118
Zaburi 118
Shukrani Kwa Ajili Ya Ushindi
1 #
1Nya 16:8; Ezr 3:11; 2Nya 7:3; 5:13 Mshukuruni Bwana, kwa kuwa ni mwema;
upendo wake wadumu milele.
2 #
Za 115:9; 106:1; 136:1-26 Israeli na aseme sasa:
“Upendo wake wadumu milele.”
3 #
Kut 30:30; Za 115:10 Nyumba ya Aroni na iseme sasa:
“Upendo wake wadumu milele.”
4 #
Za 115:11
Wote wamchao Bwana na waseme sasa:
“Upendo wake wadumu milele.”
5 #
Za 18:6; 31:7; 77:2; 120:1; 118:21; 34:4; 86:7; 116:1; 138:3 Wakati wa maumivu yangu makuu nilimlilia Bwana,
naye akanijibu kwa kuniweka huru.
6 #
Kum 31:6; Ebr 13:5; Za 56:5 Bwana yuko pamoja nami, sitaogopa.
Mwanadamu anaweza kunitenda nini?
7 #
Kum 33:29; Ebr 13:6; Za 54:4 Bwana yuko pamoja nami,
yeye ni msaidizi wangu.
Nitawatazama adui zangu
wakiwa wameshindwa.
8 #
Yer 17:5, 7; Za 9:9; 62:8; 5:11; 37:3; 40:4; 108:12; Isa 25:4; 57:13; 2:22; 2Nya 32:7-8 Ni bora kumkimbilia Bwana
kuliko kumtumainia mwanadamu.
9 #
Za 146:3; Isa 30:2, 3 Ni bora kumkimbilia Bwana
kuliko kuwatumainia wakuu.
10 #
Za 37:9
Mataifa yote yalinizunguka,
lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
11 #
Za 88:17; 3:6 Walinizunguka pande zote,
lakini kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
12 #
Mhu 7:6; Za 58:9; 37:9; Kum 1:44 Walinizunguka kama kundi la nyuki,
lakini walikufa haraka kama miiba iteketeayo;
kwa jina la Bwana naliwakatilia mbali.
13 #
Za 118:7; 86:17; 2Nya 18:31 Nilisukumwa nyuma karibu kuanguka,
lakini Bwana alinisaidia.
14 #
Kut 15:2; Za 62:2 Bwana ni nguvu yangu na wimbo wangu,
yeye amefanyika wokovu wangu.
15 #
Ay 8:21; Lk 1:51; Za 106:5; 89:13; 108:6; Kut 15:6 Sauti za shangwe na ushindi
zinavuma hemani mwa wenye haki:
“Mkono wa kuume wa Bwana
umetenda mambo makuu!
16 #
Kut 15:6
Mkono wa kuume wa Bwana
umeinuliwa juu,
mkono wa kuume wa Bwana
umetenda mambo makuu!”
17 #
Hab 1:12; Za 6:5; 64:9; 71:16; 73:28; Kum 32:3 Sitakufa, bali nitaishi,
nami nitatangaza yale Bwana aliyoyatenda.
18 #
Yer 31:18; Ebr 12:5; 1Kor 11:32; Za 86:13; Mit 3:11, 12 Bwana ameniadhibu vikali,
lakini hakuniacha nife.
19 #
Isa 26:2; Za 24:7; 100:4 Nifungulie malango ya haki,
nami nitaingia na kumshukuru Bwana.
20 #
Ufu 22:14; Za 122:1, 2; 15:1, 2; 24:3-4 Hili ni lango la Bwana
ambalo wenye haki wanaweza kuliingia.
21 #
Za 118:5; 27:1 Nitakushukuru, kwa kuwa ulinijibu,
umekuwa wokovu wangu.
22 #
Mdo 4:11; Isa 8:14; 17:10; 19:13; 28:16; Mt 21:42; Lk 20:17; Zek 4:7; 10:4; Mk 12:10; 1Pet 2:7; Efe 2:20 Jiwe walilolikataa waashi,
limekuwa jiwe kuu la pembeni.
23 #
Ay 5:9; Mt 21:42; Mk 12:11 Bwana ametenda hili,
nalo ni la kushangaza machoni petu.
24 #
Za 70:4; 2Kor 6:2 Hii ndiyo siku Bwana aliyoifanya,
tushangilie na kufurahi ndani yake.
25 #
Za 28:9; 116:4 Ee Bwana, tuokoe,
Ee Bwana, utujalie mafanikio.
26 #
Zek 4:7; Mt 11:3; 21:9; 23:39; Mk 11:9; Lk 13:35; 19:38; Yn 12:13; Za 129:8 Heri yule ajaye kwa jina la Bwana.
Kutoka nyumba ya Bwana tunakubariki.
27 #
Za 27:1; Mal 4:2; Isa 60:1; 58:10; 19:20; 1Fal 18:21; 1Pet 2:9; Mik 7:9; Law 23:40; Es 8:2; Kut 27:2 Bwana ndiye Mungu,
naye ametuangazia nuru yake.
Mkiwa na matawi mkononi,
unganeni kwenye maandamano ya sikukuu
hadi kwenye pembe za madhabahu.
28 #
Mwa 28:21; Za 16:2; 63:1; Isa 25:1; Kut 15:2 Wewe ni Mungu wangu, nitakushukuru,
wewe ni Mungu wangu, nitakutukuza.
29Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema;
upendo wake wadumu milele.