Mithali 6
NEN

Mithali 6

6
Maonyo Dhidi Ya Upumbavu
1 # Mwa 43:9; Ebr 7:22; Ezr 10:27; Mit 17:18 Mwanangu, kama umekuwa mdhamini wa jirani yako,
ikiwa umeshika mikono kwa kuweka ahadi
kwa ajili ya mwingine,
2kama umetegwa na ulichosema,
umenaswa kwa maneno ya kinywa chako,
3basi fanya hivi mwanangu, ili ujiweke huru,
kwa kuwa umeanguka mikononi mwa jirani yako:
Nenda ukajinyenyekeshe kwake;
msihi jirani yako!
4 # Rut 3:18; Za 132:4 Usiruhusu usingizi machoni pako,
usiruhusu kope zako zisinzie.
5 # Za 91:3; 2Sam 2:18; Isa 13:14; Za 91:3 Jiweke huru, kama swala mkononi mwa mwindaji,
kama ndege kutoka kwenye mtego wa mwindaji.
6 # Mit 6:11 Ewe mvivu, mwendee mchwa;
zitafakari njia zake ukapate hekima!
7Kwa maana yeye hana msimamizi,
wala mwangalizi, au mtawala,
8 # Mit 30:24-25; 10:4 lakini hujiwekea akiba wakati wa kiangazi
na hukusanya chakula chake wakati wa mavuno.
9 # Mit 24:30-34; 26:13-16 Ewe mvivu, utalala hata lini?
Utaamka lini kutoka usingizi wako?
10 # Mit 24:33; Mhu 4:5 Bado kulala kidogo, kusinzia kidogo,
bado kukunja mikono kidogo upate kupumzika:
11 # Mit 6:10-11; 20:13; 24:30-34 hivyo umaskini utakuja juu yako kama mnyangʼanyi,
na kupungukiwa kutakujia kama mtu mwenye silaha.
12Mtu mbaya sana na mlaghai,
ambaye huzungukazunguka
na maneno ya upotovu,
13 # Za 35:19; Mit 16:30 ambaye anakonyeza kwa jicho lake,
anayetoa ishara kwa miguu yake
na kuashiria kwa vidole vyake,
14 # Za 36:4; 140:2; Mik 2:1; Isa 32:7 ambaye hupanga ubaya
kwa udanganyifu moyoni mwake:
daima huchochea fitina.
15Kwa hiyo maafa yatamkumba ghafula;
ataangamizwa mara, pasipo msaada.
16 # Mit 3:32; 8:13; 15:8, 9, 26; 16:5 Kuna vitu sita anavyovichukia Bwana,
naam, viko saba vilivyo chukizo kwake:
17 # Za 120:2; Mit 12:22; Yer 2:34; Mik 7:2; Hos 4:1-2 macho ya kiburi,
ulimi udanganyao,
mikono imwagayo damu isiyo na hatia,
18 # Mwa 6:5; Ay 15:31; Rum 3:15 moyo uwazao mipango miovu,
miguu iliyo myepesi kukimbilia uovu,
19 # Kum 19:16; Za 27:12; Mit 15:18; Zek 8:17 shahidi wa uongo ambaye humwaga uongo,
na mtu ambaye huchochea fitina kati ya ndugu.
Onyo Dhidi Ya Uasherati
20 # Mit 3:21; 1:8 Mwanangu, zishike amri za baba yako,
wala usiyaache mafundisho ya mama yako.
21 # Kum 6:8; Mit 3:3 Yafunge katika moyo wako daima,
yakaze kuizunguka shingo yako.
22 # Mit 3:23; 2:11 Wakati utembeapo, yatakuongoza;
wakati ulalapo, yatakulinda;
wakati uamkapo, yatazungumza nawe.
23 # Za 19:8; 10:17 Kwa maana amri hizi ni taa,
mafundisho haya ni mwanga
na maonyo ya maadili ni njia ya uzima,
24 # Mwa 39:8; Za 55:21 yakikulinda na mwanamke aliyepotoka,
kutokana na maneno laini ya mwanamke aliyepotoka.
25 # 2Sam 11:2-5; Mt 5:28 Moyo wako usitamani uzuri wake
wala macho yake yasikuteke,
26 # Mit 27:22-23; 29:3; Eze 13:18 kwa maana kahaba atakufanya uwe maskini,
hata ukose kipande cha mkate,
naye mwanamke mzinzi huwinda maisha yako hasa.
27Je, mtu aweza kuchotea moto kwenye paja lake
bila nguo zake kuungua?
28Je, mtu aweza kutembea juu ya makaa ya moto yanayowaka
bila miguu yake kuungua?
29 # Kut 20:14; Mit 2:16-19 Ndivyo alivyo mtu alalaye na mke wa mwanaume mwingine;
hakuna yeyote amgusaye huyo mwanamke ambaye hataadhibiwa.
30Watu hawamdharau mwizi kama akiiba
kukidhi njaa yake wakati ana njaa.
31 # Kut 22:1-14 Pamoja na hayo, kama akikamatwa,
lazima alipe mara saba,
ingawa inamgharimu utajiri wote wa nyumba yake.
32 # Kut 20:14; Mit 7:7; 9:4, 16 Lakini mwanaume aziniye na mwanamke hana akili kabisa;
yeyote afanyaye hivyo hujiangamiza mwenyewe.
33 # Mit 5:9-14 Mapigo na aibu ni fungu lake
na aibu yake haitafutika kamwe;
34 # Hes 5:14; Mwa 34:7 kwa maana wivu huamsha ghadhabu ya mume,
naye hataonyesha huruma alipizapo kisasi.
35 # Ay 31:9-11; Wim 8:7 Hatakubali fidia yoyote;
atakataa malipo, hata yakiwa makubwa kiasi gani.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014