa kahaba,
nazo zitatumika tena
kulipa mishahara ya kahaba.”
Kulia Na Kuomboleza
8 # Isa 15:3; 20:2 Kwa ajili ya hili nitalia na kuomboleza;
nitatembea bila viatu na tena uchi.
Nitabweka kama mbweha
na kuomboleza kama bundi.
9 # Yer 46:11; 10:19; 2Fal 18:13; Isa 3:26 Kwa sababu jeraha lake halitibiki;
limekuja Yuda.
Limefika hasa kwenye lango la watu wangu,
hata Yerusalemu kwenyewe.
10Usiliseme hili huko Gathi;
usilie hata kidogo.
Huko Beth-le-Afra
gaagaa mavumbini.
11 # Eze 23:29 Piteni mkiwa uchi na wenye aibu,
ninyi mkaao Shafiri.
Wale waishio Saanani
hawatatoka nje.
Beth-Eseli iko katika maombolezo;
kinga yake imeondolewa kwako.
12 # Yer 14:19; 40:2 Wale waishio Marothi wanagaagaa kwa maumivu
wakingoja msaada,
kwa sababu maangamizi yamekuja
kutoka kwa Bwana,
hata katika lango la Yerusalemu.
13 # Yos 10:3; Za 9:14 Enyi mkaao Lakishi,
fungeni farasi kwenye magari ya vita.
Mlikuwa chanzo cha dhambi
kwa Binti Sayuni,
kwa kuwa makosa ya Israeli
yalikutwa kwako.
14 # 2Fal 16:8; Yos 15:44; Yer 15:18 Kwa hiyo utaipa Moresheth-Gathi
zawadi za kuagana.
Mji wa Akzibu utaonyesha wazi udanganyifu
kwa wafalme wa Israeli.
15 # Yos 15:44; 12:15 Nitawaleteeni atakayewashinda
ninyi mnaoishi Maresha.
Yeye aliye utukufu wa Israeli
atakuja Adulamu.
16 # Law 13:40; Ay 1:20; 2Fal 18:13; Amo 5:27; Kum 4:27 Nyoeni nywele zenu katika kuomboleza
kwa ajili ya watoto wenu mnaowafurahia;
jifanyieni upara kama tai,
kwa kuwa watawaacha
na kwenda uhamishoni.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014