4
Hekima Ni Bora Kupita Vitu Vyote
1 #
Mit 1:8; 19:20; Ay 8:10 Sikilizeni wanangu, mafundisho ya baba yenu;
sikilizeni kwa makini na mpate ufahamu.
2Ninawapa mafundisho ya maana,
kwa hiyo msiyaache mafundisho yangu.
3 #
1Nya 29:1; 2Sam 12:24 Nilipokuwa mvulana mdogo katika nyumba ya baba yangu,
ningali mchanga na mtoto pekee kwa mama yangu,
4 #
Mit 7:2; 1Nya 28:9 baba alinifundisha akisema,
“Yashike maneno yangu yote kwa moyo wako wote;
yashike maagizo yangu na wewe utaishi.
5 #
Mit 3:13-18; 16:16 Pata hekima, pata ufahamu;
usiyasahau maneno yangu wala usiyaache.
6 #
2The 2:10; Mit 2:11 Usimwache hekima naye atakuweka salama;
mpende, naye atakulinda.
7 #
Mt 13:44-46; Mit 23:23 Hekima ni bora kuliko vitu vyote; kwa hiyo jipe hekima.
Hata ikikugharimu vyote ulivyo navyo, pata ufahamu.
8 #
1Sam 2:30; Mit 3:18 Mstahi, naye atakukweza;
mkumbatie, naye atakuheshimu.
9 #
Mit 1:8-9
Atakuvika shada la neema kichwani mwako
na kukupa taji ya utukufu.”
10 #
Kum 11:21; Mit 3:2 Sikiliza mwanangu, kubali ninachokuambia,
nayo miaka ya maisha yako itakuwa mingi.
11 #
1Sam 12:23; 2Sam 22:37; Za 5:8 Ninakuongoza katika njia ya hekima
na kukuongoza katika mapito yaliyonyooka.
12 #
Ay 18:7; Yer 13:16; Za 18:36 Utembeapo, hatua zako hazitazuiliwa;
ukimbiapo, hutajikwaa.
13 #
Mit 3:22
Mkamate sana elimu, usimwache aende zake;
mshike, maana yeye ni uzima wako.
14 #
Za 1:1; Mit 1:15 Usiuweke mguu wako katika njia ya waovu
wala usitembee katika njia ya watu wabaya.
15Epukana nayo, usisafiri katika njia hiyo;
achana nayo, na uelekee njia yako.
16 #
Za 36:4; Mik 7:3 Kwa kuwa hawawezi kulala mpaka watende uovu;
wanashindwa hata kusinzia mpaka wamwangushe mtu.
17 #
Mwa 49:5; Za 73:6; Mit 1:10-19; Isa 59:6; Yer 22:3; Hab 1:2; Mal 2:16 Wanakula mkate wa uovu,
na kunywa mvinyo wa jeuri.
18 #
Mt 5:14; Ay 17:9; Isa 26:7; Dan 12:3; Yn 8:12 Njia ya wenye haki ni kama nuru ya kwanza ya mapambazuko,
ambayo hungʼaa zaidi na zaidi mpaka mchana mkamilifu.
19 #
Ay 18:5; Yn 12:35 Lakini njia ya waovu ni kama giza nene;
hawajui kinachowafanya wajikwae.
20 #
Za 34:11-16; Mit 1:8-9; 5:1 Mwanangu, yasikilize kwa makini yale ninayokuambia;
sikiliza kwa makini maneno yangu.
21 #
Mit 3:21
Usiruhusu yaondoke machoni pako,
yahifadhi ndani ya moyo wako;
22 #
Mit 3:8
kwa sababu ni uzima kwa wale wanaoyapata
na afya kwa mwili wote wa mwanadamu.
23 #
Mit 10:11; Mt 12:34 Zaidi ya yote, linda moyo wako, kuliko yote uyalindayo,
maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.
24Epusha kinywa chako na ukaidi;
weka mazungumzo machafu mbali na midomo yako.
25 #
Ay 31:1
Macho yako na yatazame mbele,
kaza macho yako moja kwa moja mbele yako.
26 #
Ebr 12:13
Sawazisha mapito ya miguu yako
na njia zako zote ziwe zimethibitika.
27 #
Law 10:11; Kum 28:14 Usigeuke kulia wala kushoto;
epusha mguu wako na ubaya.