Mithali 14
NEN

Mithali 14

14
1 # Rut 3:11; Mit 24:3 Mwanamke mwenye hekima huijenga nyumba yake,
bali mpumbavu huibomoa nyumba yake
kwa mikono yake mwenyewe.
2 # Ay 12:4 Yeye ambaye njia zake ni nyofu humcha Bwana,
bali yeye ambaye njia zake zimepotoka humdharau Mungu.
3 # Mit 12:6; 10:13 Mazungumzo ya mpumbavu huleta fimbo mgongoni mwake,
bali mwenye hekima hulindwa na maneno ya midomo yake.
4 # Za 12:2; Mit 12:17 Pale ambapo hakuna mafahali, hori ni tupu,
bali kutokana na nguvu za fahali huja mavuno mengi.
5 # Kut 20:16; Za 12:2; Mit 6:19 Shahidi mwaminifu hadanganyi,
bali shahidi wa uongo humimina uongo.
6 # Mit 9:9; 17:24 Mwenye mzaha huitafuta hekima na haipati,
bali maarifa huja kwa urahisi kwa anayepambanua.
7Kaa mbali na mtu mpumbavu,
kwa maana hutapata maarifa katika midomo yake.
8 # Lk 12:20; 1Kor 3:19; Mit 15:28; 21:29 Hekima ya mwenye busara ni kufikiria njia zake,
bali upumbavu wa wapumbavu ni udanganyifu.
9 # Mit 1:22; 10:23 Wapumbavu hudhihaki kujirekebisha kutoka dhambi,
bali wema hupatikana miongoni mwa wanyofu.
10Kila moyo hujua uchungu wake wenyewe,
wala hakuna yeyote awezaye kushiriki furaha yake.
11 # Za 72:7; Ay 8:15; Mit 3:33 Nyumba ya mwovu itaangamizwa,
bali hema la mnyofu litastawi.
12 # Rum 6:21; Mit 12:15; 16:25 Iko njia ionekanayo kuwa sawa kwa mtu,
bali mwisho wake huelekeza mautini.
13 # Mhu 2:2; 7:3-6 Hata katika kicheko moyo waweza kuuma,
nayo furaha yaweza kuishia katika majonzi.
14 # 2Nya 15:7; Mit 12:14 Wasio na imani watapatilizwa kikamilifu kwa ajili ya njia zao,
naye mtu mwema atapewa thawabu kwa ajili ya njia yake.
15 # Mit 14:8 Mtu mjinga huamini kila kitu,
bali mwenye busara hufikiria hatua zake.
16 # Kut 20:20; Mit 22:3 Mtu mwenye hekima humcha Bwana na kuepuka mabaya,
bali mpumbavu hukasirika kwa hamaki na uzembe.
17 # Mit 28:25; 29:22 Mtu anayekasirika kwa haraka hufanya mambo ya upumbavu,
naye mtu wa hila huchukiwa.
18Mjinga hurithi upumbavu,
bali wenye busara huvikwa maarifa kichwani kama taji.
19 # Mit 11:29 Watu wabaya watasujudu mbele ya watu wema,
nao waovu kwenye malango ya wenye haki.
20 # Mit 19:4, 7 Maskini huepukwa hata na majirani zao,
bali matajiri wana marafiki wengi.
21 # Mit 11:12; 19:17; Za 41:1 Yeye anayemdharau jirani yake hutenda dhambi,
bali amebarikiwa yeye aliye na huruma kwa mhitaji.
22 # Mit 4:16-17 Je, wale wanaopanga ubaya hawapotoki?
Bali wale wanaopanga kilicho chema
hupata upendo na uaminifu.
23Kazi zote zinazofanywa kwa bidii huleta faida,
bali mazungumzo matupu huelekea umaskini tu.
24 # Mit 14:8 Utajiri wa wenye hekima ni taji yao,
bali upumbavu wa wapumbavu huzaa upumbavu.
25 # Mit 12:17 Shahidi wa kweli huokoa maisha,
bali shahidi wa uongo ni mdanganyifu.
26 # Mit 19:23; Isa 33:6 Yeye amchaye Bwana ana ngome salama,
na kwa watoto wake itakuwa kimbilio.
27 # Za 18:5; Mit 13:14 Kumcha Bwana ni chemchemi ya uzima,
ili kumwepusha mtu na mitego ya mauti.
28 # 2Sam 19:7 Wingi wa watu ni utukufu wa mfalme,
bali pasipo watu mkuu huangamia.
29 # Mhu 7:8-9; Mit 15:18; Yak 1:19 Mtu mwenye subira ana ufahamu mwingi,
bali anayekasirika haraka huonyesha upumbavu.
30 # Ay 5:2; Mdo 7:9; Mit 12:4 Moyo wenye amani huupa mwili uzima,
bali wivu huozesha mifupa.
31 # Ay 31:15-16; Mit 17:5 Yeye amwoneaye maskini huonyesha dharau kwa Muumba wao,
bali yeyote anayemhurumia mhitaji humheshimu Mungu.
32 # Za 34:21; Mit 6:15; Ay 13:15; 2Tim 4:18 Waovu huangamizwa kwa matendo yao maovu,
bali hata katika kifo wenye haki hupata kimbilio.
33 # Mit 2:6-10 Hekima hukaa katika moyo wa mwenye ufahamu
bali haijulikani miongoni mwa wapumbavu.
34 # Mit 11:11 Haki huinua taifa,
bali dhambi ni aibu kwa watu wote.
35 # Es 8:2; Mt 25:14-30 Mfalme hupendezwa na mtumishi mwenye hekima,
bali ghadhabu yake humwangukia
mtumishi mwenye kuaibisha.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014