102
Zaburi 102
Maombi Ya Mtu Mwenye Taabu
Maombi ya mtu aliyechoka. Anapoteseka na kumimina malalamiko yake kwa Bwana.
1 #
Za 4:1; Kut 2:23 Ee Bwana, usikie maombi yangu,
kilio changu cha kuomba msaada kikufikie.
2 #
Za 22:24; 31:2; 88:2; 2Fal 19:16 Usinifiche uso wako
ninapokuwa katika shida.
Unitegee sikio lako,
ninapoita, unijibu kwa upesi.
3Kwa kuwa siku zangu zinatoweka kama moshi,
mifupa yangu inaungua kama kaa la moto.
4 #
Za 37:2; 90:5-6; 1Sam 1:7; Ezr 10:6; Ay 33:26 Moyo wangu umefifia na kunyauka kama jani,
ninasahau kula chakula changu.
5 #
Za 6:6
Kwa sababu ya kusononeka kwangu kwa uchungu,
nimebakia ngozi na mifupa.
6 #
Isa 34:11; Sef 2:14; Kum 14:15-17; Ay 30:29 Nimekuwa kama bundi wa jangwani,
kama bundi kwenye magofu.
7 #
Za 77:4; 38:11 Nilalapo sipati usingizi,
nimekuwa kama ndege mpweke
kwenye paa la nyumba.
8 #
Za 31:11; 42:10; Mdo 23:12 Mchana kutwa adui zangu hunidhihaki,
wale wanaonizunguka hutumia jina langu kama laana.
9 #
Isa 44:20; Za 6:6; 42:3; 80:5 Ninakula majivu kama chakula changu
na nimechanganya kinywaji changu na machozi
10 #
Za 7:11; 38:3; 30:7 kwa sababu ya ghadhabu yako kuu,
kwa maana umeniinua na kunitupa kando.
11 #
1Nya 29:15; Ay 14:2; 8:12; Za 39:6; Yak 1:10 Siku zangu ni kama kivuli cha jioni,
ninanyauka kama jani.
12 #
Kut 15:18; 3:15; Isa 55:13; 63:12; 40:2; Za 135:13 Lakini wewe, Ee Bwana, umeketi katika kiti chako cha enzi milele,
sifa zako za ukuu zaendelea vizazi vyote.
13 #
Za 119:126; 44:26; 77:7; Kum 32:36; 1Fal 3:26; Isa 54:8; 60:10; 40:2; Zek 10:6; Kut 13:10; Dan 8:19; Mdo 1:7 Utainuka na kuihurumia Sayuni,
kwa maana ni wakati wa kumwonyesha wema;
wakati uliokubalika umewadia.
14 #
Dan 9:2
Kwa maana mawe yake ni ya thamani kwa watumishi wako,
vumbi lake lenyewe hulionea huruma.
15 #
1Fal 8:43; Isa 2:2; Za 67:7; 76:12; 138:4; 148:11 Mataifa wataogopa jina la Bwana,
wafalme wote wa dunia watauheshimu utukufu wako.
16 #
Za 51:18; 8:1; Isa 60:1, 2 Kwa maana Bwana ataijenga tena Sayuni
na kutokea katika utukufu wake.
17 #
Neh 2:8; 1Fal 8:29; Za 4:1; 6:9 Ataitikia maombi ya mtu mkiwa,
wala hatadharau hoja yao.
18 #
Rum 4:24; 15:4; Za 22:31; 1Kor 10:1; Isa 43:21 Hili na liandikwe kwa ajili ya kizazi kijacho,
ili taifa litakaloumbwa baadaye waweze kumsifu Bwana:
19 #
Kum 26:15; Za 14:2; 53:2 “Bwana alitazama chini kutoka patakatifu pake palipo juu,
kutoka mbinguni alitazama dunia,
20 #
Za 68:6; Lk 4:19 kusikiliza vilio vya uchungu vya wafungwa
na kuwaweka huru wale waliohukumiwa kufa.”
21 #
Za 22:22; 9:14 Kwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni
na sifa zake katika Yerusalemu,
22 #
Hos 1:11; Za 22:27; Isa 49:22, 23; Zek 8:20-23 wakati mataifa na falme zitakapokusanyika
ili kumwabudu Bwana.
23 #
Za 39:5
Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu,
akafupisha siku zangu.
24 #
Mwa 21:33; Ay 36:26; Za 90:2; Hab 1:12; Ufu 1:4, 8 Ndipo niliposema:
“Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu;
miaka yako inaendelea vizazi vyote.
25 #
Mwa 1:1; Ebr 1:10; 2Nya 2:12; Za 8:3; Kut 20:11; Ay 38:4-7 Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia,
nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.
26 #
Rum 8:20; Isa 51:6; 13:10, 13; 66:21; 34:4; Mt 24:35; Yoe 2:10; Eze 32:8; 2Pet 3:7-10; Ufu 20:11 Hizi zitatoweka, lakini wewe utadumu,
zote zitachakaa kama vazi.
Utazibadilisha kama nguo
nazo zitaondoshwa.
27 #
Hes 23:19; Ebr 13:8; Mal 3:6; Yak 1:17; Za 9:7 Lakini wewe, U yeye yule,
nayo miaka yako haikomi kamwe.
28 #
Za 69:36; 25:13; 89:4 Watoto wa watumishi wako wataishi mbele zako;
wazao wao wataimarishwa mbele zako.”