9
Makaribisho Ya Hekima Na Ya Upumbavu
1 #
Efe 2:20-22; 1Tim 3:15; 1Pet 3:5 Hekima amejenga nyumba yake;
amechonga nguzo zake saba.
2 #
Lk 14:16-23; Isa 25:6; 62:8 Ameandaa nyama na kuchanganya divai yake;
pia ameandaa meza yake.
3 #
Mit 1:20; 8:1-3; Mt 22:3, 4, 9; Lk 14:17; Rum 10:15 Amewatuma watumishi wake wa kike, naye huita
kutoka mahali pa juu sana pa mji.
4 #
Mit 1:22; 6:32; Mt 11:25 Anawaambia wale wasio na akili,
“Wote ambao ni wajinga na waje hapa!
5 #
Za 42:2; Isa 44:3; Mt 26:26-28 Njooni, mle chakula changu
na mnywe divai niliyoichanganya.
6 #
Mit 8:35; 3:1-2 Acheni njia zenu za ujinga nanyi mtaishi;
tembeeni katika njia ya ufahamu.
7 #
Mit 23:9; Mt 7:6 “Yeyote anayemkosoa mwenye mzaha
hukaribisha matukano;
yeyote anayekemea mtu mwovu
hupatwa na matusi.
8Usimkemee mwenye mzaha la sivyo atakuchukia;
mkemee mwenye hekima naye atakupenda.
9 #
Mit 15:31; 19:25; Mt 13:12 Mfundishe mtu mwenye hekima
naye atakuwa na hekima zaidi;
mfundishe mtu mwadilifu
naye atazidi kufundishika.
10 #
Ay 28:28
“Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
na kumjua Aliye Mtakatifu ni ufahamu.
11 #
Mwa 15:15; Kum 11:21; Mit 10:27 Kwa maana kwa msaada wangu
siku zako zitakuwa nyingi,
na miaka itaongezwa katika maisha yako.
12 #
Ay 35:6, 7 Kama wewe una hekima, hekima yako itakupa tuzo;
kama wewe ni mtu wa mzaha,
wewe mwenyewe ndiwe utateseka.”
13 #
Mit 7:11; 5:6 Mwanamke aitwaye Mpumbavu ana kelele;
hana adabu na hana maarifa.
14 #
Eze 16:25
Huketi kwenye mlango wa nyumba yake,
juu ya kiti katika mahali pa juu sana pa mji,
15 #
Mit 1:20
akiita wale wapitao karibu,
waendao moja kwa moja kwenye njia yao.
16 #
Mit 1:22
Anawaambia wale wasio na akili,
“Wote ambao ni wajinga na waje hapa ndani!”
17 #
Mit 20:17
“Maji yaliyoibiwa ni matamu;
chakula kinacholiwa sirini ni kitamu!”
18 #
Mit 2:18; 7:26-27 Lakini hawajui hata kidogo kuwa wafu wako humo,
kwamba wageni wake huyo mwanamke
wako katika vilindi vya kuzimu.