13
Mema Ya Muda Mfupi Na Yale Ya Kudumu
1 #
1Sam 2:25; Mit 10:1; 12:1; 15:5 Mwana mwenye hekima husikia mafundisho ya babaye,
bali mwenye dharau hasikilizi maonyo.
2 #
Mit 12:14
Kutoka tunda la midomo yake mtu hufurahia mambo mema,
bali wasio waaminifu wanatamani sana jeuri.
3 #
Za 12:2; Yak 3:2; Mit 10:6; Ay 1:22 Yeye alindaye midomo yake hulinda nafsi yake,
bali yeye asemaye kwa haraka ataangamia.
4 #
Mit 21:25-26
Mvivu hutamani sana na hapati kitu,
bali nafsi ya mwenye bidii
hutoshelezwa kikamilifu.
5 #
Kol 3:9; Rum 12:9 Mwenye haki huchukia uongo,
bali waovu huleta aibu na fedheha.
6 #
Mit 11:3-5; Yer 44:5 Haki humlinda mtu mwadilifu,
bali uovu humwangusha mwenye dhambi.
7 #
2Kor 6:10
Mtu mmoja hujifanya tajiri, kumbe hana chochote;
mwingine hujifanya maskini, kumbe ana utajiri mwingi.
8 #
Mit 15:16
Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake,
bali mtu maskini hasikii kitisho.
9 #
Ay 18:5; Mit 4:18-19 Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana,
bali taa ya mwovu itazimwa.
10 #
Amu 19:30; Mit 9:9 Kiburi huzalisha magomvi tu,
bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.
11 #
Mit 10:2; 9:9; 20:21 Fedha isiyo ya halali hupungua,
bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka.
12 #
Mit 10:11
Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua,
bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.
13 #
Hes 15:31; Kut 9:20; Mit 16:20; 2Nya 36:16 Yeye anayedharau mafundisho anajiletea maangamizi,
bali yeye anayeheshimu agizo hupewa tuzo.
14 #
Mit 10:11; 14:27 Mafundisho ya mwenye busara ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
15Ufahamu mzuri hupata upendeleo,
bali njia ya asiye mwaminifu ni ngumu.
16 #
Es 5:11; Mit 12:23 Kila mwenye busara hutenda kwa maarifa,
bali mpumbavu hudhihirisha upumbavu wake.
17 #
Mit 10:26; 25:13 Mjumbe mwovu huanguka kwenye taabu,
bali mjumbe mwaminifu huleta uponyaji.
18 #
Mit 15:31-32; Za 141:5 Yeye anayedharau maonyo hupata umaskini na aibu,
bali yeye anayekubali maonyo huheshimiwa.
19 #
Mit 10:11
Tarajio lililotimizwa ni tamu kwa nafsi,
bali wapumbavu huchukia sana kuacha ubaya.
20 #
2Nya 10:8
Yeye atembeaye na mwenye hekima atapata hekima,
bali rafiki wa mpumbavu hupata madhara.
21 #
Za 32:10; Mit 19:17; 11:12 Balaa humwandama mtenda dhambi,
bali mafanikio ni thawabu kwa mwenye haki.
22 #
Es 8:2; Mhu 2:26 Mtu mwema huwaachia wana wa wanawe urithi,
bali mali ya wenye dhambi imehifadhiwa
kwa ajili ya wenye haki.
23 #
Mit 12:11
Shamba la mtu maskini laweza kuzalisha chakula kingi,
bali dhuluma hukifutilia mbali.
24 #
Mit 29:15-17; Efe 6:4 Yeye aizuiaye fimbo yake hampendi mwanawe,
bali yeye ampendaye
huwa mwangalifu kumwadibisha.
25 #
Za 34:10; Mit 10:3 Mwenye haki hula mpaka akaridhisha moyo wake,
bali tumbo la mwovu hutaabika kwa njaa.