Zaburi 119
NEN

Zaburi 119

119
Zaburi 119#119:0 Zaburi hii imetungwa kila beti likianzia, na pia kila mstari katika lile beti, na herufi 22 za alfabeti ya Kiebrania zikifuatana tangu Aleph (A) hadi Taw (T).
Sifa Za Sheria Ya Bwana
Kujifunza Sheria Ya Bwana
1 # Mwa 17:1; Za 1:2; 128:1; Kum 18:13; Mit 11:20 Heri wale walio waadilifu katika njia zao,
wanaoenenda katika sheria ya Bwana.
2 # Za 40:16; 112:1; 119:146; Isa 56:2; Kum 10:12; Mit 9:7; 1Nya 16:11 Heri wale wanaozishika shuhuda zake,
wamtafutao kwa moyo wao wote.
3 # Za 59:4; 128:1; Yn 3:9; 5:18; Yer 6:16; 7:23; Rum 7:16, 17 Wasiofanya lolote lililo baya,
wanaoenenda katika njia zake.
4 # Za 103:18; 119:56; Kum 6:17 Umetoa maagizo yako
ili tuyatii kwa ukamilifu.
5 # Law 19:37; Yer 31:33; 2Kor 3:5; Rum 7:22, 23 Laiti mwenendo wangu ungekuwa imara
katika kuyatii maagizo yako!
6 # Za 119:46, 80, 117; Ay 22:26; 1Yn 2:28 Hivyo mimi sitaaibishwa
ninapozingatia amri zako zote.
7 # Kum 4:8 # Za 90:13; 103:13; 119:47 Nitakusifu kwa moyo mnyofu
ninapojifunza sheria zako za haki.
8 # Za 38:21 Nitayatii maagizo yako;
usiniache kabisa.
Kutii Sheria Ya Bwana
9 # Za 119:65, 169; 39:1; Mit 1:4, 10 Kijana aifanye njia yake kuwa safi jinsi gani?
Ni kwa kutii, akilifuata neno lako.
10 # Za 119:21, 118; 9:1; 2Nya 15:15 Ninakutafuta kwa moyo wangu wote,
usiniache niende mbali na amri zako.
11 # Isa 63:13; Mit 3:23; Za 119:133, 165; 18:22-23; Kum 6:6; Lk 2:19; Ay 22:22 Nimelificha neno lako moyoni mwangu
ili nisikutende dhambi.
12 # Isa 63:13; Lk 2:19 Sifa ni zako, Ee Bwana,
nifundishe maagizo yako.
13 # Za 119:72 Kwa midomo yangu nitasimulia sheria zote
zinazotoka katika kinywa chako.
14 # Za 119:111 Ninafurahia kufuata sheria zako
kama mtu afurahiaye mali nyingi.
15 # Za 119:97, 148; 1:2 Ninatafakari maagizo yako
na kuziangalia njia zako.
16 # Za 112:1 Ninafurahia maagizo yako,
wala sitalipuuza neno lako.
Furaha Katika Sheria Ya Bwana
17 # Za 13:6; 116:7; 119:67; 103:20 Mtendee mema mtumishi wako, nami nitaishi;
nitalitii neno lako.
18Yafungue macho yangu nipate kuona
mambo ya ajabu katika sheria yako.
19 # Mwa 23:4; Ebr 11:13 Mimi ni mgeni duniani,
usinifiche amri zako.
20 # Za 84:2; 119:131; 42:2; 63:1; Isa 26:9 Nafsi yangu inataabika kwa shauku kubwa
juu ya sheria zako wakati wote.
21 # Za 119:10, 51; 5:5; Ay 30:1; Yer 20:7; 50:32; Kum 27:26; Dan 4:37; Mal 3:15 Unawakemea wenye majivuno, waliolaaniwa
waendao mbali na amri zako.
22 # Za 39:8; 119:2 Niondolee dharau na dhihaka,
kwa kuwa ninazishika sheria zako.
23Ingawa watawala huketi pamoja na kunisingizia,
mtumishi wako atatafakari juu ya maagizo yako.
24Sheria zako ni furaha yangu,
nazo ni washauri wangu.
Kuamua Kuitii Sheria Ya Bwana
25 # Za 44:25; 143:11; 119:9, 50, 107 Nimelazwa chini mavumbini,
yahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.
