10
Zaburi 10#10 Zaburi hii ikiunganishwa na ya 9 zimetungwa kila beti likianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Sala Kwa Ajili Ya Haki
1 #
Za 13:1; 22:1, 11; 35:22; 38:21; 71:12 Kwa nini, Ee Bwana, unasimama mbali?
Kwa nini unajificha wakati wa shida?
2 #
Ay 20:19; Mit 5:22; 10:3; Za 49:6; 94:4; Yer 48:30; Ay 1:5 Katika kiburi chake, mwovu humtesa maskini,
waovu na wanaswe katika hila wanazozitunga.
3Hujivunia tamaa za moyo wake;
humbariki mlafi na kumtukana Bwana.
4 #
Za 12:3-5; 36:1; 2Fal 18:35; Ay 21:15 Katika kiburi chake, mwovu hamtafuti Mungu,
katika mawazo yake yote
hakuna nafasi ya Mungu.
5 #
Za 18:27; 105:5; Mit 6:17; Isa 13:11; Yer 48:29 Njia zake daima hufanikiwa;
hujivuna na amri zako ziko mbali naye,
huwacheka kwa dharau adui zake wote.
6 #
Ufu 18:7
Anajisemea mwenyewe, “Hakuna kitakachonitikisa,
daima nitakuwa na furaha,
kamwe sitakuwa na shida.”
7 #
Mhu 4:1; Rum 3:14; Isa 30:12; Ay 20:12; Za 73:8; 119:134 Kinywa chake kimejaa laana, uongo na vitisho;
shida na ubaya viko chini ya ulimi wake.
8 #
Za 37:32; 59:3; 71:10; Mit 1:11; Yer 5:26; Mik 7:2; Hos 6:9 Huvizia karibu na vijiji;
kutoka mafichoni huwanasa wasio na hatia,
akivizia wapitaji.
9 #
Ay 18:8
Huvizia kama simba aliye mawindoni;
huvizia kumkamata mnyonge,
huwakamata wanyonge na kuwaburuza
katika wavu wake.
10 #
Ay 9:17
Mateka wake hupondwa, huzimia;
wanaanguka katika nguvu zake.
11 #
Ay 22:13; 22:14; Za 42:9; 77:9 Anajisemea mwenyewe, “Mungu amesahau,
huficha uso wake na haoni kabisa.”
12 #
Za 3:7; 9:12, 13; 17:7; 20:6; 106:26; Isa 26:11; Mik 5:9 Inuka Bwana! Inua mkono wako, Ee Mungu.
Usiwasahau wanyonge.
13 #
Ay 31:14
Kwa nini mtu mwovu anamtukana Mungu?
Kwa nini anajiambia mwenyewe,
“Hataniita nitoe hesabu?”
14 #
Za 22:11; 37:5; Kum 33:29 Lakini wewe, Ee Mungu, unaona shida na huzuni,
umekubali kuyapokea mkononi mwako.
Mhanga anajisalimisha kwako,
wewe ni msaada wa yatima.
15 #
Ay 31:22
Vunja mkono wa mtu mwovu na mbaya,
mwite atoe hesabu ya maovu yake
ambayo yasingejulikana.
16 #
Kut 15:18; Kum 8:20 Bwana ni Mfalme milele na milele,
mataifa wataangamia watoke nchini mwake.
17 #
Za 9:12; Kut 22:23 Unasikia, Ee Bwana, shauku ya wanaoonewa,
wewe huwatia moyo, na kusikiliza kilio chao,
18 #
Kum 24:17; Za 146:9; 9:9 ukiwatetea yatima na walioonewa,
ili mwanadamu, ambaye ni udongo, asiogopeshe tena.