101
Zaburi 101
Ahadi Ya Kuishi Kwa Uadilifu Na Kwa Haki
Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 33:1; 51:14; 89:1; 145:7 Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;
kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa.
2 #
Mwa 17:1; 18:10; 1Sam 18:14; Kum 6:7; Flp 1:10; 1Fal 9:4; 3:14 Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:
utakuja kwangu lini?
Nitatembea nyumbani mwangu
kwa moyo usio na lawama.
3 #
Yos 23:6; 1Sam 12:20; Yer 16:18; Eze 11:21; Hos 9:10; Za 5:5 Sitaweka mbele ya macho yangu
kitu kiovu.
Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;
hawatashikamana nami.
4 #
Mit 3:32; 6:16-19; 11:20; Mt 7:23; 1Kor 5:11; 2Tim 2:19 Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;
nitajitenga na kila ubaya.
5 #
Kut 20:16; Law 19:16; Za 10:5; Mit 6:17; Lk 18:14 Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,
huyo nitamnyamazisha;
mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi
huyo sitamvumilia.
6 #
Za 101:2; 119:1 Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,
ili waweze kuishi pamoja nami;
yeye ambaye moyo wake hauna lawama
atanitumikia.
7Mdanganyifu hatakaa
nyumbani mwangu,
yeye asemaye kwa uongo
hatasimama mbele yangu.
8 #
Za 5:3; 75:10; 118:10-12; 46:4; Yos 21:12; 2Sam 3:39; Hos 9:2 Kila asubuhi nitawanyamazisha
waovu wote katika nchi;
nitamkatilia mbali kila mtenda mabaya
kutoka mji wa Bwana.