111
Zaburi 111#111 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Sifa Za Bwana Kwa Matendo Ya Ajabu
1 #
Za 34:1; 109:30; 115:18; 145:10; 9:1; 89:7; 1:5 Msifuni Bwana.
Nitamtukuza Bwana kwa moyo wangu wote,
katika baraza la wanyofu na katika kusanyiko.
2 #
Ay 36:24; Za 143:5; 64:9; Ufu 15:3 Kazi za Bwana ni kuu,
wote wanaopendezwa nazo huzitafakari.
3 #
Za 112:3, 9; 119:142 Kazi zake zimejaa fahari na utukufu,
haki yake hudumu daima.
4 #
Kum 4:31; Za 86:15 Amefanya maajabu yake yakumbukwe,
Bwana ni mwenye neema na huruma.
5 #
Mwa 1:30; Za 37:25; 103:11; 105:8; Mt 6:26, 31-33; 1Nya 16:15 Huwapa chakula wale wanaomcha,
hulikumbuka agano lake milele.
6 #
Za 64:9; 66:3; 105:44 Amewaonyesha watu wake uwezo wa kazi zake,
akiwapa nchi za mataifa mengine.
7 #
Za 92:4; 19:7; 119:128 Kazi za mikono yake ni za uaminifu na haki,
mausia yake yote ni ya kuaminika.
8 #
Za 119:89, 152, 160; Isa 40:8; Mt 5:18 Zinadumu milele na milele,
zikifanyika kwa uaminifu na unyofu.
9 #
Za 34:22; 103:4; 130:7; 30:4; 99:3; Lk 1:68; 1:49 Aliwapa watu wake ukombozi,
aliamuru agano lake milele:
jina lake ni takatifu na la kuogopwa.
10 #
Ay 23:15; Kum 4:6; Za 19:9; 119:98, 104, 130; 28:6; 89:52 Kumcha Bwana ndicho chanzo cha hekima,
wote wanaozifuata amri zake wana busara.
Sifa zake zadumu milele.