114
Zaburi 114
Maajabu Ya Mungu Wakati Israeli Walipotoka Misri
1 #
Kut 13:3; 29:46 Wakati Israeli walipotoka Misri,
nyumba ya Yakobo kutoka kwa watu wa lugha ngeni,
2 #
Kut 15:17; Za 76:1; 78:68, 69 Yuda alifanywa makao matakatifu ya Mungu,
Israeli akawa milki yake.
3 #
Kut 14:21; Za 77:16; Kut 15:8; Yos 3; 16 Bahari ilitazama ikakimbia,
Yordani ulirudi nyuma,
4 #
Amu 5:5
milima ilirukaruka kama kondoo dume,
vilima kama wana-kondoo.
5 #
Kut 14:21
Ee bahari, ni nini kilichokufanya ukakimbia,
nawe, ee Yordani, ukarudi nyuma,
6enyi milima mkarukaruka kama kondoo dume,
enyi vilima, kama wana-kondoo?
7 #
Kut 15:14; 1Nya 16:30 Ee dunia, tetemeka mbele za Bwana,
mbele za Mungu wa Yakobo,
8 #
Kut 17:6; Hes 20:11 aliyegeuza mwamba kuwa dimbwi la maji,
mwamba mgumu kuwa chemchemi za maji.