26 # Za 25:4; 27:11; 86:11; 1Fal 8:36 Nilikueleza njia zangu ukanijibu,
nifundishe sheria zako.
27 # Za 105:2; 145:5 Nijulishe mafundisho ya mausia yako,
nami nitatafakari maajabu yako.
28 # Za 119:9; 116:3; 18:1; 6:7; Yer 45:3; Isa 51:11; 40:29; 41:10 Nafsi yangu imechakazwa kwa huzuni,
uniimarishe sawasawa na neno lako.
29 # Za 26:4; Hes 6:25; Mit 30:8; Ebr 8:10 Niepushe na njia za udanganyifu,
kwa neema unifundishe sheria zako.
30 # Yos 24:22; Za 26:3; 108:1 Nimechagua njia ya kweli,
nimekaza moyo wangu katika sheria zako.
31 # Kum 10:20 Nimengʼangʼania sheria zako, Ee Bwana,
usiniache niaibishwe.
32 # 1Fal 4:29; Isa 60:5; 2Kor 6:11 Nakimbilia katika njia ya maagizo yako,
kwa kuwa umeuweka moyo wangu huru.
Maombi Ili Kupata Ufahamu Wa Sheria
33 # Za 119:12 Ee Bwana, nifundishe kuyafuata maagizo yako,
nami nitayashika mpaka mwisho.
34 # Za 119:27, 69, 73, 144, 169; Mit 2:6; Ay 32:8; Yak 1:5; Kum 6:25; Dan 2:21 Nipe ufahamu, nami nitaishika sheria yako
na kuitii kwa moyo wangu wote.
35 # Za 119:32; 1:2; 25:4, 5 Niongoze kwenye njia ya amri zako,
kwa kuwa huko napata furaha.
36 # Yos 24:23; Ebr 13:5; Mk 7:21; 12:15; Eze 33:31; 1Tim 6:10 Ugeuze moyo wangu kuelekea sheria zako,
na siyo kwenye mambo ya ubinafsi.
37 # Za 119:9, 25; 71:20; Ay 31:1 Geuza macho yangu kutoka kwenye mambo yasiyofaa,
uyahifadhi maisha yangu sawasawa na neno lako.
38 # Hes 23:19; 2Sam 7:25 Mtimizie mtumishi wako ahadi yako,
ili upate kuogopwa.
39 # Za 119:22; 69:9; 89:51; Isa 25:8; 51:7; 54:4 Niondolee aibu ninayoiogopa,
kwa kuwa sheria zako ni njema.
40 # Za 119:20, 25, 149, 154 Tazama jinsi ninavyoonea shauku mausia yako!
Hifadhi maisha yangu katika haki yako.
Kuitumainia Sheria Ya Bwana
41 # Za 6:4; 119:76, 116, 154, 170 Ee Bwana, upendo wako usiokoma unijie,
wokovu wako sawasawa na ahadi yako,
42 # Mit 27:11; Za 42:10 ndipo nitakapomjibu anayenidhihaki,
kwa kuwa ninalitumainia neno lako.
43 # Za 119:74, 81, 114, 147; 1Fal 17:24 Usilinyakue neno la kweli kutoka kinywani mwangu,
kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika amri zako.
44 # Za 119:33, 34, 55; Kum 6:25 Nitaitii amri yako daima,
naam, milele na milele.
45 # Za 119:94, 155; Yn 8:32, 36; Rum 8:2 Nitatembea nikiwa huru,
kwa kuwa nimejifunza mausia yako.
46 # Mt 10:18; Mdo 26:1, 2; Za 119:6 Nitasema sheria zako mbele za wafalme
wala sitaaibishwa,
47 # Za 119:77, 97, 127, 143, 159, 163, 165 kwa kuwa ninazifurahia amri zako
kwa sababu ninazipenda.
48 # Mwa 24:63 Ninaziinulia amri zako ambazo ninazipenda mikono yangu,
nami ninatafakari juu ya maagizo yako.
Matumaini Katika Sheria Ya Bwana
49 # Za 119:9, 43 Kumbuka neno lako kwa mtumishi wako,
kwa sababu umenipa tumaini.
50 # Za 119:25; 27:13; Yer 15:16; Rum 5:3-5; Ebr 6:17-19 Faraja yangu katika mateso yangu ni hii:
Ahadi yako inahifadhi maisha yangu.
