Zaburi 105
NEN

Zaburi 105

105
Zaburi 105
Uaminifu Wa Mungu Kwa Israeli
(1 Nyakati 16:8-22)
1 # 1Nya 16:34; Za 80:18; 99:6; 116:13; Yoe 2:32; Mdo 2:21; Isa 12:4 Mshukuruni Bwana, liitieni jina lake,
wajulisheni mataifa yale aliyoyatenda.
2 # Za 30:4; 146:2; 33:3; 96:1; 7:17; 18:49; 27:6; 59:17; 71:22; 75:1 Mwimbieni yeye, mwimbieni yeye sifa,
waambieni matendo yake yote ya ajabu.
3 # Za 89:16 Lishangilieni jina lake takatifu,
mioyo ya wale wamtafutao Bwana na ifurahi.
4 # Za 24:6; 27:8 Mtafuteni Bwana na nguvu zake,
utafuteni uso wake siku zote.
5 # Za 40:5; Kum 7:18; 8:2 Kumbuka matendo ya ajabu aliyoyafanya,
miujiza yake na hukumu alizozitamka,
6 # Za 105:42; Kum 10:15; Za 106:5 enyi wazao wa Abrahamu mtumishi wake,
enyi wana wa Yakobo, wateule wake.
7 # Isa 26:8 Yeye ndiye Bwana Mungu wetu,
hukumu zake zimo duniani pote.
8 # Mwa 9:15; Za 106:45; 111:5; Eze 16:60; Lk 1:72 Hulikumbuka agano lake milele,
neno ambalo aliamuru, kwa vizazi elfu,
9 # Mwa 22:16-18; 15:18; Ebr 6:17; Lk 1:73; 17:2; 12:7; Gal 3:15-18; Dan 9:4 agano alilolifanya na Abrahamu,
kiapo alichomwapia Isaki.
10 # Mwa 28:13-15; Isa 55:3 Alilithibitisha kwa Yakobo kuwa amri,
kwa Israeli liwe agano la milele:
11 # Mwa 12:7; Hes 34:2 “Nitakupa wewe nchi ya Kanaani
kuwa sehemu utakayoirithi.”
12 # Kum 7:7; Ebr 11:9; Mwa 17:8; 23:4; 34:30 Walipokuwa wachache kwa idadi,
wachache sana na wageni ndani yake,
13 # Mwa 15:13-16; Hes 32:13; 33:3-49 walitangatanga kutoka taifa moja hadi jingine,
kutoka ufalme mmoja hadi mwingine.
14 # Mwa 35:5; 12:17-20; 20:3; Za 9:5 Hakuruhusu mtu yeyote awaonee;
kwa ajili yao aliwakemea wafalme, akisema:
15 # Mwa 26:11; 20:7; 1Sam 12:3 “Msiwaguse niliowatia mafuta;
msiwadhuru manabii wangu.”
16 # Isa 3:1; Law 26:26; Mwa 12:10; 41:54; 2Fal 8:1; Eze 4:16 Akaiita njaa juu ya nchi
na kuharibu chakula chao chote,
17 # Mwa 45:5; 37:28; Mdo 7:9 naye akatuma mtu mbele yao,
Yosefu, aliyeuzwa kama mtumwa.
18 # Mwa 40:15 Walichubua miguu yake kwa minyororo,
shingo yake ilifungwa kwa chuma,
19 # Mwa 12:10; 41:40; 40:20-21 hadi yale aliyotangulia kusema yalipotimia,
hadi neno la Bwana lilipomthibitisha.
20 # Mwa 41:14 Mfalme alituma watu wakamfungua,
mtawala wa watu alimwachia huru.
21Alimfanya mkuu wa nyumba yake,
mtawala juu ya vyote alivyokuwa navyo,
22 # Mwa 41:43-44; 41:40 kuwaelekeza wakuu wa mfalme apendavyo
na kuwafundisha wazee wake hekima.
