107
KITABU CHA TANO
(Zaburi 107–150)
Zaburi 107
Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake
1 #
1Nya 16:8; 2Nya 5:13; 7:3; Mt 19:17 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa yeye ni mwema,
upendo wake wadumu milele.
2 #
Za 106:10; Isa 35:9 Waliokombolewa wa Bwana na waseme hivi,
wale aliowaokoa kutoka mkono wa adui,
3 #
Za 106:47; Isa 49:12; Hes 1:9; Yer 29:14; Eze 39:27 wale aliowakusanya kutoka nchi mbalimbali,
kutoka mashariki na magharibi,
kutoka kaskazini na kusini.
4 #
Yos 5:6; Za 107:36 Baadhi yao walitangatanga jangwani,
hawakuona njia ya kuwafikisha mji ambao wangeweza kuishi.
5 #
Kut 16:3; 15:22; 17:2 Walikuwa na njaa na kiu,
nafsi zao zikadhoofika.
6 #
Kut 14:10; Za 50:15; Isa 41:17; Hos 5:15; Yer 29:12-14 Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
naye akawaokoa kutoka taabu yao.
7 #
Ezr 8:21, 36; Isa 38:12 Akawaongoza kwa njia iliyo sawa
hadi mji ambao wangeweza kuishi.
8 #
Za 105:1; 6:4; 75:1 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,
9 #
Za 22:26; 63:5; 23:1; 34:10; Mt 5:6; Yer 31:25; Lk 1:53; Isa 55:1; 58:11 kwa maana yeye humtosheleza mwenye kiu,
na kumshibisha mwenye njaa kwa vitu vyema.
10 #
Za 107:14; 88:6; 143:3; 102:20; Isa 9:2; 42:7, 16; 49:9; 61:1; Mik 7:9; Ay 36:8 Wengine walikaa gizani na katika huzuni kuu,
wafungwa wakiteseka katika minyororo,
11 #
Za 5:10; Hes 14:11; 1Fal 22:5; 2Nya 36:16 kwa sababu walikuwa wameasi
dhidi ya maneno ya Mungu
na kudharau shauri
la Aliye Juu Sana.
12 #
Isa 63:5; Za 72:12; 2Fal 14:26 Aliwatumikisha kwa kazi ngumu;
walijikwaa na hapakuwepo yeyote wa kuwasaidia.
13 #
Za 106:8
Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
naye akawaokoa kutoka taabu yao.
14 #
Isa 9:2; 42:7; 59:9; 50:10; 60:2; 29:18; Ay 36:8; Lk 1:79; Za 86:13; 116:16; 146:7; Mdo 12:7 Akawatoa katika giza na huzuni kuu
na akavunja minyororo yao.
15 #
Za 107:8, 21, 31; 105:1; 6:4; 75:1 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu,
16 #
Isa 45:2
kwa kuwa yeye huvunja malango ya shaba
na kukata mapingo ya chuma.
17 #
Za 53:1; 25:7; Law 14:1; 26:16; Isa 65:6, 7; Yer 30:14, 15; Gal 6:7, 8; Mt 1:22; Mao 3:39 Wengine wakawa wapumbavu kutokana na uasi wao,
wakapata mateso kwa sababu ya uovu wao.
18 #
Ay 3:24; 6:6; 17:16; 33:22 Wakachukia kabisa vyakula vyote,
wakakaribia malango ya mauti.
19 #
Za 107:13; 5:2; 34:4 Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
naye akawaokoa kutoka taabu yao.
20 #
Kum 32:2; Mt 8:8; 2Fal 20:4; Lk 7:7; Kut 15:26; Hes 21:8; Za 30:3; 16:10; 56:13; 147:15; Ay 33:28 Akalituma neno lake na kuwaponya,
akawaokoa kutoka maangamizo yao.
21 #
Za 107:15; 6:4; 75:1 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.
22 #
Law 7:12; Za 9:11; 73:28; 65:8; 50:14; 118:17; Ay 8:21; Ebr 13:15 Na watoe dhabihu za kushukuru,
na wasimulie matendo yake kwa nyimbo za furaha.
