112
Zaburi 112#112 Zaburi hii imetungwa kila mstari ukianzia na herufi ya alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T); zote ni 22.
Baraka Za Mwenye Haki
1 #
Za 33:2; 103:1; 150:1; 1:1, 2; Ay 1:8; Za 103:11; 115:13; 128:1; 1:2; 119:14, 16, 47, 92 Msifuni Bwana.
Heri mtu yule amchaye Bwana,
mtu yule apendezwaye sana na amri zake.
2 #
Za 25:13; 37:26; 128:2-4 Watoto wake watakuwa wenye uwezo katika nchi,
kizazi cha watu waadilifu kitabarikiwa.
3 #
Kum 8:18; Za 37:6; 111:3 Nyumbani mwake kuna mali na utajiri,
haki yake hudumu milele.
4 #
Za 18:28; 5:12 Hata gizani nuru humzukia mtu mwadilifu,
yule mwenye rehema, huruma na haki.
5 #
Za 37:21, 26; Lk 6:35 Mema yatamjia mtu yule aliye mkarimu na mwenye kukopesha bila riba,
anayefanya mambo yake kwa haki.
6 #
Za 15:5; 55:22; Mit 10:7; Mhu 2:16 Hakika hatatikisika kamwe,
mtu mwenye haki atakumbukwa milele.
7 #
Za 57:7; 108:1; 28:7; 56:3-4; Isa 12:2 Hataogopa habari mbaya,
moyo wake ni thabiti, ukimtegemea Bwana.
8 #
Za 3:6; 27:1; 54:7; 56:11; Mit 1:33; Isa 12:2 Moyo wake ni salama, hatakuwa na hofu,
mwishoni ataona ushindi dhidi ya adui zake.
9 #
Lk 19:8; Mdo 9:36; 2Kor 9:9; Za 111:3; 75:10 Ametawanya vipawa vyake kwa ukarimu akawapa maskini;
haki yake hudumu milele;
pembe yake itatukuzwa kwa heshima.
10 #
Za 86:17; 34:21; 37:12; Mt 8:12; Ay 8:13 Mtu mwovu ataona na kuchukizwa,
atasaga meno yake na kutoweka,
kutamani kwa mtu mwovu kutaishia patupu.