Zaburi 122
NEN

Zaburi 122

122
Zaburi 122
Sifa Kwa Yerusalemu
Wimbo wa kwenda juu. Wa Daudi.
1 # Isa 49:10; Yer 31:6; Zek 8:21 Nilishangilia pamoja na wale walioniambia,
“Twende nyumbani ya Bwana.”
2Ee Yerusalemu, miguu yetu imesimama
malangoni mwako.
3 # 2Sam 5:9; Efe 2:21 Yerusalemu imejengwa vyema kama mji
ambao umeshikamanishwa pamoja.
4 # Kum 16:16; Kut 16:34 Huko ndiko makabila hukwea,
makabila ya Bwana,
kulisifu jina la Bwana kulingana na maagizo
waliopewa Israeli.
5Huko viti vya enzi vya hukumu hukaa,
viti vya enzi vya nyumba ya Daudi.
6 # Za 26:8; Isa 62:6; Yer 51:50 Omba kwa ajili ya amani ya Yerusalemu:
“Wote wakupendao na wawe salama.
7 # 1Sam 25:6; Za 48:3 Amani na iwepo ndani ya kuta zako
na usalama ndani ya ngome zako.”
8Kwa ajili ya ndugu zangu na marafiki,
nitasema, “Amani iwe ndani yako.”
9 # Za 128:5 Kwa ajili ya nyumba ya Bwana Mungu wetu,
nitatafuta mafanikio yako.

Kiswahili Contemporary Version (Neno: Biblia Takatifu)

Copyright ©1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.® Used by permission.

All Rights Reserved Worldwide Printed.

Learn More About Neno: Bibilia Takatifu 2014