11
1 #
Law 19:36; Ay 6:2; Mit 16:11; Eze 45:10 Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,
bali vipimo sahihi ni furaha yake.
2 #
Dan 4:30; Mit 16:18; 18:12 Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,
bali unyenyekevu huja na hekima.
3 #
Mit 13:6
Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,
bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
4 #
Ay 20:20; Eze 7:19; Sef 1:18 Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu,
bali haki huokoa kutoka mautini.
5 #
1Fal 8:36; Mit 5:21-23; 13:6; 21:7 Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka,
bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
6 #
Es 7:9; 1Tim 4:8; Mhu 10:8 Haki ya wanyofu huwaokoa,
bali wasio waaminifu hunaswa na tamaa mbaya.
7 #
Ay 8:13; Mit 10:28 Wakati mtu mwovu anapokufa, matumaini yake hutoweka;
yote aliyoyatazamia kutokana na nguvu zake huwa si kitu.
8 #
Mit 21:8
Mtu mwenye haki huokolewa kutoka taabu,
naye mtu mwovu huingia humo badala yake.
9 #
Mit 12:6; Yer 45:5; Ay 8:13 Kwa kinywa chake mtu asiyemwamini Mungu
humwangamiza jirani yake,
bali kwa maarifa mwenye haki huokolewa.
10 #
2Fal 11:20; Mit 28:12; Es 8:15 Wakati mwenye haki anapofanikiwa, mji hufurahi;
mwovu atowekapo, kuna kelele za furaha.
11 #
Mit 14:34; 29:8 Kutokana na baraka ya mtu mnyofu mji hukwezwa,
bali kwa kinywa cha mwovu mji huharibiwa.
12 #
Mit 14:21; Ay 6:24 Mtu asiye na akili humdharau jirani yake,
bali mtu mwenye ufahamu huuzuia ulimi wake.
13 #
Law 19:16; 1Tim 5:13; Mit 20:19; 10:14 Masengenyo husaliti tumaini,
bali mtu mwaminifu hutunza siri.
14 #
Mit 20:18; 24:6; 2Sam 15:34; 1Fal 12:1; Mit 20:18; 2Sam 15:34; Mit 15:22; 24:6; 1Fal 12:1 Pasipo ushauri wa hekima taifa huanguka,
bali washauri wengi hufanya ushindi uwe wa hakika.
15 #
Mit 6:1; 17:18; 22:26-27 Yeye amdhaminiye mgeni hakika atateseka,
bali yeyote akataaye kuunga mkono dhamana ni salama.
16 #
Mit 31:31
Mwanamke mwenye moyo wa huruma hupata heshima,
bali wanaume wakorofi hupata mali tu.
17 #
Mt 25:34
Mwenye huruma hujinufaisha mwenyewe,
bali mkatili hujiletea taabu mwenyewe.
18 #
Hos 10:12; Kut 1:20; Ay 4:8 Mtu mwovu hupata ujira wa udanganyifu,
bali yeye apandaye haki huvuna tuzo ya uhakika.
19 #
Kum 30:15; Mit 10:2; 1Sam 2:6; Za 89:48; Mit 1:18-19; Mhu 7:2; Yer 43:1 Mtu mwenye haki kweli kweli hupata uzima,
bali yeye afuatiliaye ubaya huendea kifo chake.
20 #
1Nya 29:17; Za 52:7 Bwana huwachukia sana watu wenye moyo wa upotovu,
bali hupendezwa na wale ambao njia zao hazina lawama.
21 #
Mit 16:5; Za 112:2 Uwe na hakika na hili: Waovu hawataepuka kuadhibiwa,
bali wenye haki watakuwa huru.
22Kama pete ya dhahabu katika pua ya nguruwe
ndivyo alivyo mwanamke mzuri ambaye hana busara.
23 #
Rum 2:8, 9 Shauku ya mwenye haki huishia tu kwenye mema,
bali tumaini la mwovu huishia tu kwenye ghadhabu.
24 #
Za 112:9
Kuna mtu atoaye kwa ukarimu, hata hivyo hupata zaidi,
mwingine huzuia, lakini huwa maskini.
25 #
Mit 22:9; 2Kor 9:6-9; Mt 5:7 Mtu mkarimu atastawi;
yeye awaburudishaye wengine
ataburudishwa mwenyewe.
26 #
Amo 8:5; Ay 29:13 Watu humlaani mtu awanyimae watu nafaka,
bali baraka itamkalia kichwani kama taji
yeye aliye radhi kuiuza.
27 #
Es 7:10; Za 7:15-16 Yeye atafutaye mema hupata ukarimu,
bali ubaya huja kwake yeye autafutaye.
28 #
Yer 9:23; 17:8; Mk 10:25; Za 52:8 Yeyote ategemeaye utajiri wake ataanguka,
bali mwenye haki atastawi kama jani bichi.
29 #
Mhu 5:16; Mit 14:19 Yeye aletaye taabu kwa jamaa yake atarithi tu upepo,
naye mpumbavu atakuwa mtumishi wa wenye hekima.
30 #
Mwa 2:9; Yak 5:20 Tunda la mwenye haki ni mti wa uzima,
naye mwenye hekima huvuta roho za watu.
31 #
Yer 25:29; 49:12; 1Pet 4:18 Kama wenye haki watapokea ujira wao duniani,
si zaidi sana yule asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?