115
Zaburi 115
Mungu Mmoja Wa Kweli
1 #
Za 29:2; 96:8; Kut 34:6 Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi,
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako.
2 #
Za 42:3, 10; 79:10; Yoe 2:17 Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?”
3 #
Ezr 5:11; Neh 1:4; Za 136:26; 135:6; 103:19; Mit 6:9; Dan 4:35; 1Nya 16:26 Mungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo.
4 #
2Fal 19:18; 2Nya 32:19; Yer 10:3-5; Mdo 19:26; Kum 4:28; Ufu 9:20; Za 135:15, 16; Isa 40:19; Hos 8:6; 1Kor 10:19, 20 Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5 #
Yer 10:5
Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8 #
Za 135:18; Isa 44:9, 10; Yon 2:8; Hab 2:18 Wale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
9 #
Za 37:3; 62:8; 33:20; Mit 30:5 Ee nyumba ya Israeli, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
10 #
Kut 30:30; Za 118:3; Mal 2:7 Ee nyumba ya Aroni, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
11 #
Za 22:23; 103:11; 118:4 Ninyi mnaomcha, mtumainini Bwana,
yeye ni msaada na ngao yao.
12 #
1Nya 16:15; Mwa 12:2; Efe 1:3 Bwana anatukumbuka na atatubariki:
ataibariki nyumba ya Israeli,
ataibariki nyumba ya Aroni,
13 #
Za 24:4; 112:1; Law 26:3; Mit 10:6; Kum 11:27 atawabariki wale wanaomcha Bwana,
wadogo kwa wakubwa.
14 #
Kum 1:11
Bwana na awawezeshe kuongezeka,
ninyi na watoto wenu.
15 #
Mdo 14:15; Ufu 10:6; Za 96:5; Mwa 1:1; 14:19 Mbarikiwe na Bwana
Muumba wa mbingu na dunia.
16 #
Za 89:11; Mwa 1:28; 8:6-8 Mbingu zilizo juu sana ni mali ya Bwana,
lakini dunia amempa mwanadamu.
17 #
Za 88:10-12
Sio wafu wanaomsifu Bwana,
wale washukao mahali pa kimya,#115:17 Mahali pa kimya maana yake ni Kuzimu, yaani Sheol kwa Kiebrania.
18 #
Za 111:1; 113:2; 28:6; 33:2; 105:1; 145:2; Dan 2:20 bali ni sisi tunaomtukuza Bwana,
sasa na hata milele.
Msifuni Bwana.#115:18 Msifuni Bwana ni Kiebrania Hallelu Yah.