100
Zaburi 100
Dunia Yote Yaitwa Kumsifu Mungu
Zaburi ya shukrani.
1 #
Za 98:6
Mpigieni Bwana kelele za shangwe, dunia yote.
2 #
Kum 10:12; Za 95:2 Mwabuduni Bwana kwa furaha;
njooni mbele zake kwa nyimbo za shangwe.
3 #
1Fal 18:21; Za 74:1; 46:10; 79:13; Isa 19:25; 63:8, 17-19; 64:9; Ay 10:3, 8, 9; Mhu 12:1; Efe 2:10; Eze 34:30 Jueni kwamba Bwana ndiye Mungu.
Yeye ndiye alituumba, sisi tu mali yake;
sisi tu watu wake,
kondoo wa malisho yake.
4 #
Za 42:4; 96:8; 116:17 Ingieni malangoni mwake kwa shukrani
na katika nyua zake kwa kusifu,
mshukuruni yeye na kulisifu jina lake.
5 #
1Nya 16:34; Ezr 3:11; Za 106:1; 108:4; 119:90 Kwa maana Bwana ni mwema
na upendo wake wadumu milele;
uaminifu wake unadumu kwa vizazi vyote.