Mika 5
NEN

Mika 5

5
Mtawala Aliyeahidiwa Kutoka Bethlehemu
1 # Ay 16:10; Mt 27:30; Mao 3:30 Panga majeshi yako, ee mji wa majeshi,
kwa kuwa kuzingirwa kumepangwa dhidi yetu.
Watampiga mtawala wa Israeli
shavuni kwa fimbo.
2 # Yn 7:42; Mwa 35:19; 48:7; 1Sam 13:14; Hes 24:19; 2Sam 6:21; 2Nya 7:18; Za 90:2; 132:6; 102:25; Isa 9:6; Mit 8:22; Yn 1:1; Mt 2:6 “Lakini wewe, Bethlehemu Efrathi,
ingawa u mdogo miongoni mwa koo za Yuda,
kutoka kwako atatokea kwa ajili yangu
yeye atakayekuwa mtawala katika Israeli,
ambaye asili yake ni kutoka zamani,
kutoka milele.”
3 # Yer 7:29 Kwa hiyo Israeli utaachwa mpaka wakati
mwanamke aliye na utungu atakapozaa
na ndugu zake wengine warudi
kujiunga na Waisraeli.
4 # Isa 40:11; 49:9; 52:13; Za 72:8; Zek 9:10; Mik 7:14; Eze 34:11-15; Lk 1:32 Atasimama na kulichunga kundi lake
katika nguvu ya Bwana,
katika utukufu wa jina la Bwana Mungu wake.
Nao wataishi kwa usalama, kwa kuwa wakati huo
ukuu wake utaenea hadi miisho ya dunia.
5 # Isa 8:7; 9:6; 10:24-27; Lk 2:14; Efe 2:14; Kol 1:19-20 Naye atakuwa amani yao.
Ukombozi Na Uharibifu
Wakati Mwashuru atakapovamia nchi yetu
na kupita katika ngome zetu,
tutawainua wachungaji saba dhidi yake,
hata viongozi wanane wa watu.
6 # Mwa 10:8; Sef 2:13; Lk 1:71; Nah 2:11-13 Wataitawala nchi ya Ashuru kwa upanga,
nchi ya Nimrodi kwa upanga.
Atatuokoa kutoka kwa Mwashuru
atakapoivamia nchi yetu
na kuingia katika mipaka yetu.
7 # Amo 5:15; Mik 2:12; Isa 44:4; Za 110:3; 133:3 Mabaki ya Yakobo yatakuwa
katikati ya mataifa mengi
kama umande kutoka kwa Bwana,
kama manyunyu juu ya majani,
ambayo hayamngoji mtu
wala kukawia kwa mwanadamu.
8 # Mwa 49:9; Mik 4:13; Zek 10:5; Isa 5:29; Za 50:22; Hos 5:14 Mabaki ya Yakobo yatakuwa miongoni mwa mataifa,
katikati ya mataifa mengi,
kama simba miongoni mwa wanyama wa msituni,
kama mwana simba miongoni
mwa makundi ya kondoo,
ambaye anaumiza vibaya na kuwararua
kila anapopita katikati yao,
wala hakuna awezaye kuokoa.
9 # Za 10:12 Mkono wako utainuliwa juu kwa ushindi juu ya watesi wako,
nao adui zako wote wataangamizwa.
10 # Kut 15:4, 19; Hos 14:3; Hag 2:22; Zek 9:10 “Katika siku ile,” asema Bwana,
“nitaangamiza farasi zenu katikati yenu
na kubomoa magari yenu ya vita.
11 # Kum 29:23; Isa 6:11; Mao 2:2; Hos 10:14; Amo 5:9 Nitaiangamiza miji ya nchi yenu
na kuziangusha chini ngome zenu zote.
12 # Kum 18:10-12; Isa 8:19; 2:9 Nitaangamiza uchawi wenu
na hamtapiga tena ramli.
13 # Nah 1:14; Hos 2:10; Isa 2:8; 2:18; Eze 6:9; Zek 13:2 Nitaangamiza vinyago vyenu vya kuchonga
na mawe yenu ya ibada yatoke katikati yenu;
hamtasujudia tena
kazi ya mikono yenu.
14 # Kut 34:13; Amu 3:7; 2Fal 17:10 Nitangʼoa nguzo za Ashera katikati yenu
na kubomoa miji yenu.
15 # Isa 65:12 Nitalipiza kisasi kwa hasira na ghadhabu
juu ya mataifa ambayo hayajanitii.”

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014