51 # Za 119:21; Ay 16:10; 17:2; 23:11; Yer 20:7 Wenye majivuno wamenisimanga bila kuchoka,
hata hivyo sitaiacha sheria yako.
52 # Za 103:18 Ee Bwana, ninazikumbuka sheria zako za zamani,
nazo zinanifariji.
53 # Kut 32:19; 33:4; Za 89:30; Ezr 9:3 Nimeshikwa sana na ghadhabu kwa ajili ya waovu,
ambao wameacha sheria yako.
54 # Za 119:172; 101:1; 138:5 Maagizo yako ni kiini cha nyimbo zangu
popote ninapoishi.
55 # Za 119:44, 62, 72; 1:2; 42:8; 63:6; 77:2; Isa 26:9; Mdo 16:25 Ee Bwana, wakati wa usiku ninalikumbuka jina lako,
nami nitatii sheria yako.
56 # Za 119:4, 100, 134; Hes 15:40 Hili limekuwa zoezi langu:
nami ninayatii mausia yako.
Kujitolea Katika Sheria Ya Bwana
57 # Kum 32:9; Yer 51:19; Za 119:17, 67, 101; Mao 3:24 Ee Bwana, wewe ni fungu langu,
nimeahidi kuyatii maneno yako.
58 # Kum 4:29; Ezr 9:8; 1Nya 16:11; Za 34:4; 119:41; Mwa 43:29 Nimetafuta uso wako kwa moyo wangu wote,
nihurumie sawasawa na ahadi yako.
59 # Yoe 2:13; Lk 15:17; Yos 24:14, 15 Nimezifikiri njia zangu
na nimeelekeza hatua zangu katika mausia yako.
60 # Za 119:115 Nitafanya haraka bila kuchelewa
kuzitii amri zako.
61 # Za 119:83, 109, 153, 176 Hata waovu wanifunge kwa kamba,
sitasahau sheria yako.
62 # Za 119:55; 119:7; Mdo 16:25 Usiku wa manane ninaamka kukushukuru
kwa sababu ya sheria zako za haki.
63 # Za 15:4; 101:6, 7; 103:11; 119:56; 111:10 Mimi ni rafiki kwa wale wote wakuchao,
kwa wote wanaofuata mausia yako.
64 # Za 33:5; 119:12, 108 Ee Bwana, dunia imejaa upendo wako,
nifundishe maagizo yako.
Thamani Ya Sheria Ya Bwana
65 # Isa 50:2; 59:1; Za 119:9, 17; 125:4; Mik 2:7 Mtendee wema mtumishi wako
Ee Bwana, sawasawa na neno lako.
66 # Za 51:6 Nifundishe maarifa na uamuzi mzuri,
kwa kuwa ninaamini amri zako.
67 # Za 116:10; 95:10; 119:17; Ebr 12:11; Yer 8:4; 31:18; Kum 32:15; Ufu 3:19 Kabla sijapata shida nilipotea njia,
lakini sasa ninalitii neno lako.
68 # Za 100:5; 106:1; 107:1; 135:3; Kut 18:20; 34:6; Mt 19:17 Wewe ni mwema, unalotenda ni jema,
nifundishe maagizo yako.
69 # Ay 13:4; Za 109:2 Ingawa wenye majivuno wamenisingizia uongo,
nitafuata mausia yako kwa moyo wangu wote.
70 # Mdo 28:27; Za 17:10; Isa 29:13 Mioyo yao ni katili na migumu,
bali mimi napendezwa na sheria yako.
71 # Za 119:67, 75; Ebr 12:10 Ilikuwa vyema mimi kupata shida
ili nipate kujifunza maagizo yako.
72 # Ay 28:17; Za 19:10; Mt 8:10 Sheria inayotoka kinywani mwako ina thamani kubwa kwangu
kuliko maelfu ya vipande vya fedha na dhahabu.
Haki Ya Sheria Ya Bwana
73 # Mwa 1:27; Ay 4:17; 10:8; Za 139:13-16; 100:3; 138:8 Mikono yako ilinifanya na kuniumba,
nipe ufahamu niweze kujifunza amri zako.
74 # Za 34:2; 119:9; 130:5 Wakuchao wafurahie wanaponiona,
kwa kuwa nimeweka tumaini langu katika neno lako.
75 # Za 89:30, 31; 119:7, 138, 172; Ebr 12:5-11 Ee Bwana, ninajua kwamba sheria zako ni za haki,
katika uaminifu wako umeniadhibu.
