Mithali 7
NEN

Mithali 7

7
Onyo Dhidi Ya Mwanamke Mzinzi
1 # Mt 1:8 Mwanangu, shika maneno yangu
na kuzihifadhi amri zangu ndani yako.
2 # Mit 4:4; Law 18:5; Kum 32:10 Shika amri zangu nawe utaishi;
linda mafundisho yangu kama mboni ya jicho lako.
3 # Kum 6:8; Mit 3:3; Isa 30:8; 2Kor 3:3 Yafunge katika vidole vyako;
yaandike katika kibao cha moyo wako.
4Mwambie hekima, “Wewe ni dada yangu,”
uite ufahamu jamaa yako;
5 # Ay 31:9; Mit 2:16 watakuepusha na mwanamke mzinzi,
kutokana na mwanamke mpotovu
na maneno yake ya kubembeleza.
6Kwenye dirisha la nyumba yangu
nilitazama nje kupitia upenyo
kwenye mwimo wa dirisha.
7 # Mit 6:32 Niliona miongoni mwa wajinga,
nikagundua miongoni mwa wanaume vijana,
kijana asiye na akili.
8Alikuwa akishuka njiani karibu na pembe ya kwake,
akielekea kwenye nyumba ya huyo mwanamke
9 # Ay 24:15 wakati wa machweo, jua likipungua nuru yake,
giza la usiku lilipokuwa likiingia.
10 # 1Tim 2:9 Ndipo huyo mwanamke akatoka kumlaki,
hali amevaa kama kahaba akiwa na nia ya udanganyifu.
11 # Mit 9:13; 1Tim 5:13 (Ni mwanamke mwenye makelele na mkaidi,
miguu yake haitulii nyumbani;
12 # Mit 8:1-36; 23:26-28 mara kwenye barabara za mji,
mara kwenye viwanja vikubwa,
kwenye kila pembe huvizia.)
13 # Mwa 39:12; Mit 1:20 Huyo mwanamke alimkumbatia kijana na kumbusu,
na kwa uso usio na haya akamwambia:
14 # Law 7:11-18 “Nina sadaka za amani nyumbani;
leo nimetimiza nadhiri zangu.
15Kwa hiyo nimetoka nje kukulaki;
nimekutafuta na nimekupata!
16 # Isa 19:9 Nimetandika kitanda changu
kwa kitani za rangi kutoka Misri.
17 # Amo 6:4; Mwa 37:25 Nimetia manukato kitanda changu
kwa manemane, udi na mdalasini.
18 # Mwa 39:7 Njoo, tuzame katika mapenzi mpaka asubuhi;
tujifurahishe wenyewe kwa mapenzi!
19Mume wangu hayupo nyumbani;
amekwenda safari ya mbali.
20Amechukua mkoba uliojazwa fedha
na hatakuwepo nyumbani karibuni.”
21 # Mit 1:8-9; 8:32 Kwa maneno laini yule mwanamke akampotosha;
alimshawishi kwa maneno yake laini.
22 # Ay 18:10 Mara huyo kijana alimfuata yule mwanamke
kama fahali aendaye machinjoni,
kama kulungu aingiaye kwenye kitanzi,
23 # Ay 15:22; 16:13; Mit 6:26; Mhu 9:12 mpaka mshale umchome ini lake,
kama ndege anayenaswa kwenye mtego,
bila kujua itamgharimu maisha yake.
24 # Mit 1:8-9; 8:32 Sasa basi wanangu, nisikilizeni;
sikilizeni kwa makini nisemalo.
25 # Mit 5:7-8 Usiruhusu moyo wako ugeukie njia za huyo mwanamke,
wala usitangetange katika mapito yake.
26 # Neh 13:26 Aliowaangusha ni wengi;
aliowachinja ni kundi kubwa.
27 # Amu 16:19; Ufu 22:15 Nyumba yake ni njia kuu iendayo kaburini,#7:27 Kaburini hapa maana yake ni Kuzimu, kwa Kiebrania ni Sheol.
ielekeayo chini kwenye vyumba vya mauti.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014