120
Zaburi 120
Kuomba Msaada
Wimbo wa kwenda juu.
1 #
2Sam 22:7; Za 18:1; 118:5 Katika dhiki yangu namwita Bwana,
naye hunijibu.
2 #
Za 31:18; 52:4 Ee Bwana, uniokoe kutoka midomo ya uongo
na ndimi za udanganyifu.
3Atakufanyia nini,
au akufanyie nini zaidi, ewe ulimi mdanganyifu?
4 #
Kum 32:23
Atakuadhibu kwa mishale mikali ya shujaa,
kwa makaa yanayowaka ya mti wa mretemu.
5 #
Mwa 25:13; 2:10; Yer 2:10; 49:28; 1Sam 25:1 Ole wangu kwa kuwa naishi Mesheki,
kwamba naishi katikati ya hema za Kedari!
6Nimeishi muda mrefu mno
miongoni mwa wale wanaochukia amani.
7Mimi ni mtu wa amani;
lakini ninaposema, wao wanataka vita.