76 # Za 6:4; 119:41 Upendo wako usiokoma uwe faraja yangu,
sawasawa na ahadi yako kwa mtumishi wako.
77Huruma yako na inijie ili nipate kuishi,
kwa kuwa naifurahia sheria yako.
78 # Za 119:51; 35:19; 119:86, 161; 25:3; Yer 50:32 Wenye majivuno na waaibishwe kwa kunikosea mimi bila sababu,
lakini mimi nitatafakari juu ya mausia yako.
79 # Za 119:27, 125 Wale wakuchao na wanigeukie mimi,
hao ambao wanazielewa sheria zako.
80 # Za 119:1; 119:6; 1Fal 8:61; Mwa 26:5 Moyo wangu usiwe na lawama katika kutii maagizo yako,
ili nisiaibishwe.
Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa
81 # Za 119:20, 43, 123; 84:2; 73:26 Nafsi yangu inazimia kwa kutamani wokovu wako,
lakini nimeweka tumaini langu katika neno lako.
82 # Mao 2:11; Za 6:7; 69:3; 119:41, 123 Macho yangu yamefifia, nikingoja ahadi yako;
ninasema, “Utanifajiri lini?”
83 # Za 119:61; 119:84; Ay 30:30; Ufu 6:10; Yer 12:3; 15:15; 20:11; Za 39:4; 6:3; 119:51; 7:6 Ingawa nimekuwa kama kiriba kwenye moshi,
bado sijasahau maagizo yako.
84Mtumishi wako itampasa angoje mpaka lini?
Ni lini utawaadhibu washtaki wangu?
85 # Za 35:7; 119:51; 57:6; Yer 18:20, 22 Wenye majivuno wananichimbia mashimo,
kinyume na sheria yako.
86 # Za 109:26; 7:1-5; 35:19; 119:78, 138 Amri zako zote ni za kuaminika;
unisaidie, kwa sababu watu wananishtaki bila sababu.
87 # Isa 1:4, 28; 59:13; 58:2; Za 119:150 Walikaribia kabisa kunifuta kutoka uso wa dunia,
lakini sijaacha mausia yako.
88 # Za 41:2; 119:2, 100, 124, 129, 134, 168; 51:1; 109:26 Yahifadhi maisha yangu sawasawa na upendo wako,
nami nitatii sheria za kinywa chako.
Imani Katika Sheria Ya Bwana
89 # Za 119:111, 144; 111:8; Isa 51:6; Mt 5:18; 1Pet 1:25 Ee Bwana, neno lako ni la milele,
linasimama imara mbinguni.
90 # Za 36:5; 45:17; 148:6; Ay 8:19 Uaminifu wako unaendelea kwa vizazi vyote,
umeiumba dunia, nayo inadumu.
91 # Yer 33:25; 31:35; Za 148:6; 104:2-4; Mwa 8:22 Sheria zako zinadumu hadi leo,
kwa kuwa vitu vyote vinakutumikia.
92 # Za 37:4, 5; 112:1; 119:50, 67; Rum 15:4 Kama nisingefurahia sheria yako,
ningeangamia katika taabu zangu.
93 # Za 119:83; 103:5 Sitasahau mausia yako kamwe,
kwa maana kwayo umehifadhi maisha yangu.
94 # Za 119:45, 146; 54:1; 116:4; Yer 17:14; 31:18; 42:11; Hos 2:7, 16 Uniokoe, kwa maana mimi ni wako,
kwa kuwa nimetafuta mausia yako.
95 # Za 69:4; 119:99 Waovu wanangojea kuniangamiza,
bali mimi ninatafakari sheria zako.
96 # Za 19:7; Isa 40:8; Mt 5:18 Katika ukamilifu wote ninaona mna kikomo,
lakini amri zako hazina mpaka.
Kuipenda Sheria Ya Bwana
97 # Za 1:2; 119:15, 47 Aha! Tazama, sheria yako naipenda mno ajabu.
Ninaitafakari mchana kutwa.
98 # 2Tim 3:17; Kum 4:6, 8; 19:7; Isa 48:17 Amri zako zimenipa hekima zaidi kuliko adui zangu,
kwa kuwa nimezishika daima.
99 # 2Tim 3:15; Za 119:15 Nina akili zaidi kuliko walimu wangu wote,
kwa kuwa ninatafakari juu ya sheria zako.
