Zaburi 103
NEN

Zaburi 103

103
Zaburi 103
Upendo Wa Mungu
Zaburi ya Daudi.
1 # Za 28:6; 104:1; 30:4 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.
Vyote vilivyomo ndani yangu
vilihimidi jina lake takatifu.
2 # Za 106:1; 117:1; Kum 6:12; Za 77:11 Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana,
wala usisahau wema wake wote,
3 # Kut 34:7; 15:26; Kol 3:13; 1Pet 2:24; 1Yn 1:9 akusamehe dhambi zako zote,
akuponya magonjwa yako yote,
4 # Za 34:22; 56:13; 8:5; 23:6; Isa 43:1 aukomboa uhai wako na kaburi,
akuvika taji ya upendo na huruma,
5 # Ay 33:25; Za 90:14; 104:28; 119:25, 93; 2Kor 4:16; Kut 19:4 atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema,
ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.
6 # Za 9:8; 74:21; 65:5; Isa 9:7; Lk 4:10 Bwana hutenda haki,
naye huwapa hukumu ya haki wote wanaoonewa.
7 # Za 99:7; 147:19; 106:22; Kut 33:13 Alijulisha Mose njia zake,
na wana wa Israeli matendo yake.
8 # Kut 22:27; 34:6; Za 86:15; Mik 7:18-19; Yak 5:11; Kum 5:10; Hes 14:18 Bwana ni mwingi wa huruma na mwenye neema;
si mwepesi wa hasira, bali amejaa upendo.
9 # Yer 3:5, 12; Mik 7:18; Isa 57:16; Za 30:5; 79:5 Yeye hatalaumu siku zote,
wala haweki hasira yake milele,
10 # Ezr 9:13; Rum 6:23 yeye hatutendei kulingana na dhambi zetu
wala hatupatilizi kwa kadiri ya maovu yetu.
11 # Efe 3:18; Za 13:5; 57:10; 100:5; 106:45; 117:2; Mao 3:22; 2Nya 6:31 Kama vile mbingu zilivyo juu ya dunia sana,
ndivyo wema wake ulivyo mwingi kwa wanaomcha;
12 # 2Sam 12:13; Rum 4:7; Efe 1:7; 2:5; Isa 43:25 kama mashariki ilivyo mbali na magharibi,
ndivyo Mungu alivyoziweka dhambi zetu mbali nasi.
13 # Mal 3:17; Kum 8:5; 1Yn 3:1; Isa 63:15, 16 Kama baba alivyo na huruma kwa watoto wake,
ndivyo Bwana anavyowahurumia wale wanaomcha;
14 # Za 119:73; 139:13-15; 146:4; Isa 29:16; Mwa 2:7 kwa kuwa anajua tulivyoumbwa,
anakumbuka kwamba sisi tu mavumbi.
15 # Za 37:2; 90:5; 102:11; Yak 1:10; Isa 40:6; Ay 14:2 Kuhusu mwanadamu, siku zake ni kama majani,
anachanua kama ua la shambani;
16 # Isa 40:7; Hag 1:9; Ay 7:8 upepo huvuma juu yake nalo hutoweka,
mahali pake hapalikumbuki tena.
17 # Mwa 48:11; Ezr 9:12; Kut 20:6 Lakini kutoka milele hata milele
upendo wa Bwana uko kwa wale wamchao,
nayo haki yake kwa watoto wa watoto wao:
18 # Yn 14:15; Kum 7:9; 28:9; Za 119:52; Hes 15:40; Za 47:8; 80:1; 113:5; 22:28; 66:7; Dan 4:17 kwa wale walishikao agano lake
na kukumbuka kuyatii mausia yake.
19 Bwana ameweka imara kiti chake cha enzi mbinguni,
ufalme wake unatawala juu ya vyote.
20 # Neh 9:6; Lk 2:13; Ebr 1:14; Za 29:1; 28:6; 107:25; 135:7; 148:8; Mt 6:10 Mhimidini Bwana, enyi malaika zake,
ninyi mlio mashujaa mnaozitii amri zake,
ninyi mnaotii neno lake.
21 # 1Fal 22:19; Neh 7:73; Dan 7:9; Mwa 32:2 Mhimidini Bwana, ninyi jeshi lake lote la mbinguni,
ninyi watumishi wake mnaofanya mapenzi yake.
22 # Za 104:1; 67:3; 19:1; 145:10; 150:1, 6 Mhimidini Bwana, kazi zake zote
kila mahali katika milki yake.
Ee nafsi yangu, umhimidi Bwana.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014