Mithali 3
NEN

Mithali 3

3
Faida Nyingine Za Hekima
1 # Kum 30:16; Za 44:17; Mit 4:5 Mwanangu, usisahau mafundisho yangu,
bali zitunze amri zangu moyoni mwako,
2 # Mit 9:6; 4:10 kwa kuwa zitakuongezea miaka mingi ya maisha yako
na kukuletea mafanikio.
3 # Kum 6:8; Mit 6:21; 2Kor 3:3 Usiache kamwe upendo na uaminifu vitengane nawe;
vifunge shingoni mwako,
viandike katika ubao wa moyo wako.
4 # 1Sam 2:26; Lk 2:52; Mdo 2:47 Ndipo utapata kibali na jina zuri
mbele za Mungu na mwanadamu.
5 # Za 4:5; Yer 9:23 Mtumaini Bwana kwa moyo wako wote
wala usizitegemee akili zako mwenyewe;
6 # 1Nya 28:9; Ay 33:11; Yer 42:3 katika njia zako zote mkiri yeye,
naye atayanyoosha mapito yako.
7 # Isa 5:21; Rum 12:16; Kum 4:6 Usiwe mwenye hekima machoni pako mwenyewe;
mche Bwana ukajiepushe na uovu.
8 # Za 38:3; Mit 4:22; Ay 21:24 Hii itakuletea afya mwilini mwako,
na mafuta kwenye mifupa yako.
9 # Kut 23:19; 26:1-15 Mheshimu Bwana kwa mali zako na
kwa malimbuko ya mazao yako yote;
10 # Kum 28:8; Za 144:13; Ay 22:21; Mal 3:10-12 ndipo ghala zako zitakapojaa hadi kufurika,
viriba vyako vitafurika kwa mvinyo mpya.
11 # Mit 1:8-9; Ay 5:17 Mwanangu, usiidharau adhabu ya Bwana
na usichukie kukaripiwa naye,
12 # Mit 13:24; Ufu 3:19; Ay 3:19; 5:17; Ebr 12:5-6 kwa sababu Bwana huwaadibisha wale awapendao,
kama vile baba afanyavyo
kwa mwana apendezwaye naye.
13 # Mit 8:34, 35 Heri mtu yule aonaye hekima,
mtu yule apataye ufahamu,
14 # Ay 28:15; Mit 16:16 kwa maana hekima ana faida kuliko fedha
na mapato yake ni bora kuliko ya dhahabu safi.
15 # Ay 28:17-19 Hekima ana thamani kuliko marijani;
hakuna chochote unachokitamani
kinachoweza kulinganishwa naye.
16 # 1Fal 3:13-14; Mit 8:18 Maisha marefu yako katika mkono wake wa kuume;
katika mkono wake wa kushoto
kuna utajiri na heshima.
17 # Mit 16:7; Mt 11:28-30 Njia zake zinapendeza,
mapito yake yote ni amani.
18 # Mwa 2:9; Ufu 2:7 Yeye ni mti wa uzima kwa wale wanaomkumbatia;
wale wamshikao watabarikiwa.
19 # Ay 28:25-27; Za 104:24; Mit 8:27-29 Kwa hekima Bwana aliiweka misingi ya dunia,
kwa ufahamu aliziweka mbingu mahali pake;
20 # Kum 33:28; Ay 36:28 kwa maarifa yake vilindi viligawanywa,
nayo mawingu yanadondosha umande.
21 # Mit 1:8-9; 6:20; 4:20-22 Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara,
usiache vitoke machoni pako;
22 # Kum 30:20; Mit 4:20-22 ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako
na pambo la neema shingoni mwako.
23Kisha utaenda katika njia yako salama,
wala mguu wako hautajikwaa;
24 # Law 26:6; Za 3:5; Ay 11:18; Yer 31:25 ulalapo, hautaogopa;
ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.
25 # Za 91:5; 112:7 Usiogope maafa ya ghafula
au maangamizi yanayowapata waovu,
26 # 1Sam 2:9 kwa kuwa Bwana atakuwa tumaini lako
na kuepusha mguu wako kunaswa katika mtego.
27 # Rum 13:7; Gal 6:10 Usizuie wema kwa wale wanaostahili
ikiwa katika uwezo wako kutenda.
28 # Law 19:13; Lk 10:25-37; Kum 24:15 Usimwambie jirani yako,
“Njoo baadaye, nitakupa kesho”:
wakati wewe unacho kitu kile karibu nawe.
29 # Zek 8:17 Usifanye hila ya kumdhuru jirani yako,
ambaye anaishi karibu na wewe akikuamini.
30 # Rum 12:18 Usimshtaki mtu bila sababu,
wakati hajakutenda dhara lolote.
31 # Za 37:1; Mit 24:1-2 Usimwonee wivu mtu mwenye jeuri
wala kuchagua njia yake iwayo yote,
32 # Za 101:4; Ay 29:4 kwa kuwa Bwana humchukia mtu mpotovu,
lakini siri yake iko kwa mwenye haki.
33 # Ay 5:3; Mal 2:2; Zek 5:4 Laana ya Bwana i juu ya nyumba ya mwovu,
lakini yeye huibariki nyumba ya mwenye haki.
34 # Za 18:25-27; Mt 23:12 Huwadhihaki wale wanaodhihaki,
lakini huwapa neema wale wanyenyekevu.
35Wenye hekima hurithi heshima,
bali huwaaibisha wapumbavu.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014