100 # Ay 12:12; 32:7; Za 119:56; Kum 6:17 Nina ufahamu zaidi kuliko wazee,
kwa kuwa ninayatii mausia yako.
101 # Mit 1:15; 2Kor 7:1; Za 119:57 Nimezuia miguu yangu isiende kwenye kila njia mbaya,
ili niweze kutii neno lako.
102 # Kum 17:20; 4:5 Sijaziacha sheria zako,
kwa kuwa umenifundisha wewe mwenyewe.
103 # Mit 24:13, 14; 8:11; Za 19:10 Tazama jinsi maneno yako yalivyo matamu kwangu,
matamu kuliko asali katika kinywa changu!
104 # Za 111:10; 119:7 Ninapata ufahamu kutoka mausia yako,
kwa hiyo ninachukia kila njia ya upotovu.
Nuru Kutoka Kwenye Sheria Ya Bwana
105 # Mit 6:23; 20:27; 2Pet 1:19; Za 119:130 Neno lako ni taa ya miguu yangu
na mwanga katika njia yangu.
106 # Neh 10:29; Za 119:7 Nimeapa na nimethibitisha,
kwamba nitafuata sheria zako za haki.
107 # Za 119:25 Nimeteseka sana, uhifadhi maisha yangu, Ee Bwana,
sawasawa na neno lako.
108 # Za 51:15; 109:30; 63:5; 119:64; 71:8; Ebr 13:15; Hos 14:2 Ee Bwana, pokea sifa za hiari za kinywa changu,
nifundishe sheria zako.
109 # Amu 12:3; Za 119:61; Ay 13:14 Ingawa maisha yangu yako hatarini siku zote,
sitasahau sheria yako.
110 # Za 25:15; 64:5; 119:10; Isa 8:14; Amo 3:5 Waovu wamenitegea mtego,
lakini sijayakiuka maagizo yako.
111 # Kum 33:4; Za 119:14, 162 Sheria zako ni urithi wangu milele,
naam ni furaha ya moyo wangu.
112 # Za 108:1; 119:33 Nimekusudia moyoni mwangu
kuyafuata maagizo yako mpaka mwisho.
Usalama Ndani Ya Sheria Ya Bwana
113 # 1Fal 18:21; Yak 1:8; 4:8; Za 119:47 Ninachukia watu wa nia mbili,
lakini ninapenda sheria yako.
114 # Za 18:2; 119:43; 32:7; Mwa 15:1 Wewe ni kimbilio langu na ngao yangu,
nimeweka tumaini langu katika neno lako.
115 # Za 6:8; Mt 7:23 Ondokeni kwangu, ninyi mtendao mabaya,
ili niweze kushika amri za Mungu wangu!
116 # Za 18:35; 41:3; 55:22; 119:41; Isa 46:4; Rum 5:5; 9:33 Nihifadhi sawasawa na ahadi yako, nami nitaishi;
usiache matumaini yangu yakavunjwa.
117 # Isa 41:10; 46:4; Za 34:4; 119:6; 71:6; Yn 10:28; Rum 14:4 Nitegemeze, nami nitaokolewa,
nami daima nitayaheshimu maagizo yako.
118 # Za 119:10 Unawakataa wote wanaoyaasi maagizo yako,
kwa maana udanganyifu wao ni bure.
119 # Isa 1:22, 25; Eze 18:19; Za 119:47 Waovu wa nchi unawatupa kama takataka,
kwa hivyo nazipenda sheria zako.
120 # Ay 4:14 Mwili wangu unatetemeka kwa kukuogopa wewe,
ninaziogopa sheria zako.
Kuitii Sheria Ya Bwana
121 # 2Sam 8:15; Ay 27:6 Nimetenda yaliyo haki na sawa,
usiniache mikononi mwa watesi wangu.
122 # Ay 17:3 Mhakikishie mtumishi wako usalama,
usiache wenye kiburi wanionee.
123 # Isa 38:14; Za 119:81, 82 Macho yangu yamefifia, yakitazamia wokovu wako,
na kuitazamia ahadi yako ya kweli.
124 # Za 119:12, 88; 25:7 Mfanyie mtumishi wako kulingana na upendo wako
na unifundishe maagizo yako.
125 # Za 116:16; 119:79 Mimi ni mtumishi wako; nipe ufahamu
ili niweze kuelewa sheria zako.
