108
Zaburi 108
Kuomba Msaada Dhidi Ya Adui
(Zaburi 57:7-11; 60:5-12)
Wimbo. Zaburi ya Daudi.
1 #
Za 112:7; 119:30, 112; 18:49 Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti;
nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote.
2 #
Ay 21:12
Amka, kinubi na zeze!
Nitayaamsha mapambazuko.
3Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa;
nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu.
4 #
Hes 14:18; Kum 7:9; Kut 34:6; Za 36:5; Mik 7:18-20 Kwa maana upendo wako ni mkuu, ni juu kuliko mbingu;
uaminifu wako unazifikia anga.
5 #
Za 8:1; 57:5 Ee Mungu, utukuzwe juu ya mbingu,
utukufu wako na uenee duniani kote.
6 #
Ay 40:14
Tuokoe na utusaidie kwa mkono wako wa kuume,
ili wale uwapendao wapate kuokolewa.
7 #
Za 89:35; 68:35; 102:19; Mwa 12:6; 33:17 Mungu amenena kutoka patakatifu pake:
“Nitaigawa Shekemu kwa ushindi
na kulipima Bonde la Sukothi.
8 #
Za 78:68; Mwa 49:10 Gileadi ni yangu, Manase ni yangu,
Efraimu ni kofia yangu ya chuma,
nayo Yuda ni fimbo yangu ya utawala.
9 #
Mwa 19:37; 2Sam 8:1, 13-14 Moabu ni sinia langu la kunawia,
juu ya Edomu natupa kiatu changu;
nashangilia kwa kushindwa kwa Ufilisti.”
10 #
Za 60:9
Ni nani atakayenipeleka hadi mji wenye ngome?
Ni nani atakayeniongoza hadi nifike Edomu?
11 #
Za 44:9
Ee Mungu, si ni wewe uliyetukataa sisi,
na hutoki tena na majeshi yetu?
12 #
Isa 10:3; 30:3, 5; 31:3; Yer 2:36; 17:7; Za 118:8; 146:3 Tuletee msaada dhidi ya adui,
kwa maana msaada wa mwanadamu haufai kitu.
13 #
Za 44:5; Isa 22:5; 63:3, 6; 25:10; Mao 1:15; Mal 4:3; Ufu 14:9 Kwa msaada wa Mungu tutapata ushindi,
naye atawaponda adui zetu.