116
Zaburi 116
Shukrani Kwa Kuokolewa Kutoka Mauti
1 #
Za 18:1; 31:22; 40:1; 6:9; 28:2 Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu;
amesikia kilio changu ili anihurumie.
2 #
Za 5:1
Kwa sababu amenitegea sikio lake,
nitamwita siku zote za maisha yangu.
3 #
2Sam 22:6; Za 18:4-5 Kamba za mauti zilinizunguka,
maumivu makuu ya kuzimu yalinipata,
nikalemewa na taabu na huzuni.
4 #
Za 80:2, 18; 118:5 Ndipo nikaliitia jina la Bwana:
“Ee Bwana, niokoe!”
5 #
Kut 22:27; 9:27; Ezr 9:15; Za 11:7; 86:15; 2Nya 12:6; Neh 9:8; Yer 12:1; Mao 1:18; Ufu 16:5 Bwana ni mwenye neema na haki,
Mungu wetu ni mwingi wa huruma.
6 #
Za 79:8; 18:3; 22:5; 107:13 Bwana huwalinda wanyenyekevu,
nilipokuwa katika shida kubwa, aliniokoa.
7 #
Za 13:6; 106:1; 142:7; 46:10; 62:1; 131:2; Mt 11:29; Yer 6:16 Ee nafsi yangu, tulia tena,
kwa kuwa Bwana amekuwa mwema kwako.
8 #
Za 86:13
Kwa kuwa wewe, Ee Bwana,
umeniokoa nafsi yangu na mauti,
macho yangu kutokana na machozi,
miguu yangu kutokana na kujikwaa,
9 #
Mwa 5:22; Za 56:13; 89:15; 27:13; Ay 28:13; Isa 38:11; Yer 11:9 ili niweze kutembea mbele za Bwana,
katika nchi ya walio hai.
10 #
Za 9:18; 72:2; 107:17; 119:67, 71, 75; 2Kor 4:13 Niliamini, kwa hiyo nilisema,
“Mimi nimeteseka sana.”
11 #
Yer 9:3-5
Katika taabu yangu nilisema,
“Wanadamu wote ni waongo.”
12 #
Za 103:2; 106:1 Nimrudishie Bwana nini
kwa wema wake wote alionitendea?
13 #
Za 105:1
Nitakiinua kikombe cha wokovu
na kulitangaza jina la Bwana.
14 #
Hes 30:2; Za 66:13 Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana
mbele za watu wake wote.
15 #
Za 72:14; Hes 23:10; Ay 5:26; Lk 16:22; Ufu 14:13 Kifo cha watakatifu kina thamani
machoni pa Bwana.
16 #
Za 119:125; 143:12; 86:16; Ay 12:18 Ee Bwana, hakika mimi ni mtumishi wako,
mimi ni mtumishi wako,
mwana wa mjakazi wako;#116:16 Au: mwanao mwaminifu.
umeniweka huru
toka katika minyororo yangu.
17 #
Law 7:12; Ezr 1:4 Nitakutolea dhabihu ya kukushukuru
na kuliita jina la Bwana.
18 #
Za 116:14; Law 22:18 Nitazitimiza nadhiri zangu kwa Bwana
mbele za watu wake wote,
19 #
Za 102:21; 92:13; 135:2; 96:8; 100:4 katika nyua za nyumba ya Bwana,
katikati yako, ee Yerusalemu.
Msifuni Bwana.