126 # Hes 15:31 Ee Bwana, wakati wako wa kutenda umewadia,
kwa kuwa sheria yako inavunjwa.
127 # Efe 3:8; Za 19:10; 119:47; Ay 3:21; Mit 3:13, 18; 8:11 Kwa sababu nazipenda amri zako zaidi ya dhahabu,
naam, zaidi ya dhahabu safi,
128 # Za 19:8; 31:6; 119:104, 163; Mit 13:5 na kwa sababu naona maagizo yako yote ni adili,
nachukia kila njia potovu.
Shauku Ya Kuitii Sheria Ya Bwana
129 # Za 119:18, 22, 88 Sheria zako ni za ajabu,
hivyo ninazitii.
130 # Za 119:105; 19:7, 10; Mit 1:4; 2Pet 1:19 Kuingia kwa maneno yako kunaleta nuru,
kunampa mjinga ufahamu.
131 # Za 42:1; 119:20 Nimefungua kinywa changu na kuhema,
nikitamani amri zako.
132 # 2Sam 24:14; Kut 4:31; Za 6:4; 9:13; 5:11; 106:4; 1Sam 1:11 Nigeukie na unihurumie, kama uwafanyiavyo siku zote
wale wanaolipenda jina lako.
133 # Kum 6:12; Za 119:9, 11, 122; Rum 6:16 Ongoza hatua zangu kulingana na neno lako,
usiache dhambi yoyote initawale.
134 # Lk 1:74; Za 119:56, 88, 122 Niokoe na uonevu wa wanadamu,
ili niweze kutii mausia yako.
135 # Hes 6:25; Za 4:6; 80:3; 4:6; 119:12 Mwangazie mtumishi wako uso wako
na unifundishe amri zako.
136 # Yer 9:1; 9:1, 18; 13:17; 14:17; Mao 1:16; 3:48; Isa 22:4; 42:24; Eze 9:4; Za 6:6; 119:158; 106:25 Chemchemi za machozi zinatiririka kutoka machoni yangu,
kwa kuwa sheria yako haifuatwi.
Haki Ya Sheria Ya Bwana
137 # Kut 9:27; Ezr 9:15; Neh 9:13, 33; Yer 12:1; Dan 9:7 Ee Bwana, wewe ni mwenye haki,
sheria zako ni sahihi.
138 # Za 119:75, 86; 19:7 Sheria ulizoziweka ni za haki,
ni za kuaminika kikamilifu.
139 # Za 69:9; Yn 2:17 Jitihada yangu imenidhoofisha, kwa kuwa adui zangu
wanayapuuza maneno yako.
140 # Yos 23:14; Za 12:6; 119:47 Ahadi zako zimejaribiwa kikamilifu,
mtumishi wako anazipenda.
141 # Za 22:6; 119:61, 134; Mit 15:16; Amo 7:2; Lk 6:20; 2Kor 8:9; Yak 2:5 Ingawa ni mdogo na ninadharauliwa,
sisahau mausia yako.
142 # Za 119:151, 160; 19:7, 9; Yn 17:17; Efe 1:3 Haki yako ni ya milele,
na sheria yako ni kweli.
143 # Za 119:24, 47 Shida na dhiki zimenipata,
lakini amri zako ni furaha yangu.
144 # Za 119:34 Sheria zako ni sahihi milele,
hunipa ufahamu ili nipate kuishi.
Maombi Kwa Ajili Ya Kuokolewa
145 # Za 119:10, 22, 55 Ee Bwana, ninakuita kwa moyo wangu wote,
nami nitayatii maagizo yako.
146 # Za 119:94 Ninakuita; niokoe
nami nitazishika sheria zako.
147 # Za 3:3; 57:8; 108:2 Ninaamka asubuhi na mapema na kukuomba msaada;
nimeweka tumaini langu katika neno lako.
148 # Za 63:6; 63:1, 6 Sikufumba macho yangu usiku kucha,
ili niweze kutafakari juu ya ahadi zako.
149 # Za 27:7; 124; 119:40 Usikie sauti yangu sawasawa na upendo wako,
Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na sheria zako.
150 # Za 37:7 Wale wanaopanga mipango miovu wako karibu nami,
lakini wako mbali na sheria yako.
151 # Flp 4:5; Za 34:18; 119:142; 145:18 Ee Bwana, hata hivyo wewe u karibu,
na amri zako zote ni za kweli.
