110
Zaburi 110
Bwana Na Mfalme Wake Mteule
Zaburi ya Daudi.
1 #
Mt 22:44; Lk 20:42; Mdo 2:34; Mk 12:36; 16:19; Ebr 1:13; 12:2; Yos 10:24; 1Fal 5:3; 1Kor 15:25; Za 45:6 Bwana amwambia Bwana wangu:
“Keti mkono wangu wa kuume,
mpaka nitakapowafanya adui zako
kuwa mahali pa kuweka miguu yako.”
2 #
Mwa 49:10; Za 45:6; 2:6; 72:8; Isa 14:5; Yer 48:17 Bwana ataeneza fimbo yako ya utawala yenye nguvu kutoka Sayuni;
utatawala katikati ya adui zako.
3 #
Kut 15:11; Mik 5:7 Askari wako watajitolea kwa hiari
katika siku yako ya vita.
Ukiwa umevikwa fahari takatifu,
kutoka tumbo la mapambazuko
utapokea umande wa ujana wako.#110:3 Au: vijana wako watakujia kama umande.
4 #
Hes 23:19; Zek 6:13; Ebr 5:6; 5:10; 7:15-17; 7:21; Mwa 14:18 Bwana ameapa,
naye hatabadilisha mawazo yake:
“Wewe ni kuhani milele,
kwa mfano wa Melkizedeki.”
5 #
Za 16:8; 2:12; 68:21; 76:12; Kum 7:24; Isa 60:12; Dan 2:44; Za 2:5; Rum 2:5; Ufu 6:17; 11:18 Bwana yuko mkono wako wa kuume,
atawaponda wafalme siku ya ghadhabu yake.
6 #
Za 9:19; 18:38; Isa 5:25; 34:3; 66:24 Atawahukumu mataifa, akilundika mizoga
na kuwaponda watawala wa dunia nzima.
7 #
Za 3:3; 27:6 Atakunywa maji katika kijito kando ya njia,#110:7 Au: Yeye atoaye mtu wa kurithi mwingine atamweka kwenye mamlaka.
kwa hiyo atainua kichwa chake juu.