121
Zaburi 121
Bwana Mlinzi Wetu
Wimbo wa kwenda juu.
1Nayainua macho yangu nitazame vilima,
msaada wangu utatoka wapi?
2 #
Mwa 1:1; Za 104:5 Msaada wangu hutoka kwa Bwana,
Muumba wa mbingu na dunia.
3 #
1Sam 2:9; Isa 27:3 Hatauacha mguu wako uteleze,
yeye akulindaye hatasinzia,
4 #
Za 127:1
hakika, yeye alindaye Israeli
hatasinzia wala hatalala usingizi.
5 #
Za 1:6
Bwana anakulinda,
Bwana ni uvuli wako mkono wako wa kuume,
6 #
Isa 49:10
jua halitakudhuru mchana,
wala mwezi wakati wa usiku.
7 #
Za 9:9, 10; 91:9, 10; Ay 5:19; Mit 12:21 Bwana atakukinga na madhara yote,
atayalinda maisha yako,
8 #
Kum 28:6; Mit 2:8 Bwana atakulinda unapoingia na unapotoka,
tangu sasa na hata milele.