152 # Za 119:7, 73, 89; 111:8; Lk 21:33 Tangu zamani nimejifunza kutoka shuhuda zako
kwamba umezithibitisha ili zidumu milele.
Maombi Kwa Ajili Ya Msaada
153 # Za 13:3; 3:7; 44:17; Mao 5:1 Yaangalie mateso yangu, uniokoe,
kwa kuwa sijasahau sheria yako.
154 # Za 119:24, 41; 35:1; 1Sam 24:15; Yer 50:34; Mik 7:9 Nitetee katika hali hii yangu na unikomboe,
uyahifadhi maisha yangu sawasawa na ahadi yako.
155 # Za 119:94, 118; Ay 5:4 Wokovu uko mbali na waovu,
kwa kuwa hawatafuti maagizo yako.
156 # Neh 9:27; Yak 5:11; Za 119:25, 149 Ee Bwana, huruma zako ni kuu,
uyahifadhi maisha yangu sawasawa na sheria zako.
157 # Za 7:1; 44:18 Adui wanaonitesa ni wengi,
lakini mimi sitaziacha sheria zako.
158 # Za 119:104, 136; Kut 32:19 Ninawatazama wasioamini kwa chuki,
kwa kuwa hawalitii neno lako.
159 # Za 119:25; 41:2 Tazama jinsi ninavyopenda mausia yako;
Ee Bwana, uyahifadhi maisha yangu, sawasawa na upendo wako.
160 # Za 119:89; 111:8 Maneno yako yote ni kweli,
sheria zako zote za haki ni za milele.
Kujiweka Wakfu Kwa Sheria Ya Bwana
161 # Za 119:23, 122, 157; 119:120; 1Sam 24:14-15 Watawala wamenitesa bila sababu,
lakini moyo wangu unatetemeka kwa neno lako.
162 # Za 119:25; 41:2 Nafurahia ahadi zako
kama mtu aliyepata mateka mengi.
163Ninachukia na kuchukizwa sana na uongo,
lakini napenda sheria yako.
164 # Za 119:111; 1Sam 30:16; Isa 9:3; 53:12 Ninakusifu mara saba kwa siku,
kwa ajili ya sheria zako za haki.
165 # Za 119:11; 37:11; 37:24; Isa 26:3, 12; 27:5; 32:17; 57:19; 66:12; 1Yn 2:10; Mit 3:2 Wanaopenda sheria yako wana amani tele,
wala hakuna kitu kinachoweza kuwakwaza.
166 # Za 119:81 Ee Bwana, ninangojea wokovu wako,
nami ninafuata amri zako,
167 # Za 119:47 Ninazitii sheria zako,
kwa sababu ninazipenda mno.
168 # Za 139:3; Ay 10:4; 23:10; Mit 5:21 Nimetii mausia yako na sheria zako,
kwa kuwa njia zangu zote zinajulikana kwako.
Kuomba Msaada
169 # Ay 16:18; Za 119:9, 34 Ee Bwana, kilio changu na kifike mbele zako,
nipe ufahamu sawasawa na neno lako.
170 # 1Fal 8:30; 2Nya 6:24; Za 28:2; 140:6; 143:1; 3:7; 22:20; 59:1; 119:41 Maombi yangu na yafike mbele zako,
niokoe sawasawa na ahadi yako.
171 # Za 51:15; 63:3; 94:12; Isa 2:3; Mik 4:2 Midomo yangu na ibubujike sifa,
kwa kuwa unanifundisha maagizo yako.
172 # Za 51:14; 119:7, 75 Ulimi wangu na uimbe kuhusu neno lako,
kwa kuwa amri zako zote ni za haki.
173 # Za 37:24; 73:23; Isa 41:10; Lk 10:42; Yos 24:22; Mit 1:29 Mkono wako uwe tayari kunisaidia,
kwa kuwa nimechagua mausia yako.
174 # Za 119:16, 24, 166 Ee Bwana, ninatamani wokovu wako,
na sheria yako ni furaha yangu.
175 # Za 119:116, 159; Isa 55:3 Nijalie kuishi ili nipate kukusifu,
na sheria zako zinitegemeze.
176 # Za 119:10; 95:10; Yer 50:17; Eze 34:11; Lk 15:4 Nimetangatanga kama kondoo aliyepotea.
Mtafute mtumishi wako,
kwa kuwa sijasahau amri zako.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014