1
Utangulizi: Kusudi Na Kiini
1 #
1Fal 4:29-34
Mithali za Solomoni mwana wa Daudi, mfalme wa Israeli:
2Kwa kupata hekima na nidhamu;
kwa kufahamu maneno ya busara;
3 #
Mit 2:1; 2:1, 9 kwa kujipatia nidhamu na busara,
kufanya lililo sawa, haki na bila kupendelea;
4 #
Mit 8:5, 12; 2:10-11 huwapa busara wajinga,
maarifa na akili kwa vijana;
5 #
Mit 9:9
wenye hekima na wasikilize nao waongeze elimu yao,
wenye kupambanua na wapate mwongozo;
6 #
Za 78:2; Mt 13:10-17; Hes 12:8; Amu 14:12 kwa kufahamu mithali na mifano,
misemo na vitendawili vya wenye hekima.
7 #
Kut 20:20; Ay 28:28 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha maarifa,
lakini wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Onyo Dhidi Ya Ushawishi Wa Marafiki Waovu
8 #
Mit 6:20; 22:17; Kum 21:18 Mwanangu, sikiliza mwongozo wa baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
9 #
Mit 3:21-22; 4:1-9 Hayo yatakuwa taji la maua la neema kichwani pako,
na mkufu wa kuipamba shingo yako.
10 #
Mwa 39:7; Ay 24:15; Kum 13:8; Rum 16:18 Mwanangu, kama wenye dhambi wakikushawishi,
usikubaliane nao.
11 #
Mit 12:6; Yer 5:26; Mik 7:2 Kama wakisema, “Twende tufuatane;
tukamvizie mtu na kumwaga damu,
njoo tukavizie nafsi isiyo na hatia;
12 #
Ay 33:18; Mwa 38:25; Za 40:3 tuwameze wakiwa hai kama kaburi,#1:12 Kaburi hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
wakiwa wazima kama wale wanaotumbukia shimoni.
13Tutapata aina zote za vitu vya thamani
na kujaza nyumba zetu kwa nyara.
14 #
Mit 1:19
Njoo ushirikiane nasi,
vitu vyote tutakavyopata tutagawana.”
15 #
Za 119:101; Mwa 49:6; Mit 4:14 Mwanangu, usiandamane nao.
Usiweke mguu wako katika njia zao,
16 #
Mit 6:18; Isa 59:7 kwa kuwa miguu yao hukimbilia kwenye dhambi,
ni wepesi kumwaga damu.
17Tazama ni jinsi gani ilivyo kazi bure kutandaza wavu
wakati ndege wote wanakuona!
18 #
Za 71:10
Watu hawa huvizia kumwaga damu yao wenyewe;
hujivizia tu wenyewe!
19 #
Mit 11:19; 15:27; 2Fal 5:20-27 Huu ndio mwisho wa wote ambao wanajipatia mali kwa hila;
huuondoa uhai wa wale wenye mali.
Onyo Dhidi Ya Kukataa Hekima
20 #
Ay 28:12; Mt 7:10-13; 9:1-3, 13-15 Hekima huita kwa sauti kuu barabarani,
hupaza sauti yake kwenye viwanja vikubwa;
21kwenye makutano ya barabara za mji
zenye makelele mengi hupaza sauti,
kwenye malango ya mji hutoa hotuba yake:
22 #
Mit 6:32; 7:7; 8:5; 9:4, 16; Za 50:17 “Enyi wajinga, mtangʼangʼania ujinga wenu hadi lini?
Mpaka lini wenye mizaha watafurahia mizaha,
na wapumbavu kuchukia maarifa?
23 #
Yoe 2:28; Yn 7:37 Kama mngekuwa mmeitikia karipio langu,
ningekuwa nimemimina roho yangu kwenu
na kuwafahamisha maneno yangu.
24 #
Isa 65:12; Zek 7:11 Lakini kwa kuwa mlinikataa nilipowaita
na hakuna yeyote aliyekubali
niliponyoosha mkono wangu,
25 #
Lk 7:30
kwa kuwa mliyapuuza mashauri yangu yote
na hamkukubali karipio langu,
26 #
Za 2:4; Kum 28:63; Mit 10:24 mimi nami nitawacheka katika maafa yenu,
nitawadhihaki wakati janga litawapata:
27 #
Za 18:18; Mit 5:12-14 wakati janga litawapata kama tufani,
wakati maafa yatawazoa kama upepo wa kisulisuli,
wakati dhiki na taabu zitawalemea.
28 #
Isa 1:15; Mik 3:4; Eze 8:18; Hos 5:6 “Ndipo watakaponiita lakini sitawajibu;
watanitafuta lakini hawatanipata.
29 #
Ay 21:14; Isa 27:11; Mdo 7:51 Kwa kuwa walichukia maarifa,
wala hawakuchagua kumcha Bwana,
30 #
Ay 21:14; Za 81:11 kwa kuwa hawakukubali mashauri yangu,
na kukataa maonyo yangu,
31 #
2Nya 36:16; Yer 14:16 watakula matunda ya njia zao,
na watashibishwa matunda ya hila zao.
32 #
Isa 66:4; Yer 2:19 Kwa kuwa ukaidi wa wajinga utawaua,
nako kuridhika kwa wajinga kutawaangamiza.
33 #
Hes 24:21; Za 25:12; 112:8 Lakini yeyote anisikilizaye ataishi kwa usalama,
atatulia, bila kuwa na hofu ya madhara.”