Zaburi 106
NEN

Zaburi 106

106
Zaburi 106
Wema Wa Bwana Kwa Watu Wake
1 # Ezr 3:11; Za 63:7; 22:23; 103:2; 119:68; 136:1-26; Yer 33:11; Mt 19:17 Msifuni Bwana.
Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;
upendo wake wadumu milele.
2 # Za 40:5; 71:16 Ni nani awezaye kusimulia matendo makuu ya Bwana
au kutangaza kikamilifu sifa zake?
3 # Yer 22:15, 16; Mt 22:37; Za 15:2; 112:5; Hos 12:6 Heri wale wanaodumisha haki,
ambao daima wanafanya yaliyo mema.
4 # Za 25:6-7; 77:7; Mwa 50:24 Ee Bwana, unikumbuke unapowatendea mema watu wako,
uwe msaada wangu unapowaokoa,
5 # Kum 30:15; Za 1:3; 105:6; 20:5; 27:5; 47:5; 118:15; Kut 34:9 ili niweze kufurahia mafanikio ya wateule wako,
niweze kushiriki katika furaha ya taifa lako,
na kuungana na urithi wako katika kukusifu.
6 # 1Fal 8:47; Neh 1:7; Dan 9:5; Rum 3:9; 2Nya 30:7; Law 26:40 Tumetenda dhambi, kama vile baba zetu walivyotenda,
tumekosa na tumetenda uovu.
7 # Amu 3:7; Za 78:42; Kut 14:11, 12 Wakati baba zetu walipokuwa Misri,
hawakuzingatia maajabu yako,
wala hawakukumbuka wingi wa fadhili zako,
bali waliasi kando ya bahari, Bahari ya Shamu.
8 # Kut 9:16; 14:30-31; Za 80:3; 107:13; 23:3; 143:11; Isa 25:9; Yoe 2:32; Yos 7:9; Yer 14:7, 21 Hata hivyo aliwaokoa kwa ajili ya jina lake,
ili apate kudhihirisha uweza wake mkuu.
9 # Nah 1:4; Isa 50:3; 63:11-14; Kut 14:21; Za 18:15; 78:13 Alikemea Bahari ya Shamu, nayo ikakauka,
akawaongoza katika vilindi vyake kama vile jangwani.
10 # Kut 14:30; Za 107:13; 78:42, 53; Isa 35:9; 62:12 Aliwaokoa mikononi mwa adui;
kutoka mikononi mwa adui aliwakomboa.
11 # Kut 14:28 Maji yaliwafunika adui zao,
hakunusurika hata mmoja.
12 # Kut 15:1-21; Za 105:43 Ndipo walipoamini ahadi zake,
nao wakaimba sifa zake.
13 # Kut 15:24; 16:28; Hes 27:21 Lakini mara walisahau aliyowatendea,
wala hawakungojea shauri lake.
14 # 1Kor 10:9; Kut 17:2; Za 78:40; 68:7 Jangwani walitawaliwa na tamaa zao,
walimjaribu Mungu nyikani.
15 # Isa 10:16; Hes 11:33; Kut 16:13; Za 78:29 Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba,
lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha.
16 # Hes 16:1-3 Kambini walimwonea wivu Mose,
na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.
17 # Kum 11:6; 15:12; Hes 16:1 Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani,
ikawazika Abiramu na kundi lake.
18 # Law 10:2 Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao,
mwali wa moto uliwateketeza waovu.
19 # Kut 32:4; Mdo 7:41 Huko Horebu walitengeneza ndama,
na kuabudu sanamu ya kusubu kwa chuma.
20 # Yer 2:11; Rum 1:23 Waliubadilisha Utukufu wao
kwa sanamu ya fahali, ambaye hula majani.
21 # Za 78:11; 75:1; Kum 10:21 Walimsahau Mungu aliyewaokoa,
aliyekuwa ametenda mambo makuu huko Misri,
22 # Za 78:51; Kut 3:20; Kum 4:34 miujiza katika nchi ya Hamu
na mambo ya kutisha huko Bahari ya Shamu.
23 # Kut 32:10-14; Hes 11:2; Eze 13:5; 20:13; Kum 9:19 Kwa hiyo alisema kwamba angewaangamiza:
kama Mose mteule wake,
asingesimama kati yao na Mungu
kuizuia ghadhabu yake kuwaangamiza.
24 # Ebr 3:18; Yer 3:19; Hes 14:11, 30, 31; Kum 8:7 Kisha waliidharau ile nchi nzuri,
hawakuiamini ahadi yake.
25 # Kut 15:24; Kum 1:27; 1Kor 10:10 Walinungʼunika ndani ya mahema yao,
wala hawakumtii Bwana.
