109
Zaburi 109
Lalamiko La Mtu Aliyeko Kwenye Shida
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 #
Kut 15:2; Yer 17:14; Ay 34:29; Za 83:1 Ee Mungu, ambaye ninakusifu,
usiwe kimya,
2 #
Za 43:1; 52:4 kwa maana watu waovu na wadanganyifu
wamefungua vinywa vyao dhidi yangu;
wasema dhidi yangu
kwa ndimi za udanganyifu.
3 #
Za 69:4; 35:7; 35:7, 10; Yn 15:25; 1Sam 19:4, 5 Wamenizunguka kwa maneno ya chuki,
wananishambulia bila sababu.
4 #
Za 69:13; 141:5 Wanachonilipa badala ya urafiki wangu ni kunishtaki,
lakini mimi ninawaombea.
5 #
Mwa 44:4; Za 38:20 Wananilipiza mabaya kwa mema,
chuki badala ya urafiki wangu.
6 #
1Nya 21:1; Ay 1:6; Zek 3:1 Agiza mtu mwovu ampinge,
mshtaki#109:6 Mshtaki hapa maana yake ni Shetani. asimame mkono wake wa kuume.
7 #
Za 1:5; Mit 28:9; Zek 3:1 Anapohukumiwa, apatikane na hatia,
nayo maombi yake yamhukumu.
8 #
Ay 15:32; Mdo 1:20 Siku zake za kuishi na ziwe chache,
nafasi yake ya uongozi ichukuliwe na mtu mwingine.
9 #
Kut 22:24; Yer 18:21 Watoto wake na waachwe yatima,
mke wake na awe mjane.
10 #
Mwa 4:12
Watoto wake na watangetange wakiomba,
na wafukuzwe kwenye magofu ya nyumba zao.
11 #
Hes 14:3; Isa 1:7; 6:11; 36:1; Mao 5:2; Neh 5:3; Ay 20:18; 18:9 Mtu anayemdai na ateke vyote alivyo navyo,
matunda ya kazi yake yatekwe nyara na wageni.
12 #
Ay 5:4
Asiwepo mtu yeyote wa kumtendea mema
wala wa kuwahurumia yatima wake.
13 #
Za 21:10; 9:5; 37:28; Hes 14:12; Mit 10:7; Ay 18:19 Uzao wake na ukatiliwe mbali,
majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho.
14 #
Kut 20:5
Maovu ya baba zake na yakumbukwe
mbele za Bwana,
dhambi ya mama yake
isifutwe kamwe.
15 #
Za 90:8; Kut 17:14; Kum 32:26; Ay 18:17 Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana,
ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.
16 #
Ay 20:19; Za 35:10; 34:18 Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema,
bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,
aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo.
17 #
Mit 28:27; Mt 7:2 Alipenda kulaani,
nayo laana ikampata;
hakupenda kubariki,
kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.
18 #
Za 10:7; Hes 5:22 Alivaa kulaani kama vazi lake,
nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji,
kwenye mifupa yake kama mafuta.
19 #
Za 109:29; 73:6; Eze 7:27 Na iwe kama joho alilozungushiwa,
kama mshipi aliofungiwa daima.
20 #
Kut 32:34; Za 54:5; 94:23; 7:10; Isa 3:11; 2Tim 4:14 Haya na yawe malipo ya Bwana kwa washtaki wangu,
kwa wale wanaoninenea mabaya.
21 #
Kut 9:16; Za 3:7; 23:3; 69:16 Lakini wewe, Ee Bwana Mwenyezi,
unitendee wema kwa ajili ya jina lako,
uniokoe kwa wema wa pendo lako.
22Maana mimi ni maskini na mhitaji,
moyo wangu umejeruhiwa ndani yangu.
23 #
Ay 14:2
Ninafifia kama kivuli cha jioni,
nimerushwa-rushwa kama nzige.
24 #
Ebr 12:12; Ay 16:8; Za 35:13 Magoti yangu yamelegea kwa kufunga,
mwili wangu umedhoofika na kukonda.
25 #
Za 22:6; Ay 16:4; Mt 27:39; Mk 15:29; Isa 37:22 Nimekuwa kitu cha kudharauliwa kwa washtaki wangu,
wanionapo, hutikisa vichwa vyao.
26 #
Za 12:1; 119:86 Ee Bwana, Mungu wangu nisaidie,
niokoe sawasawa na upendo wako.
27 #
Ay 37:7
Watu na wafahamu kuwa ni mkono wako,
kwamba wewe, Ee Bwana, umetenda hili.
28 #
2Sam 16:12; Za 66:4; Isa 35:10; 51:11; 54:1; 65:14; Hes 22:12 Wanaweza kulaani, lakini wewe utabariki,
watakaposhambulia wataaibishwa,
lakini mtumishi wako atashangilia.
29 #
Za 35:26
Washtaki wangu watavikwa fedheha,
na kufunikwa na aibu kama joho.
30 #
Za 35:18
Kwa kinywa changu nitamtukuza sana Bwana,
katika umati mkubwa nitamsifu.
31 #
Za 16:8; 108:6 Kwa maana husimama mkono wa kuume wa mhitaji,
kuokoa maisha yake kutoka kwa wale wanaomhukumu.