23 #
Isa 42:10; Za 104:26 Wengine walisafiri baharini kwa meli,
walikuwa wafanyabiashara kwenye maji makuu.
24 #
Za 64:9; 111:2; 143:5 Waliziona kazi za Bwana,
matendo yake ya ajabu kilindini.
25 #
Za 105:31; 50:3; 93:3 Kwa maana alisema na kuamsha tufani
iliyoinua mawimbi juu.
26 #
Za 22:14; Isa 13:7; Nah 2:10; Lk 8:23; Yos 2:11 Yakainuka juu mbinguni, yakashuka chini hadi vilindini,
katika hatari hii ujasiri wao uliyeyuka.
27 #
Isa 19:14; 24:20; 28:7 Walipepesuka na kuyumbayumba kama walevi,
ujanja wao ukafikia ukomo.
28 #
Za 107:19; 4:1; Yon 1:6 Ndipo walipomlilia Bwana katika shida yao,
naye akawatoa kwenye taabu yao.
29 #
Lk 8:24; Za 93:3; 65:7; Mk 4:39-41; Yon 1:15; Isa 50:2; Mt 8:26 Akatuliza dhoruba kwa mnongʼono,
mawimbi ya bahari yakatulia.
30 #
Za 107:7
Walifurahi ilipokuwa shwari,
naye akawaongoza hadi bandari waliyoitamani.
31 #
Za 107:15; 6:4; 75:1; 106:2 Basi na wamshukuru Bwana kwa upendo wake usiokoma,
na kwa matendo yake ya ajabu kwa wanadamu.
32 #
Za 30:1; 34:3; 99:5; 1:5; 22:22; 26:12; 35:18 Na wamtukuze yeye katika kusanyiko la watu,
na wamsifu katika baraza la wazee.
33 #
1Fal 17:1; Yoe 1:20; Isa 41:15; 42:15; 50:2; 34:9, 10; Eze 30:12; Nah 1:4; Za 74:15; 104:10 Yeye aligeuza mito kuwa jangwa,
chemchemi za maji zitiririkazo kuwa ardhi yenye kiu,
34 #
Mwa 13:10
nchi izaayo ikawa ya chumvi isiyofaa,
kwa sababu ya uovu wa wale walioishi humo.
35 #
2Fal 3:17; Za 105:41; 126:4; Isa 43:19; 51:3; 35:7; Ay 38:26 Aligeuza jangwa likawa madimbwi ya maji,
nayo ardhi kame kuwa chemchemi za maji zitiririkazo;
36 #
Mdo 17:26
aliwaleta wenye njaa wakaishi humo,
nao wakajenga mji wangeweza kuishi.
37 #
2Fal 19:29; Isa 37:30 Walilima mashamba na kupanda mizabibu,
nayo ikazaa matunda mengi,
38 #
Mwa 12:2; 49:25; Kum 7:13 Mungu aliwabariki, hesabu yao ikaongezeka sana,
wala hakuruhusu mifugo yao kupungua.
39 #
2Fal 10:32; Eze 5:12; Za 44:9 Kisha hesabu yao ilipungua, na walinyenyekeshwa
kwa kuonewa, maafa na huzuni.
40 #
Ay 12:18, 21; Kum 32:10 Yeye ambaye huwamwagia dharau wakuu,
aliwafanya watangetange nyikani isiyo na njia.
41 #
1Sam 2:8; 2Sam 7:8; Za 113:7-9; Ay 21:11; 8:7 Lakini yeye aliwainua wahitaji katika taabu zao,
na kuongeza jamaa zao kama makundi ya kondoo.
42 #
Ay 22:19; 5:16; Mit 10:11; Rum 3:19; Za 97:10-12 Wanyofu wataona na kufurahi,
lakini waovu wote watafunga vinywa vyao.
43 #
Yer 9:12; Hos 14:9; Za 103:11; Dan 12:10 Yeyote aliye na hekima, ayasikie mambo haya,
na atafakari upendo mkuu wa Bwana.