2
Faida Za Hekima
1 #
Mit 1:8
Mwanangu, kama utayakubali maneno yangu
na kuyaweka akiba maagizo yangu ndani mwako,
2 #
Mit 22:17
kutega sikio lako kwenye hekima
na kuweka moyo wako katika ufahamu,
3 #
Yak 1:5
na kama ukiita busara
na kuita kwa sauti ufahamu,
4 #
Ay 3:21; Mt 13:44; 6:19-21 na kama utaitafuta kama fedha
na kuitafuta sana kama hazina iliyofichwa,
5 #
Kum 4:6
ndipo utakapoelewa kumcha Bwana
na kupata maarifa ya Mungu.
6 #
Ay 12:13; Lk 21:15; Yak 1:5 Kwa maana Bwana hutoa hekima,
na kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7 #
Mwa 6:9; 15:1; Mit 30:5-6; Za 84:11 Anahifadhi ushindi kwa ajili ya mwadilifu,
yeye ni ngao kwa wale wasio na lawama,
8 #
1Sam 2:9; Za 18:25 kwa kuwa hulinda mwenendo wa mwenye haki
na kuhifadhi njia ya waaminifu wake.
9 #
Kum 1:16
Ndipo utafahamu lipi lililo kweli na haki
na sawa: yaani kila njia nzuri.
10 #
Mit 14:33
Kwa maana hekima itaingia moyoni mwako,
nayo maarifa yataifurahisha nafsi yako.
11 #
Mit 4:6
Busara itakuhifadhi
na ufahamu utakulinda.
12 #
Mit 2:16; 3:13-18; 4:5 Hekima itakuokoa kutoka njia za waovu,
kutoka kwa watu ambao maneno yao yamepotoka,
13 #
Mit 4:19; Yn 3:19; Efe 4:18 wale waachao mapito yaliyonyooka
wakatembea katika njia za giza,
14 #
Mit 15:21; Yer 11:15 wale wapendao kutenda mabaya
na kufurahia upotovu wa ubaya,
15 #
Za 125:5; Mit 21:8 ambao mapito yao yamepotoka
na ambao ni wapotovu katika njia zao.
16 #
Mit 6:20-29; 7:5-27 Itakuokoa pia kutokana na mwanamke kahaba,
kutokana na mke aliyepotoka mwenye maneno
ya kushawishi kutenda ubaya,
17 #
Mal 2:14; Mwa 2:24 aliyemwacha mwenzi wa ujana wake
na kupuuza agano alilofanya mbele ya Mungu.
18 #
Mit 5:5; 7:27; 9:18 Kwa maana nyumba yake huelekea kwenye kifo
na mapito yake kwenye roho za waliokufa.
19 #
Mit 5:8; Mhu 7:26; Ebr 13:4 Hakuna yeyote aendaye kwake akarudi,
au kufikia mapito ya uzima.
20 #
Ebr 6:12
Hivyo utatembea katika njia za watu wema
na kushikamana na mapito ya wenye haki.
21 #
Za 37:29
Kwa maana wanyofu wataishi katika nchi,
nao wasio na lawama watabakia ndani yake.
22 #
Ay 18:17; Za 37:38; Kum 29:28 Bali waovu watakatiliwa mbali kutoka nchi,
nao wasio waaminifu watangʼolewa kutoka humo.