26 # Hes 14:23; Ebr 4:3; 3:17; Kum 2:14 Kwa hiyo akaapa kwa mkono ulioinuliwa
kwamba atawafanya waanguke jangwani,
27 # Law 26:33 kuwatawanya wazao wao waanguke miongoni mwa mataifa,
na kuwatawanya katika nchi zote.
28 # Hes 23:28; 25:2, 3; Kum 4:3; Hos 9:10; Ufu 2:14 Walijifunga nira na Baali wa Peori,
wakala dhabihu zilizotolewa kwa miungu isiyo na uhai.
29 # Za 64:2; 141:4; Hes 16:46; 25:3, 8 Waliichochea hasira ya Bwana,
wakamkasirisha kwa matendo yao maovu,
nayo tauni ikazuka katikati yao.
30 # Kut 6:25; Hes 25:8 Lakini Finehasi alisimama na kuingilia kati,
nayo tauni ikazuiliwa.
31 # Mwa 15:6; Za 49:11; Hes 15:11-13 Hili likahesabiwa kwake haki,
kwa vizazi visivyo na mwisho vijavyo.
32 # Kum 1:37; Kut 17:7; Hes 20:2-13 Kwenye maji ya Meriba, walimkasirisha Bwana,
janga likampata Mose kwa sababu yao;
33 # Kut 17:4-7; 23:21; Yak 3:2; Isa 63:10; Za 107:11; 51:11; Hes 20:8-12 kwa maana walimwasi Roho wa Mungu,
na maneno yasiyofaa yakatoka midomoni kwa Mose.
34 # Amu 1:21, 27-36; 2:2; Yos 9:15; Kum 2:34; 7:2, 16; 20:10; Kut 23:24 Hawakuyaangamiza yale mataifa
kama Bwana alivyowaagiza,
35 # Amu 3:5, 6; Ezr 9:1, 2 bali walijichanganya na mataifa
na wakazikubali desturi zao.
36 # Kut 10:7; 23:33; Amu 2:12; 2Fal 17:8-11; 2Nya 33:2-7; Kum 7:10, 16 Waliabudu sanamu zao,
zikawa mtego kwao.
37 # Isa 57:5; Kut 10:7; 22:20; Law 18:21; Kum 32:17; 12:31; 7:16; 1Kor 10:20; Eze 16:20-21 Wakawatoa wana wao
na binti zao dhabihu kwa mashetani.
38 # 2Fal 3:27; Hes 35:33; Law 18:21; Kum 18:10 Walimwaga damu isiyo na hatia,
damu za wana wao na binti zao,
ambao waliwatoa dhabihu kwa sanamu za Kanaani,
nayo nchi ikanajisika kwa damu zao.
39 # Mwa 3:17; Law 18:24; Eze 20:18; Hes 15:39 Wakajinajisi wenyewe kwa yale waliyotenda;
kwa matendo yao wenyewe wakajifanyia ukahaba.
40 # Law 26:28; Kut 34:9; 9:29 Kwa hiyo Bwana akawakasirikia watu wake
na akauchukia sana urithi wake.
41 # Amu 2:14; Neh 9:27 Akawakabidhi kwa mataifa
na adui zao wakawatawala.
42 # Amu 4:3 Adui zao wakawaonea
na kuwatia chini ya mamlaka yao.
43 # Amu 7:1-25; 2:16-19; 6:1-7; Yos 10:14; Neh 9:28 Mara nyingi aliwaokoa
lakini walikuwa wamezama kwenye uasi,
nao wakajiharibu katika dhambi zao.
44 # Amu 3:9; 10:10 Lakini akaangalia mateso yao
wakati aliposikia kilio chao;
45 # Mwa 9:15; Lk 1:72; Za 105:8; 103:11; 17:7; Law 26:41; Mao 3:32; Kut 32:14 kwa ajili yao akakumbuka agano lake,
na kutokana na upendo wake mkuu akapooza hasira yake.
46 # 1Nya 16:8; Mt 19:17; 2Nya 5:13; 7:3 Akawafanya wahurumiwe
na wote waliowashikilia mateka.
47 # Za 147:2; 105:1; 30:4; 99:3; 28:9; 107:3; Isa 11:12; 27:13; 56:8; 66:20; Yer 31:8; Lk 1:74; Eze 20:34; Mik 4:6; 2Kor 5:15 Ee Bwana Mungu wetu, tuokoe.
Tukusanye tena kutoka kwa mataifa,
ili tuweze kulishukuru jina lako takatifu,
na kushangilia katika sifa zako.
48 # Za 41:13; 72:19 Atukuzwe Bwana, Mungu wa Israeli,
tangu milele na hata milele.
Watu wote na waseme, “Amen!”
Msifuni Bwana.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014