113
Zaburi 113
Kumsifu Bwana Kwa Wema Wake
1 #
Za 22:23; 34:22; 103:21; 134:1 Msifuni Bwana.
Enyi watumishi wa Bwana msifuni,
lisifuni jina la Bwana.
2 #
Za 30:4; 48:10; 145:21; 148:13; 149:3; 115:18; 131:3; Isa 12:4; Dan 2:20 Jina la Bwana na lisifiwe,
sasa na hata milele.
3 #
Isa 24:15; 45:6; 59:19; Mal 1:11 Kuanzia mawio ya jua hadi machweo yake,
jina la Bwana linapaswa kusifiwa.
4 #
Za 99:2; 8:1; 57:11 Bwana ametukuka juu ya mataifa yote,
utukufu wake juu ya mbingu.
5 #
Kut 8:10; Ay 16:19; Za 35:10; 103:19 Ni nani aliye kama Bwana Mungu wetu,
Yeye ambaye ameketi juu kwenye kiti cha enzi,
6 #
Za 11:4; 138:6; Isa 57:15 ambaye huinama atazame chini
aone mbingu na nchi?
7 #
1Sam 2:8; Za 35:10; 68:10; 140:12; 107:41 Huwainua maskini kutoka mavumbini,
na kuwanyanyua wahitaji kutoka kwenye jalala,
8 #
2Sam 9:11
huwaketisha pamoja na wakuu,
pamoja na wakuu wa watu wake.
9 #
1Sam 2:5
Humjalia mwanamke tasa kutulia nyumbani mwake,
akiwa mama watoto mwenye furaha.
Msifuni Bwana.