23 # Mdo 7:15; 13:17; Mwa 46:6; 47:28; Za 78:51 Kisha Israeli akaingia Misri,
Yakobo akaishi kama mgeni katika nchi ya Hamu.
24 # Kut 1:7; Kum 26:7; Mdo 7:17 Bwana aliwafanya watu wake kuzaana sana,
akawafanya kuwa wengi sana kuliko adui zao,
25 # Kut 4:21; 1:6-10; Mdo 7:19 ndiye aliigeuza mioyo yao iwachukie watu wake,
wakatenda hila dhidi ya watumishi wake.
26 # Kut 3:10; 4:16; Hes 33:1; 16:5; 17:5-8 Akamtuma Mose mtumishi wake,
pamoja na Aroni, aliyemchagua.
27 # Za 105:28-37; Kut 7:8; 12:51; 4:17; 10:1; 3:20; Dan 4:3 Walifanya ishara zake za ajabu miongoni mwao,
miujiza yake katika nchi ya Hamu.
28 # Mwa 1:4; Za 99:7; Kut 10:22; 7:22 Alituma giza na nchi ikajaa giza,
kwani si walikuwa wameyaasi maneno yake?
29 # Za 78:44; Kut 7:21 Aligeuza maji yao kuwa damu,
ikasababisha samaki wao kufa.
30 # Kut 8:2, 6 Nchi yao ilijaa vyura tele, ambao waliingia
hadi kwenye vyumba vya kulala vya watawala wao.
31 # Za 78:45; 107:25; 148:8; Kut 8:16-18; 8:21-24 Alisema, yakaja makundi ya mainzi,
na viroboto katika nchi yao yote.
32 # Kut 9:22-25; Ay 38:22; Za 78:47 Alibadilisha mvua yao ikawa mvua ya mawe,
yenye umeme wa radi nchini yao yote,
33 # Za 78:47; Kut 10:5, 12 akaharibu mizabibu yao na miti ya tini,
na akaangamiza miti ya nchi yao.
34 # Za 107:25; Kut 10:4, 12-15; 1Fal 8:27; Yoe 1:6 Alisema, nzige wakaja,
tunutu wasio na idadi,
35wakala kila jani katika nchi yao,
wakala mazao ya ardhi yao.
36 # Kut 4:23; 12:12 Kisha akawaua wazaliwa wote wa kwanza katika nchi yao,
matunda ya kwanza ya ujana wao wote.
37 # Kut 3:21, 22 Akawatoa Israeli katika nchi
wakiwa na fedha na dhahabu nyingi,
wala hakuna hata mmoja
kutoka kabila zao aliyejikwaa.
38 # Kut 15:16 Misri ilifurahi walipoondoka,
kwa sababu hofu ya Israeli ilikuwa imewaangukia.
39 # Kut 13:21; 1Kor 10:1; Za 78:14; Neh 9:12 Alitandaza wingu kama kifuniko,
na moto kuwamulikia usiku.
40 # Za 78:18; Kut 16:4; Yn 6:31; Kut 16:12 Waliomba, naye akawaletea kware,
akawashibisha kwa mkate wa mbinguni.
41 # Hes 20:11; 1Kor 10:4; Kut 17:6; Neh 9:15; Isa 48:21 Alipasua mwamba, maji yakabubujika,
yakatiririka jangwani kama mto.
42 # Mwa 15:1-4, 13-16; 13:14-17 Kwa maana alikumbuka ahadi yake takatifu,
aliyompa Abrahamu mtumishi wake.
43 # Kut 15:1-19; Za 106:12 Aliwatoa watu wake kwa furaha,
wateule wake kwa kelele za shangwe,
44 # Kum 6:10-11; Za 106:12 akawapa nchi za mataifa, wakawa warithi
wa mali wengine walikuwa wameitaabikia:
45 # Kum 6:14-21; 4:1, 40; Za 105:35; 78:5-7 alifanya haya ili wayashike mausia yake
na kuzitii sheria zake.
Msifuni Bwana.#105:45 Msifuni Bwana kwa Kiebrania ni Hallelu Yah.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014